- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Enyi Majeshi ya Waislamu Je, Mnaiacha Gaza Pekee Yake katika Kukabiliana na Mayahudi na Makruseda?!”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliandaa matembezi yenye kichwa “Enyi Majeshi ya Waislamu Je, Mnaiacha Gaza Pekee Yake katika Kukabiliana na Mayahudi na Makruseda?!” baada ya swala ya Ijumaa kutoka Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu, ambayo yalipangwa kufika Al-Barabara ya Al-Thawra kama ilivyo kila Ijumaa. Ni matembezi ya 29 mfululizo baada ya zaidi ya siku 200 tangu vita vya mauaji ya halaiki vizuke dhidi ya Waislamu katika Ukanda wa Gaza katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina).
Wakati wa maandamano hayo, umati wa watu ulipiga takbira na tahlil muda wote wa matembezi hayo na kuinua mabango, ambayo la kwanza lilikuwa na kichwa cha matembezi hayo na mengine yalikuwa yameandikwa juu yake jumbe mbali mbali ambazo zilikuwa zikielekezwa kwa Umma wa Kiislamu na majeshi yake, miongoni mwazo “Enyi Majeshi ya Waislamu itikieni amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuinusuru Gaza” na “Umma Mmoja... Dola Moja... Jeshi Moja” na “Enyi Majeshi ya Waislamu: Ukombozi wa Palestina Unaanza kwa Kuwapindua Vibaraka... Unamalizika kwa Kuswali ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa”... na mtembezi hayo yalimazika kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb aliyotaja ndani yake kwamba sababu ya yanatojiri mjini Gaza ni Magharibi kafiri kuiondoa dola ambayo aliisimamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kwamba hakuna njia ya kuinusuru Gaza na Waislamu wanyonge wangine isipokuwa kwa kusimamishwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Na hivyo, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendeleza kuinusuru kwake Gaza ambapo mpaka sasa imeandaa matembezi 29 tangu kuzinduliwa cheche ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na ina nia ya kuuamsha Umma na majeshi yake hadi wasimamishe dola la Uislamu aliyowafaradhishia juu yao Mwenyezi Mungu, hivyo wawaokoe wanadamu wote kutokana na dhulma na jinai za Mayahudi na Magharibi Makruseda wa kuchukiza.
Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 17 Shawwal Al-Khair 1445 H sawia na 26 Aprili 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/3903.html#sigProIdb849d8c63f
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: