Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan Kampeni kwa Kichwa

“Rudisheni Khilafah”
kwa mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuanguka Khilafah

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan imeandaa kampeni kwa kichwa “Rudisheni Khilafah” katika mitandao ya kijamii kwa mwezi mzima wa Rajab 1444 Hijri, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 102 ya kuanguka dola ya Kiislamu – Khilafah – kwa wakoloni makafiri.

Kwa mabadiliko ya kweli, kataeni demokrasia, simamisheni Khilafah!

Ewe Mola irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume… Allahuma Ameen!

#BringBackKhilafah

Jumatatu, 1 Rajab 1444 H - 23 Januari 2023 M

Bonyeza Hapa kwa Maelezo Zaidi

Mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijria, makafiri walikula njama na wasaliti kutoka kwa Waarabu na Waturuki ili kuiondoa ngao ya Ummah, Khilafah. Hii ndiyo siku ambayo Waislamu walikuwa kama mayatima, bila ya mlezi wa kuwachunga.

Jumatatu, 1 Rajab 1444 H - 23 Januari 2023 M

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ  amesema, إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ ، يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ ، وَيُتَّقَى بِهِ “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao (Waislamu) hupigana nyuma yake, na hujihami kwake.” (Muslim) Tangu 28 Rajab 1342 Hijri hadi sasa, Waislamu wamenyimwa ngao hii.

Jumanne, 2 Rajab 1444 H - 24 Januari 2023 M

Baada ya kuvunjwa kwa Khilafah inayounganisha, wakati wa Rajab, Waislamu walidhoofishwa na mgawanyiko katika makumi ya dola ndogo ndogo, kupitia sumu ya utaifa.

Jumatano, 3 Rajab 1444 H - 25 Januari 2023 M

Rajab aliona ushindi wa jeshi la Kiislamu dhidi ya Warumi huko Tabuk, kutokana na hofu pekee. Majeshi ya Khilafah yataandamana katika kutafuta ushindi na kufa kishahidi hivi karibuni, inshaaAllah.

Alhamisi, 4 Rajab 1444 H - 26 Januari 2023 M

Rajab ni mwezi wa Israa na Miraj ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ. Msikiti wa Al-Aqswa leo hii unakaliwa na adui makafiri, licha ya kuwa Ummah una mamilioni ya askari walio tayari na wenye uwezo. Ummah unamngoja mtawala wake mwenye kuuunganisha, Khalifa.

Ijumaa, 5 Rajab 1444 H - 27 Januari 2023 M

Wakati wa Rajab, Sultan Salah ud-Din al-Ayyubi aliongoza majeshi ya Khilafah, kuikomboa Al-Quds, kutoka kwa Makruseda. Je, ni kamanda yupi wa kijeshi ataukomboa Msikiti wa Al-Aqsa leo?

Jumamosi, 6 Rajab 1444 H - 28 Januari 2023 M

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ تَكْثُرُ “Na hakika yake hakutakuwa na Mtume mwengine baada yangu, lakini kutakuwepo na Makhalifa na watakuwa ni wengi...” [Muslim]. Hivyo basi katika kila zama, Waislamu lazima watawaliwe na Khalifa, anayehukumu kwa Uislamu.

Jumapili, 7 Rajab 1444 H - 29 Januari 2023 M

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema,  فَالأَمِيرُ الَّذِى عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ“Na Iman (mtawala wa Kiislamu) anayewatawala watu ni mchungaji na yeye ni mwenye kuulizwa juu ya raia wake…” [Bukhari]. Katika Uislamu, mamlaka, nguvu na utawala ni amana. Yeyote asiyehukumu kwa Shariah, amekhini amana hiyo.

Jumatatu, 8 Rajab 1444 H - 30 Januari 2023 M

Katika mfumo wa sasa wa kiliberali, wa kirasilimali, kila mzazi ana wasiwasi juu ya malezi ya watoto wake. Khilafah itakomesha ushawishi wa maadili haribifu ya Kimagharibi kwa familia na watoto wetu. Itawafanya kustawi chini ya mwongozo wa malezi ya Uislamu.

Jumanne, 9 Rajab 1444 H - 31 Januari 2023 M

Uislamu unachunga mambo yote ya Waislamu kupitia mfumo wake wa utawala. Mfumo tawala wa Uislamu ni Khilafah. Sio tu kwamba Khilafah ililinda ibada yetu binafsi kwa Mwenyezi Mungu , bali ilihakikisha kwamba tunamtii Mwenyezi Mungu kama mujtamaa na dola.

Jumatano, 10 Rajab 1444 H - 01 Februari 2023 M

Khalifa wa Waislamu atahamasisha vyombo vyote vya dola, vikiwemo vyombo vya habari na elimu, kukanusha kikamilifu mawazo potofu ya hadhara ya Kikafiri ya Kimagharibi, huku akifafanua utukufu wa Dini ya Haki.

Alhamisi, 11 Rajab 1444 H - 02 Februari 2023 M

Khilafah ilihakikisha Uislamu ulikuwa ndio hadhara inayotawala duniani kwa karne nyingi. Itafanya hivyo tena hivi karibuni inshaa Allah

Ijumaa, 12 Rajab 1444 H - 03 Februari 2023 M

Khilafah itazileta Ardhi zote za Kiislamu kuwa dola moja, na kufidia udhaifu wa eneo moja kwa nguvu ya eneo jengine, iwe udhaifu huo ni wa kiuchumi au wa kijeshi, na kuugeuza Ummah kuwa nguvu ya kimataifa.

Jumamosi, 13 Rajab 1444 H - 04 Februari 2023 M

Umma wa Kiislamu umo katikati ya ulimwengu na ndio nguvu kuu ya asili ya Eurasia. Khilafah itaunganisha Ummah mzima kutoka Indonesia hadi Morocco kuwa dola moja kubwa yenye nguvu.

Jumapili, 14 Rajab 1444 H - 05 Februari 2023 M

Khilafah ni njia ya Shariah ya utabikishaji Uislamu kama njia mfumo kamili wa maisha, kuhakikisha elimu, uchumi, vyombo vya habari, maadili ya familia, mahakama na utawala wetu ni kwa mujibu wa Uislamu.

Jumatatu, 15 Rajab 1444 H - 06 Februari 2023 M

Iwe urais au ubunge, Demokrasia inatufanya watumwa wa sheria zilizotungwa na mwanadamu. Khilafah inatukomboa kupitia hukmu za Shariah, zinazotokana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume.

Jumanne, 16 Rajab 1444 H - 07 Februari 2023 M

Wakati majeshi ya Kiislamu yanapounganishwa chini ya uongozi mmoja wa kisiasa, kama Khilafah, maadui makafiri wenye uadui wataogopa mzozo. Kisha, mambo ya ulimwengu yataongozwa na Khalifa.

Jumatano, 17 Rajab 1444 H - 08 Februari 2023 M

Khilafah iliilinda Palestina kwa karne nyingi. Haikuzungumza kamwe juu ya maridhiano au kugawanya ardhi pamoja na makafiri wanaoikalia kimabavu. Badala yake, Khilafah ilihakikisha kukombolewa kwa Al-Masjid Al-Aqswa kutoka kwenye kukaliwa kimabavu na makruseda. Ni Khilafah ndiyo itakayozikomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.

Alhamisi, 18 Rajab 1444 H - 09 Februari 2023 M

Khilafah ilihakikisha upanuzi wa haraka wa Uislamu, na kufungua ardhi mpya kwa nuru ya Dini ya Mwenyezi Mungu , kuingia Ulaya, Magharibi, na China, Mashariki.

Ijumaa, 19 Rajab 1444 H - 10 Februari 2023 M

Mtume wa Mwenyezi Mungu  amesema, ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ   “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha yeye  akanyamaza.” [Ahmad]

Jumamosi, 20 Rajab 1444 H - 11 Februari 2023 M

[وَعَدَ اللّٰهُ الَّذِیْنَ اٰمَنُوْا مِنْكُمْ وَ عَمِلُوا الصّٰلِحٰتِ لَیَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِی الْاَرْضِ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi.” (Surah An-Noor 24: 55)

Jumapili, 21 Rajab 1444 H - 12 Februari 2023 M

Sa'ad bin Mu'adh (ra) alikuwa kamanda wa kijeshi, ambaye alitoa msaada wa kijeshi (Nusrah) kwa ajili ya utawala wa Kiislamu. Malaika waliibeba Janazah yake, huku Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu kikitikisika kwa furaha baada ya kuipokea roho yake.

Jumatatu, 22 Rajab 1444 H - 13 Februari 2023 M

Wapiganaji wa Madina walipata cheo cha Answaar kwa kutoa msaada wao wa kijeshi (Nussrah) kwa Uislamu, hivyo kwamba tuzo yao ni Jannah. Maafisa wa kijeshi lazima wasonge mbele sasa, bila ya matamanio au visingizio vya kidunia, kutafuta Jannah, ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wema.

Jumanne, 23 Rajab 1444 H - 14 Februari 2023 M

Wapiganaji Maansar (ra) walitoa msaada wa kijeshi (Nussrah) kwa ajili ya kusimamisha utawala wa Kiislamu. Ni maafisa gani wa kijeshi watakaotoa Nussrah yao kwa ajili ya Khilafah leo?

Jumatano, 24 Rajab 1444 H - 15 Februari 2023 M

Leo dunia ina aina mbili za watu. Kuna wanaoamini kuwa Khilafah itasimama mara tu Mwenyezi Mungu atakapotoa Nusra yake, na wengine wataamini mara tu watakapoiona.

Alhamisi, 25 Rajab 1444 H - 16 Februari 2023 M

Nusra (Ushindi) ya Mwenyezi Mungu haimaanishi kwamba Khilafah itashuka kutoka mbinguni, ikibebwa na Malaika. Tumewajibishwa na Mwenyezi Mungu kufanya kazi ya kusimamisha utawala wa Dini yake.

Ijumaa, 26 Rajab 1444 H - 17 Februari 2023 M

Rizq (riziki) iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu ﷻ pekee, lakini Uislamu unatuwajibisha kufanya sa’ee (juhudi) ya kuchuma. Vile vile, Nusra (Ushindi) uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu ﷻ, lakini tunawajibika kufanya juhudi ili kuipata.

Jumamosi, 27 Rajab 1444 H - 18 Februari 2023 M

Na kuvunjwa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijria, iwe ni ukumbusho mchungu wa hitajio la dharura la kusimamishwa tena.

Jumapili, 28 Rajab 1444 H - 19 Februari 2023 M

Fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambacho ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa duniani kinacho fanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah na ambacho kimeanzisha harakati ya kiulimwengu kwa ajili ya kuasisiwa kwake.

Jumatatu, 29 Rajab 1444 H - 20 Februari 2023 M

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah #TurudisheniKhilafah
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
أقيموا_الخلافة# كيف_تقام_الخلافة#
#YenidenHilafet #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu