Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan:

Ripoti ya Habari 07/02/2022

Amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ziliendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hii ili kujenga rai jumla yenye ufahamu kuhusu hukmu za Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na nidhamu tofauti tofauti za maisha. Amali hizo zilizungumzia mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa utawala na mpango wa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na mada nyenginezo...

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko El Obeid walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Januari 6, 2022 katika Uwanja wa Uhuru, ambapo Ustadh Abdul Rahim Muhammad Hasan alizungumza kuhusu kumhisabu mtawala.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat pia walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Januari 7, 2022 katika uwanja wa Msikiti wa Bilal bin Rabah huko Qadisiyah, baada ya Swala ya Ijumaa, yenye kichwa: Suluhisho katika Uislamu na Dola yake ya Khilafah, ambamo Ustadh Al-Fateh Abdullah alitaja kwamba demokrasia ambayo Magharibi Kafiri inaipigia upatu kwa nchi za Kiislamu. Ni nidhamu ya kikafiri, na haina uhusiano wowote na Uislamu.

Pia katika mji wa El-Obeid, mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walifanya mkao wao wa kila mwezi mnamo Jumamosi, Januari 8, 2022, katika afisi ya hizb mjini humo, uliopewa kichwa: Mgogoro wa Utawala nchini Sudan. Je, kuna mwanga mwishoni mwa handaki? Imam Muhammad Ibrahim alizungumza na kuashiria kuwa moja ya sababu za mgogoro wa kiutawala nchini Sudan ni mzozo baina ya vyama wa kupigania viti vya mamlaka bila ya kuwa na mpango wa kifikra unaowasilishwa kama mradi wa kujitoa katika mgogoro huo wa utawala nchini humo, kama ilivyolezwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu.

Chini ya mada: Kuziba Upeo wa Kisiasa na Kutoka kwenye Handaki, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayat Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi mnamo Januari 11, 2022 ambapo Ust. Ishaq Muhammad Husayn alirudia tafsiri ya Ibn Kathir ya Aya ambayo kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamuru watu kunapotokea mzozo waliregeshe suala hilo kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw).

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa mjini El-Obeid yenye kichwa: Uadui wa Makafiri dhidi ya Waislamu, mnamo Januari 13, 2022 katika Uwanja wa Uhuru, ambapo Muhammad Qoni alizungumza, akielezea uadui wa Makafiri dhidi ya Waislamu, akitolea mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyesema: Aliifuata dini yao, akieleza kwamba uadui wa makafiri ulianza tangu utume wa Mtume (saw) hadi walipoipindua dola ya Kiislamu nchini Uturuki na kufanya kazi ya kuichana chana kuwa vijidola vidogo vya kitaifa ambavyo dhamira yake ni kulinda maslahi ya nchi za kikoloni.

Katika muktadha wa mgogoro wa kisiasa nchini humu, Mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa mjini Gadharef mnamo Januari 13, 2022 chini ya mada: "Kutoka katika mgogoro wa kisiasa ni kwa kupitia kutekeleza Uislamu na sio mipango ya kimataifa.", ambapo Ust. Maysara Yahya alihutubia hadhira, akizungumza kuhusu mzozo unaoendelea katika ulingo wa kisiasa wa Sudan.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi pia walitoa hotuba ya kisiasa yenye kichwa: "Utiifu kwa makafiri ni haramu", katika Soko la Libya, mnamo Januari 18, 2022, Abd al-Rahim Abdullah alizungumza ambaye alieleza kwamba upande wa kijeshi na kiraia ulianguka mikononi mwa makafiri wa Kimagharibi. Na hayo yalikuwa kupitia wajumbe ambao uingiliaji kati wao haukuacha kuwepo nchini, na akabainisha utukufu wa yale yaliyo katika Shariah na akatoa wito kwa waliohudhuria kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

"Mnamwaga damu kwa ajili ya nini?" chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Omdurman Magharibi, mnamo Januari 25, 2022, walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya ambapo Babiker Mahdi (Abu Musab) alizungumza kuhusu damu inayomwagika nchini Sudan haswa na nchi za Kiislamu kwa jumla, huku akisisitiza kwamba wanamapinduzi walijitolea mhanga sana, lakini kwa ajili ya hadhara na mabadiliko ya kidemokrasia, ambayo yanagongana na Uislamu.

Vilevile ndani ya muundo wa uingiliaji kati wa kigeni, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la El Obeid walitoa hotuba ya kisiasa katika soko kubwa karibu na Msikiti wa Suwar al-Dhahab mnamo Januari 27, 2022, yenye kichwa: "Je, Umoja wa Mataifa unastahili kusuluhisha masuala ya Sudan?" Ahmed Wadaa alisema kuwa Umoja wa Mataifa ulioasisiwa mnamo Oktoba 24, 1945 kwa kutabanniwa hati ya kikatiba na wanachama watano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Amerika, Ufaransa, Uingereza, China na Urusi, na moja ya malengo ya kuanzishwa kwake kama wanavyodai kwamba unalenga kudumisha amani na usalama wa kimataifa na kuendeleza mahusiano ya Kimataifa kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa, kuunda kituo cha uratibu wa hatua za mataifa na kuzuia vita vya siku za usoni, kwa hakika kinyume chake ndio kweli.

Chini ya anwani: "Tumregelee nani kutatua matatizo yetu?" mnamo Februari 1, 2022, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Omdurman Magharibi, walitoa hotuba ya kisiasa katika Soko la Libya ambapo Ishaq Muhammad alizungumza.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika mji wa El Obeid, yenye mada: "Jukumu la Mtawala kwa Watu", mnamo Februari 3, 2022 karibu na Gold Soir Musala, ambapo Majzoub Abdel Rahman alizungumza.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu