Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tanzania: Amali kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah

Chini ya uongozi wa Amir wa Hizb ut-Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashta, Mwenyezi Mungu amhifadhi, Hizb ut-Tahrir amezindua kampeni pana ya kiulimwenguni kwa mnasaba wa kumbukumbu ya karne moja Hijria ya kuvunjwa kwa Khilafah, 28 Rajab al-Muharram 1442 H / 2021 M, na katika ukurasa huu, tutaangazia amali zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Tanzania ndani ya wigo wa kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Hizb.

Jumamosi, 01 Rajab 1442 H sawia na 13 Februari 2021 M

- Amali za Wiki ya Kwanza ya Mwezi wa Rajab -

Mashababu wa Hizb ut-Tahrir nchini Tanzania mnamo siku ya Jumamosi ya kwanza ya Rajab 1442 Hijria, sawia na 13 Februari 2021 M, waliandaa amali na maandamano baridi katika maeneo kadhaa kutangaza rasmi kampeni ya karne moja ya kuvunjwa kwa Khilafah mnamo Rajab 1342 H sawia na Machi 1924 M.

Kabla ya hapo, mnamo siku ya Ijumaa, 30 Jumada al-Akhira, na kutoka kwenye mimbari za swala ya Ijumaa, waliwahutubia watu katika misikiti anuwai kwa hotuba za hadhara za kupigia debe kampeni hii ya kiulimwengu. Na miongoni mwa maeneo ambayo kampeni hii ilizinduliwa jana: Dar es Salaam, nje ya Msikiti wa Kichangani (Majumini), Msikiti wa Mtoro (Kariakoo), Msikiti wa Idrissa (Kariakoo), Msikiti wa Nuru, Mbandi na Mbagala.

Na huko Zanzibar, misikiti ya Mchanjani na Mbuyuni (Zanzibar mjini) na msikiti wa Qatar Chake Chake (Kisiwa cha Pemba), pamoja na misikiti maarufu katika mikoa ya Mwanza na Tanga. Iliandaa visimamo pamoja na kalima fupi kuwakumbusha Waislamu juu ya uchungu na hali mbaya ambayo Ummah inateseka kwayo kwa sababu ya kukosekana kwa Khilafah, na jinsi Sharia ilivyo faradhisha juu ya Ummah kufanya kazi kuisimamisha tena, na ikawalingania watembee pamoja na Hizb ut-Tahrir, na wafanye kazi pamoja nayo na kuinusuru, kwa sababu ina uwezo wa kihakika wa kuukomboa Ummah kupitia Uislamu.

- Taarifa kwa Vyombo vya Habari -

Hizb ut Tahrir Tanzania Yazindua Kampeni ya Miaka 100 ya Kuangushwa Khilafah

Ili Kusoma Taarifa Hii Bonyeza Hapa

- Video -

[ Miji 100 Inatamka Neno Lake ] 

Khalil Ar-Rahman - Kabul - Zanzibar

Ijumaa, 21 Rajab Muharram 1442 H - 05 Machi 2021 M

[ Miji 100 Inatamka Neno Lake ] 

JawharLama - MaaratMasrin - Dar es Salaam

Jumamosi, 08 Rajab Muharram 1442 H - 20 Februari 2021 M

- Alama Ishara za Kampeni -

#أقيموا_الخلافة

ReturnTheKhilafah#

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Tanzania:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania

Ukurasa wa Face wa Hizb ut Tahrir / Tanzania

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Tanzania

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Tanzania

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Tanzania

Mkusanyiko wa Picha

Click to enlarge image 1 1.jpg

Click to open image!

 

 

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu