- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Kitengo cha Wanawake “Kongamano la Kimataifa la Wanawake: Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”
Mwaka mzima umepita tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vikali vilivyofuata huko Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wa Gaza wamevumilia mitihani mikubwa, wakiishi katika machungu, mateso, na majanga yasiyohesabika: kuhamishwa, mauaji, njaa... mabaki yaliyotawanyika ya watoto na wanawake yaliyokusanywa kwenye mifuko, na mashahidi walionaswa chini ya vifusi, wasiowezekani kutolewa, na kuongeza katika maumivu na huzuni kutokana na kushindwa kuwaheshimu na kuwazika. Mauaji ya kikatili ya halaiki yanafanywa na umbile halifu kwa mtazamo kamili wa ulimwengu ambao unashiriki na kupuuza. Hata hivyo, licha ya mikasa na majonzi ya vita hivi, vimejaa mafunzo na tafakari zinazotolewa na kundi aminifu, vumilivu na thabiti linalosimama kidete dhidi ya njama za maadui na khiyana za watawala na wale wanaodai kuwa marafiki. Kundi hili dogo, bila kukatishwa tamaa na wale waliowatelekeza, linabaki stahimilivu, bila kupoteza kamwe tumaini la ushindi wa Mola wa mbingu na ardhi. Licha ya vilio, maombi, na wito wa kuomba msaada kutoka kwa watu wa Gaza, majibu yamefichua na kudhihirisha usaliti wa watawala wa Waislamu ambao wamekaa kwenye viti vyao vya utawala, viziwi, mabubu na vipofu kwa uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile hilo halifu dhidi ya watu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Watawala hawa wamejitolea kuonyesha uaminifu na utiifu kwake, kuhalalisha mahusiano nalo, na kuimarisha uwepo wake.
Vita hivyo pia vimewafichua sura za wanazuoni wengi, na kuwafichua wakweli kutoka kwa wadanganyifu. Vimefunua pazia machoni, vikionyesha ukweli wa kile kinachotokea. Asili ya halisi ya mzozo wa Palestina imekuwa wazi: mapambano kati ya haki na batili, kati ya Waislamu wa Palestina na umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, nyakuzi, la kikafiri. Ndiyo, watu wa Palestina kwa jumla, na hasa Gaza, wameuita Ummah. Hivyo, je jibu lilikuwaje?! Lilikuwa dhaifu, likidhihirika katika maandamano machache, au kususia baadhi ya taasisi na maduka yanayounga mkono umbile hilo, au kutuma chakula na nguo kama msaada! Licha ya umbile hilo vamizi kuendelea kutekeleza uhalifu wa kivita mmoja baada ya mwingine, na licha ya maombi yote hayo yanayokaririwa, vilio vya kuomba msaada, na matukio ya kuhuzunisha, kimya cha dunia nzima, usaliti wa serikali, kimya cha Umma wa Kiislamu na majeshi yake, na ukosefu wao wa kuchukua hatua yamekuwa, na bado yangali, kama majibu yao!
Haya yote yanazua maswali kuhusu sababu za kuzuia kumalizika kwa mauaji haya ya halaiki na ukombozi wa Palestina! Je, ni suluhisho gani la msingi ambalo kwalo kadhia hii inaweza kutatuliwa milele? Maswali haya na mengine yatashughulikiwa na kujibiwa mnamo Jumamosi, Oktoba 5, 2024, wakati wa kongamano la kimataifa la wanawake la mtandaoni lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote duniani, chini ya kichwa: “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema” Kongamano hili litaainisha njia sahihi ya kutatua kadhia hii na mambo mengine yanayohusu Umma wa Kiislamu. Litaangazia nukta muhimu za kadhia ya Palestina na kutoa suluhu zinazohitajika ili kukomesha mateso ya watu wa Palestina na Waislamu kwa jumla, kwa kuzingatia kuwa ni kadhia ya Ummah mzima na sio kadhia ya kitaifa inayofungamana na mipaka bandia iliyoundwa na dola za kikoloni. Wazungumzaji kutoka Palestina, Tunisia, Syria, Lebanon, Indonesia, na Amerika watashiriki. Kongamano hili litawafichua wale wanaozuia kumalizika kwa mauaji hayo ya halaiki, kufafanua sababu za kuzuia kukombolewa Palestina kutoka kwa Mayahudi, na kujadili dori ya taasisi za kimataifa na maamuzi yao katika kula jama dhidi ya kadhia ya Palestina. Zaidi ya hayo, litazungumzia dori ovu ya vyombo vya habari katika kupotosha na kuficha ukweli, na kuionyesha kama ni kadhia ya kitaifa au ya kikabila, ili kuwapotosha Waislamu kutoka kwenye njia sahihi ambayo wanapaswa kufuata ili kuitatua kimsingi.
Kongamano hili pia litazungumzia dori ya Umma wa Kiislamu katika kufikia suluhisho hili la kimsingi, ambalo lazima litoke kwenye Aqida (itikadi yake). Litaangazia kwamba masuluhisho yaliyopandikizwa na maadui na wakoloni ni silaha tu zinazotumiwa kuupiga vita Ummah, kuupotosha kutoka kwenye njia sahihi. Masuluhisho ya kivipande na ya muda yanayopendekezwa si chochote zaidi ya njia ya kuutia ganzi Ummah, kuuzuia kuchukua dori ambayo lazima uicheze. Kongamano hilo pia litaelezea vikwazo vinavyowazuia watu kutabanni ruwaza ya Kisharia kwa ajili ya ukombozi wa Palestina, na litafafanua kwa nini majeshi yanasalia katika kambi zao, kutoitikia wito wa mara kwa mara wa kuchukua hatua.
Zaidi ya hayo, kongamano hilo litafichua juhudi zinazolenga kupanua mwanya kati ya Ummah na majeshi yake kwa kuyaonyesha majeshi hayo kuwa hayana nguvu, tiifu kwa tawala, na hayana uwezo wa kutoa nusra au ushindi. Madai na tuhma hizi zitakanushwa kwa kutoa mifano ya watu wenye ikhlasi ndani ya jeshi waliojitolea mhanga kwa ajili ya dini yao na ushindi wake, na kubainisha dori ya ufahamu na rai jumla katika kuwahamasisha watu wengi wenye ikhlasi katika majeshi kuchukua hatua.
Aidha, kongamano hilo litafichua sababu msingi zilizo nyuma ya kuweka mzigo wa kukomboa ardhi takatifu kwa watu wa Palestina pekee, huku zikificha mjadala kuhusu dori ya Umma na majeshi yake, ambayo yana vifaa vya kutosha na yako tayari.
Kongamano hilo pia litaangazia dori ya kila Muislamu katika kutatua kadhia hii, kwa kuzingatia makhsusi wanawake wa Kiislamu na hatua wanazopaswa kuchukua ili kuchangia kukomesha mauaji ya halaiki na uchinjaji unaofanywa dhidi ya watu wetu wa Gaza na Palestina kwa jumla. Litasisitiza wajibu wao wa kufanya kazi pamoja na wengine wanaopigania ukombozi wake. Kongamano hilo litasisitiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi na tamkini, na kutukumbusha kwamba faraja huja baada ya dhiki, na kwamba ushindi hufuata mitihani. Litasisitiza tena utukufu wa Ummah huu, wenye uwezo wa kupata ushindi Inshallah.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba kongamano hili litaangaza njia sahihi ambayo Ummah unapaswa kuchukua ili kuregesha tena mamlaka yake, uongozi, na kufikia ukombozi wa Palestina kutoka mikononi mwa maadui na makafari. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu:
[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj:40].
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Jumatano, 22 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 25 Septemba 2024 M
[Video za Amali ya Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Kuinusuru Gaza]
Jumamosi, 2 Rabi’ ul-Akhir 1446 H sawia na 05 Oktoba 2024 M
- Utangulizi -
Ukombozi wa Palestina … Changamoto na Bishara Njema
- Mada ya Kwanza -
Vikwazo vya ukombozi wa Palestina!
- Video iliyoonyeshwa Wakati wa Kongamano -
[Khiyana ya Watawala]
- Mada ya Pili -
Dori ya Umma wa Kiislamu katika Kutatua Kadhia ya Palestina kwa njia ya Kimsingi!
- Mada ya Tatu -
Pindi Wakiomba Msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu Kuwasaidia
- Video iliyoonyeshwa wakati wa Kongamano -
[Nguvu za Majeshi ya Waislamu na Uwezo Wao]
- Mada ya Nne -
Dori ya Wanawake na Wengine miongoni mwa Watoto wa Umma katika Kukomesha Mauaji na Ukaliaji Kimabavu!
- Mada ya Tano -
Matumaini yapo na Hakuna Kukata Tamaa na Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Bishara Njema ya Mtume wake ﷺ
- Video iliyoonyeshwa wakati wa Kongamano -
[Risala kwa Umma Kiislamu: “Umma Bora uliotolewa kwa Watu”]
- Kipindi cha Maingiliano na Kuhitimisha -
Video ya Ualishi wa Kongamano
Mialiko ya Kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake Kuinusuru Gaza
[Mwaliko kutoka Lebanon]
Kushiriki katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake
Mtandaoni chini ya kichwa “Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”
Kwa kuzingatia aqida iliyoijaalia Gaza na Palestina yote kuwa jiji kuu la Waislamu na kito katika taji la Umma huu, na kuifanya kuwa mwana wa Mashariki na Magharibi yenye kushuhudia huku tukishuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, imewafanya wote kuwa watu wa kadhia hii na wenye kuulizwa kuhusu Palestina na pia watu wake, na hata zaidi. Kwa kuzingatia shahada hii tukufu, ambayo imetufanya sisi sote, bila kuzingatia makabila yetu mbalimbali, jinsia, na nchi, ndugu katika imani, na fungamano hili la pekee likawa ni lenye nguvu na la kudumu, tunapaswa kufanya nini kama Waislamu ili kuinusuru Gaza? Kama wanawake wa Kiislamu, vipi tutainusuru Gaza? Haya ndiyo tutakayoyaweka wazi na kuyafafanua katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir duniani. Tunakualikeni kutoka Lebanon kufuatilia shughuli za kongamano hili chini ya kichwa “Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema” siku ya Jumamosi, 5 Oktoba 2024.
Saa kumi kamili jioni, kwa saa za Madina Al-munawwara, hivyo basi fikeni kwa wakati.
Alhamisi, 23 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 26 Septemba 2024 M
[Mwaliko kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina]
Kushiriki katika kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lenye kichwa: Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema!
Baada ya zaidi ya miezi 10 ya mauaji ya kikatili, kuhamishwa, njaa, utekaji nyara na mateso, Je, ni nani atakayekomesha chuki hizi nyeusi? Je, vita vitaisha baada ya kuangamizwa kwa Gaza? Nani atatunusuri Palestina na kutuzuia na ushenzi wa umbile la Kiyahudi? Je, Palestina itakombolewa kupitia makubaliano na mikataba? Je, Umoja wa Mataifa na taasisi zake kuanzia Baraza la Usalama na Mahakama ya Kimataifa ya Haki sio zilizowapongeza wauaji? Je, tunaamini hatua zake, maamuzi na masuluhisho yake? Nani ataondoa dhulma dhidi yetu na kukomesha uadui huu? Haya ni maswali ambayo yapo akilini mwa kila mmoja wetu, na tutayajibu, Mwenyezi Mungu akipenda, katika kongamano la kimataifa la wanawake Mtandaoni... linaloandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kushirikiana na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote duniani, kuweni kwa wakati.
Jumamosi, 25 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 28 Septemba 2024 M
[Mwaliko kutoka Tunisia]
Kushiriki katika kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni linaloitwa:
Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema!
Je, kadhia ya Palestina imekuwa mujarrad wa idadi na takwimu tu?
Je, tumezoea mauaji na kuridhika na kilio cha muda mfupi kisha tukarudi kwenye mahangaiko yetu ya kila siku kana kwamba hakuna kilichotokea?
Je, Umma umekabidhiwa kheri yake, au ni dhaifu na hauna udhibiti wa mambo yake?
Maswali haya yote na mengine mutayapata majibu yake ya kutosha na ya kuridhisha.
Sisi, kutoka Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, tunakualikeni kuhudhuria kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut
Tahrir kote ulimwenguni kwa kichwa: “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema”... Hivyo kuweni kwa wakati.
Ijumaa, 01 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 04 Oktoba 2024 M
[Mwaliko kutoka Australia]
Kushiriki katika kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lenye kichwa:
Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema!
Licha ya usaliti na uhalalisha mahusiano, licha ya khiyana na utelekezwaji wa Ardhi ya Palestina, ambayo ni amana mikononi mwa Waislamu wote na hakuna mtu anayeweza kutoa hata shubiri moja kwa maadui wa Mwenyezi Mungu, je, kuna matumaini baada ya maumivu haya? Je, umbile la Kiyahudi linakaribia kutoweka? Je, kuna watu wenye nguvu na uwezo ambao wana ikhlasi na watakuwa wenye kuunusuru dini hii kama vile Answari walivyokuwa wenye kunusuru Uislamu na kuwaongoza Waislamu kwenye viwanja vya izza na ushindi? Haya ndiyo tutakayoyapata katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake chini ya kichwa “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema... Basi kuweni kwa wakati.”
Jumatano, 29 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 02 Oktoba 2024 M
[Mwaliko kutoka Indonesia]
Kushiriki katika kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lenye kichwa:
Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema!
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambaye amesema, “Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwengine, hamdhulumu, wala hamdharau”. Kutoka Indonesia.. Tunawezaje kufikia maana ya mwili mmoja na tuwanusru watu wa Palestina? Ni nani anayetelekeza jihad ili kulinda uvamizi dhidi ya Umma na kumtoa adui katika nchi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu? Je, mipaka ya Sykes-Picot inaondoa wajibu wa majeshi ya Waislamu wa kuinusuru Palestina? Je, kukusanya majeshi na kuikomboa Al-Aqsa ni jambo la uhalisia au haliwezekani? Tutajadili maswali haya yote, Mwenyezi Mungu akipenda, katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake chini ya kichwa “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema... Isikupiteni kheri hii.”
Jumatatu, 27 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 30 Septemba 2024 M
Ili kuhifadhi nafasi katika ukumbi wa mikutano:
https://us06web.zoom.us/j/81685047416
Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na:
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Mapendekezo
*Maeneo ni machache kwa hivyo tafadhali jisajili mapema ili kupata nafasi yako katikahafla hii muhimu
* Kushiriki ni kwa wanawake pekee
* Hotuba za kongamano zitakuwa kwa lugha ya Kiarabu
(Kuingia katika ukumbi wa mikutano ni kuanzia saa 15:30 Alasiri kwa saa za Madina Al-Munawwara)
Wito kwa Majeshi
Kutoka kwa kina Mama, Mabinti na Dada wa Umma wa Kiislamu
ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)!
Wanawake wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanawataka watoto katika majeshi ya Kiislamu kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu katika kuwalinda Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na najisi ya umbile la Kiyahudi linaokalia kwa mabavu, na kukomboa kila shubiri ya Ardhi hii Iliyobarikiwa kutoka kwa makucha ya uvamizi huu wa kikatili.
Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M
[Wito wa haraka]
Kutoka kwa kina Mama wa Kiislamu... kwenda kwa Majeshi ya Nchi za Kiislamu!
Jumatano, 29 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 02 Oktoba 2024 M
Kusoma Taarifa ya Kitengo cha Wanawake
ambayo ilitangaza Kongamano la Kimataifa la Wanawake lenye kichwa:
“Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”
Kongamano la Kimataifa la Wanawake la Mtandaoni kuhusu Palestina lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir duniani kote
Jumatano, 22 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 25 Septemba 2024 M
Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha Wanawake
Barua ya Wazi
Kwa kina Mama wa Watu wenye Nguvu katika majeshi ya Kiislamu, Wake zao, Dada zao na Binti zao
Jumamosi, 18 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 21 Septemba 2024 M
Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha Wanawake
Ujumbe wa wazi kutoka kwa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
kwa Majeshi ya Waislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)
Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M
Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha wanawake
Barua ya wazi kwa Watu wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu
Kutoka kwa kina Mama, Dada na Mabinti wa Umma wa Kiislamu ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)
Jumanne, 14 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 17 Septemba 2024 M
Alama Ishara za Kongamano
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Bonyeza Kufuatilia kwa Lugha Nyenginezo
Mabango, picha na vitu kutoka katika Kongamano la Kimataifa la Wanawake
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/afisi-kuu-ya-habari/4211.html#sigProId56e3652d8f