Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina:

Maandamano ya Halaiki ya Hizb ut Tahrir ya Kuionya Al-Khalil juu ya Njama Chafu na Kuishutumu Mamlaka ya Palestina kwa Kushiriki katika Njama Hizo!

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina ilionya juu ya njama chafu ya kuishambulia Al-Khalil kwa kutumia mizozo ya kifamilia na kuibua taharuki kwa kuzifinika kwa kufiniko cha ukoo. Hizb iliishutumu Mamlaka hiyo kwa kushiriki katika mipango hii kwa kuwaficha wavamizi na washambuliaji na kutowashtaki au kuwakamata licha ya kuwafahamu.

Hayo yamejiri katika kisimamo cha halaiki kilicho andaliwa na Hizb mchana wa Jumamosi tarehe 20/11/2021 katikati ya mji wa Al-Khalil licha ya hali mbaya ya hewa ambapo maelfu ya watu walishiriki, na hotuba zikatolewa kuiwakilisha Hizb na nyengine kuwakilisha koo, Meya wa Al-Khalil na raisi wa Baraza la Wafanyabiashara.

Katika hotuba yake iliyotolewa na Dkt Ibrahim Al-Tamimi, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Hizb iliviona vitendo vya mauaji, kuchoma moto, hujuma na vitisho kuwa ni vitendo vilivyoharamishwa na vinatokana na hamasa za kijinga.

Alisisitiza, "Vitendo hivi vimetumiwa na kuchochewa na njama kubwa kuliko koo na tofauti zao, na tunaposema hivi tunamaanisha kila herufi ndani yake. Kwa hiyo, tunazionya familia kwa tahadhari kubwa dhidi ya wale wanaotumia hisia za wasiwasi miongoni mwa wanafamilia ili kuwasukuma kukiuka matukufu na kutumbukia katika damu iliyoharamishwa, na kuwafanya kuwa chombo cha maafa kwa mji huu." Hawahisi wala hawatambui ukubwa wa hatari yake na ukubwa wa ubaya na uovu wake, na tunaziambia familia kwamba wapo wanaotumia kifiniko cha familia kama njia ya kuzichana familia vipande vipande na kuvunja miiba yao na kutekeleza njama walizoamriwa, na hawa hutumia kwa njia chafu na mbaya ukiukaji wa uhalali na uhalifu ambao baadhi ya watu katika familia hufanya ili kuwafanya kufuata mipango hii Kutoka mahali wasipohisi."

Hizb iliishutumu Mamlaka hiyo kwa kushiriki katika njama, huku ikishangaa: Je, Mamlaka ya Palestina na vyombo vyake vya usalama wako na nia ya dhati ya kukomesha hali hii ya machafuko, au wanatoa hifadhi kwa wahalifu?!

Dondoo za Amali mjini Hebron [Khalil ar-Rahman]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu