Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Angazo la Vyombo vya Habari la Kisimamo
Mabadiliko Makubwa kwa Msingi wa Uislamu Ndiyo Njia ya Wokovu Wetu!

Jumapili asubuhi, Mei 22, 2022, Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa kisimamo cha kukataa miradi ya kisiasa ya kisekula ambayo inaupinga Uislamu waziwazi na hukmu zake inayofungamana na maadui wa Waislamu kutoka katika ukoloni wa Magharibi na mfano wake. Kilikuwa chini ya kichwa: "Mabadiliko makubwa kwa msingi wa Uislamu ndiyo njia ya wokovu wetu!"

Ingawa kisimamo hicho kilipangwa katika Barabara ya Al-Thawra mbele ya ukumbi wa michezo wa Manispaa, vikosi vya usalama vilizingira eneo hilo na kuigeuza barabara kuu ya mji mkuu kuwa kambi ya jeshi, ambapo idadi kubwa ya vikosi vya polisi vilikusanyika na kuweka magari yao kwenye sehemu ndogo za viingilio vya barabara hii, ili barabara zote zinazoelekea kwenye ukumbi wa michezo wa Manispaa zifungike. Hata hivyo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir walikusanyika mwishoni mwa barabara hii kuu na wakafaulu kufanya kisimamo upande ulio karibu nayo. Hata hivyo, serikali hii, inayotoa usalama kwa Wazayuni, ilisisitiza kulizingira eneo hilo kutoka kila upande na kuwazuia watu kuwasili na kujiunga na kisimamo hicho, pamoja na kukamatwa kwa baadhi ya Mashababu wa hizb. Baadaye waliachiliwa.

Hata hivyo, Hizb ilitoa hotuba tatu, kama ifuatavyo:

Kwanza: Hotuba ya Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya Tunisia, Ustadh Khabib Karbaka, na ilikuwa ni hotuba moto baada ya mkanyagano uliotokea na vikosi vya usalama, ambapo Khabib alizungumzia usaliti uliofanywa na watawala wa Tunisia na dori ya serikali katika kuendeleza ufisadi na mfumo wake, na alilaumu jukumu zima la jamii ya kisiasa kwa hali nchini Tunisia kuwa chini ya maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na udhalilishaji wa watu wake.

Pili: Hotuba ya Ustadha Fatima Arous, ambapo alizungumzia kuhusu Uislamu wakati ulipokuwa ukitabikishwa na dola, na Waislamu kuishi katika kivuli chake kwa karne nyingi, ambapo hapakuwa na matatizo ya watu walio wachache au matatizo ya umasikini, ukosefu wa ajira na ugaidi, na hakukuwa na ugumu wa maisha kama huu tunaoulalamikia leo, kwa sababu ya kubadilishiwa mfumo uliotungwa na mwanadamu badala ya mfumo wa Mola wa walimwengu wote.

Alihitimisha hotuba yake kwa kutoa wito kwa watu wa Tunisia kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kuung'oa mfumo huu kutoka kwenye mizizi yake na kusimamisha mamlaka ya Uislamu yanayowaunganisha Waislamu chini ya bendera ya La Ilaha illa Allah.

Tatu: Hotuba ya Mkuu wa Kamati ya Kisiasa ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia, Ustadh Abdel Raouf Al Ameri, ambapo alitenganisha kwa uwazi haki na batili, ikisisitiza kwamba tunayoyapitia leo si mapambano ya kisiasa baina ya vyama, bali ushindani kati ya wanasiasa kutumikia ukoloni. Aliongeza kuwa "sababu kwa yale tuliyomo ndani yake ni kwamba jambo letu haliko mikononi mwetu, achilia mbali miongo kadhaa ya uingiliaji kati wa kigeni na kuibuka tabaka la kisiasa linalotawala na kuamrisha amri ya adui yetu mkoloni." Badala yake, "wanasiasa wote leo wanategemea mipango ya Magharibi, na hivi ndivyo ninavyotaka wawe wote kwa pamoja."

Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Kalima ya Ustadh Khabib Karbaka's
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Tunisia
Wakati wa Kisimamo

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu