Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ripoti ya Habari 23/04/2022

Katika muendelezo wa amali za umma zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, ili kuuamsha Umma wa Kiislamu na kuimarisha azma yake ya kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida upya, kupitia kuunda rai jumla inayofahamu hukmu na masuluhisho ya Kiislamu, Hizb ilifanya amali nyingi za umma katika mikoa mbalimbali ya nchi, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwezi wa ugunguzi na ushindi.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Umdurman walifanya Iftar ya kila mwaka katika kijiji cha Al-Ikhlas mnamo tarehe 5 Ramadhan 1443 H sawia na Aprili 6, 2022 M. Ustadh Ahmed Abkar alihutubia umati mkubwa wa watu mara baada ya iftar, na akazungumzia fadhila za mwezi mtukufu wa Ramadhan, fadhila ya kufunga na kufanya kazi ndani yake, na kwamba saumu, swala, zaka na ibada zote za mtu binafsi zinawakilisha ushuri moja ya Uislamu. Ama ushuri tisa zengine za Uislamu, hutekelezwa tu na mamlaka, kama ilivyonukuliwa kutoka kwa Imam Ali, Mwenyezi Mungu amkrimu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Madani pia walifanya mkutano wa hadhara wenye anwani: Hizb ut Tahrir inawaalika mufanye kazi nayo ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume katika mwezi huu uliobarikiwa, katika ua wa Msikiti wa Al-Khatmiya katika Kisiwa cha El-Fil baada ya swala ya Taraweh mnamo tarehe 7 Ramadhan 1443 H - 8 Aprili 2022 M, Ustadh Siwar alieleza kuwa Ramadhan ni mwezi wa kujitolea mihanga, ushindi na ufunguzi, hivyo tunapaswa kuutumia kufanya kazi na Hizb ut Tahrir. Iko tayari, chini ya uongozi wa mwanachuoni wake mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, na mashababu wake waliotawanyika kote duniani. Inachokosa ni nyinyi tu kusimama pamoja nayo na kukusanyika pambizoni mwake hadi itoke kiapo cha utiifu kwa khalifa kwa Waislamu na kutatua masuala na matatizo yote ambayo Waislamu na dunia nzima wanakumbana nayo, ili Ummah huu uregee katika utukufu wake wa zamani kabla ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah Rashidun. Maingiliano yalikuwa mazuri, kwani takbira za hadhira zilienea kwenye hotuba, na mmoja wao ambaye machozi yalimlengalenga alitoa maoni, "Nyinyi ni Mashababu wa Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu akupeni nusra, kwa sababu mnafanya vitendo sawa na vitendo vya maswahaba, tuko pamoja nanyi licha ya uzee wetu."

Katikati ya hadhara ya adhama na msongamano mkubwa wa watu, kumbi za afisi ya Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan katika mji wa Gadharif zilipambwa kwa ajili ya kuwapokea wageni waheshimiwa kuitikia mwaliko wa hizb kuhudhuria iftar ya Ramadhan ya kila mwaka, mnamo Jumamosi 8 Ramadhan 1443 H - 9 Aprili 2022 M. Na pamoja nanyi mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake (saw) ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Iftar ilifuatiwa na kalima fupi zilizogundua ugonjwa na kubeba dawa. Katika kalima ya kwanza, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, alizungumza kuhusu mgogoro wa utawala nchini Sudan, ambao haujasimama tangu kuondoka kwa yule anayejiita mkoloni hadi leo, na kwamba utekelezaji wa mifumo iliyotungwa na binadamu, ya kiraia na kijeshi, haijatatua na haitatua mgogoro huo. Bali wao ni pande mbili za sarafu moja, na suluhisho na tiba yao ni kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Katika kalima ya pili, Ustadh Muhammad Al-Hassan Ahmed, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia kuhusu kung’ang’ania mamlaka, na kueleza kuwa mamlaka si nguvu, bali mamlaka ni kwa niaba ya Ummah katika kutabikisha hukmu za Uislamu, hivyo hakuna mtu awezaye kuyapata isipokuwa kwa kiapo cha utiifu, kwani hakuna mtu aliye mlinzi wa Ummah. Suluhisho la matatizo ya kung’ang’ania madaraka liko katika kanuni kuu ya Uislamu. Katika kalima ya tatu, Dkt. Ali Abdel Qader, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia sera ya kiuchumi katika dola ya Kiislamu, ambayo imejikita katika kuhakikisha kukidhi mahitaji ya kimsingi ya mwanadamu. Kwa kumalizia, Ustadh Al-Mahi Abdeen, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia uwezo wa Khilafah kutatua tatizo la umasikini, na kwamba umaskini ni matokeo ya utabikishaji wa mfumo wa kirasilimali, ambao umewaachilia watu wachache kuhodhi pesa na kudhibiti maisha ya watu, na kwamba Uislamu unadhamini uwiano wa kiuchumi baina ya jamii kwa kutekeleza hukmu za Shariah kwa raia wa dola, ambazo huzuia kulimbikiza pesa na kuzifanya zizunguke miongoni mwa watu wote. Hadhira iliingiliana vyema, huku wakiisifu hizb na kuthibitisha kuiunga mkono.

Ujumbe wa unaozuru kutoka Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kutoka Khartoum, hadi Gadharif, ulifanya mihadhara ya kina katika misikiti mikubwa ya mji, ikifuatiwa na idadi kubwa ya waumini. Ustadh Nassir Ridha (Abu Ridha) alitoa mhadhara katika Msikiti Mkuu wa Gadharif mnamo tarehe 8 Ramadhan 1443 H - Aprili 9 2022 M yenye kichwa: Ramadhan ni mwezi wa utiifu na ushindi, na juu ya mada hiyo hiyo na mnamo tarehe 9 Ramadhan 1443 H, Ustadh Muhammad Jameh (Abu Ayman) alitoa mhadhara katika Msikiti wa Abdul Qadir Abdul Mohsen katika Soko la Al-Gadharif, na Bwana Abdullah Abdul Hussein katika Msikiti Mkongwe wa mji wa miiba, ambapo mihadhara hii ilihusu utukufu wa mwezi huu mtukufu.

Ujumbe huo pia ulitembelea wanazuoni, viongozi, maimamu na watu mashuhuri katika jimbo la Gadharif.

Darsa mbalimbali zilitolewa katika misikiti tafauti tafauti katika maeneo tofauti.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu