Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Austria:

Nusra kwa Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!

Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Austria katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”kuwanusuru ndugu na dada zetu wafungwa wa kisiasa kwenye magereza maovu ya Uzbekistan kwa sababu tu wanasema [Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu].

Jumatano, 11 Muharram 1446 H sawia na 17 Julai 2024 M

Siku ya Jumatano, tarehe 11 Muharram Tukufu 1446 H sawia na 17/7/2024 M, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir ukiongozwa na Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb katika nchi zinazozungumza Kijerumani, mhandisi Shaker Assem, ulikwenda kwa ubalozi wa Uzbekistan jijini Vienna kutoa hati ya kulaani dhidi ya kukamatwa tena kwa mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan baada ya kutumikia kifungo chao chote cha takriban miaka 20. Ujumbe huo ulipokelewa na mfanyakazi wa ubalozi.

Mkuu wa ujumbe aliitambulisha hizb na kueleza kuwa ni harakati ya kifikra na kisiasa tu na haijishughulishi na shughuli zozote za kimada.

Kinyume chake, hizb inakataa vurugu kama njia ya kufikia malengo yake na inajitahidi kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume katika nchi za Kiislamu. Kwa hivyo, ni kosa kubwa kwa serikali ya Uzbekistan kuainisha Hizb ut Tahrir kama shirika la kigaidi ili tu kuzifurahisha nchi za kikoloni kama vile Urusi. Pia ni jambo lisilokubalika kabisa kwa mashababu hao baada ya kukamatwa tena kuwasilishwa kwa ushahidi wa uongo ili kutia kusaini, na kutishiwa kubakwa kwa wake zao na kukamatwa kwa watoto wao ikiwa watakataa kusaini.

Mfanyakazi wa ubalozi huo aliahidi kutuma hati hiyo kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uzbekistan, hivyo wajumbe hao walimshukuru kwa hilo na kumaliza mkutano huo kwa salamu za Kiislamu.

Jumatano, 11 Muharram Tukufu 1446 H sawia na 17 Julai 2024 M

Alama Ishara za Kampeni

#صرخة_من_أوزبيكستان

#PleaFromUzbekistan

#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu