Jumapili, 05 Rajab 1446 | 2025/01/05
Saa hii ni: 11:44:29 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 025
M.  Jumanne, 17 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Barua ya Wazi kwa Watu Wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu

Kutoka kwa kina Mama, Dada na Mabinti wa Ummah wa Kiislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Huu ni ujumbe kwa ndugu zetu, baba zetu na watoto wetu wanyoofu katika majeshi ya nchi za Kiislamu kutoka kwa wanawake wa Umma huu mtukufu wa Kiislamu. Tunakuhutubieni kama wale ambao wamepewa wajibu na Mola wa Walimwengu wote (swt) kuwalinda Waislamu na kulinda heshima yetu. Tunakuhutubieni kama watu wenye uwezo wa kukomesha mauaji ya Ummah wetu. Tunakuhutubieni kama wale ambao ni warithi wa Khalid bin Walid (RA), Salahuddin Ayubi (RH), Muhammad bin Qasim (RH) na makamanda wengine wakubwa wa Kiislamu wa zamani. Tunaomba kwamba maneno yetu yafike masikioni na kufungua nyoyo za wale miongoni mwenu wanaotaka kukumbatia urithi mtukufu wa mashujaa hawa watukufu wa Uislamu.

Tunajua uchungu wenu mnaposhuhudia mauaji yasiyokwisha ya kaka na dada zenu huko Gaza na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Tunahisi hasira zenu mnapoona mauaji baada ya mauaji, kaburi baada ya kaburi la watu wengi, na safu baada ya safu ya miili iliyofunikwa Sanda (Kaffan). Tunajua kwamba mayowe ya wanawake, watoto wadogo na wachanga walio na hofu kubwa ambao nyumba zao zimepigwa mabomu au waliozikwa kwenye vifusi vinakutesa akilini, na kwamba machozi ya kina mama wanaoomboleza na watoto yatima yanazichana nafsi zenu. Hatuna shaka kwamba damu yenu inachemka mnapoiona Al-Aqsa inanajisiwa na majeshi ya Kiyahudi na walowezi na dada zenu waheshimiwa wakidhulumiwa na kushambuliwa mitaani na katika jela za uvamizi huo, na kwamba munaunguzwa na hamu ya kuja kuwasaidia. Na tunajua kwamba moyo wenu unadunda pamoja na wetu kwa Palestina.

Basi kwa nini hamuitikii vilio vya wanawake na watoto wa ardhi hii iliyobarikiwa wanaokuiteni kuwakomboa kutoka katika uvamizi huu wa kikatili wa Kizayuni na maangamizi, wakati Mwenyezi Mungu (swt) anasema, ﴿وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُLakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal:72]? Je, mutaendelea kubaki kivulini hadi lini huku Ummah wenu ukiteseka na ardhi ya Masra, safari ya usiku ya kipenzi chenu Mtume (saw) inanajisiwa? Ni maelfu ngapi zaidi wanapaswa kuuawa, ni watoto wangapi zaidi wanapaswa kuchomwa moto wakiwa hai, ni watoto wangapi zaidi watakufa kwa njaa na kiu kabla ya kusonga dhidi ya umbile hili la mauaji? Vipi mutasimama tuli hali Ummah wenu unaangamizwa? Hamjayaona ya kutosha? Je, ni jambo gani zaidi mnalohitaji kushuhudia kabla hamjainuka na kutekeleza wajibu wenu wa Kiislamu wa kuwa watetezi na wakombozi wa Ummah wenu? Iko wapi Imani yenu, hisia zenu za heshima, hisia zenu za uungwana? Je, Mtume wenu (saw) hakusema «لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ» “Kuangamia kwa dunia ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuuliwa Muislamu mmoja?” Kwa hiyo, ni nini ambacho munasubiri? Ni nyinyi pekee ndio wenye uwezo wa kimada - vifaru, ndege, risasi, askari - kutokomeza saratani hii ya uvamizi na kukomesha umwagaji damu huu na jinamizi hili lililopo milele! Inatosha sasa! Ikiwa matukio haya ya kutisha hayakusukumini, basi mutasukumwa lini?!!

Enyi Wanajeshi Wanyoofu wa Majeshi ya Waislamu! Wako wapi watu wajasiri miongoni mwenu ambao watakuja kusaidia Ummah wenu? Wako wapi watu wa heshima kutoka miongoni mwenu ambao watatetea utu wa dada zenu? Wako wapi wanaume miongoni mwenu wanaotaka kupata hadhi kubwa ya kuikomboa Al Aqsa? Mafunzo yenu yote, silaha zenu, nguvu zenu za kijeshi ni za nini kama si kwa ajili ya kulinda Ummah wenu na kukomboa ardhi zetu? Ikiwa dola za Magharibi zimeunganisha silaha na mali zao ili kulinusuru umbile la Kiyahudi na mauaji ya halaiki, basi je, sio kwa majeshi ya nchi za Kiislamu kuungana ili kuwaokoa ndugu zao na umwagaji damu huu? Mnajua kwamba usitishaji mapigano hautamaliza mauaji haya ya muda mrefu ya miongo saba na Nakba. Mnajua kuwa mauaji, machungu na mateso ya Waislamu wa Palestina hayatakuwa na mwisho bila nyinyi kukusanya nguvu zenu za kijeshi ili kuikomboa ardhi yote ya Palestina kutokana na uvamizi huu wa mauaji wa kinyama.

Enyi Wana wa Majeshi ya Waislamu! Mtamjibu nini Mola (Rabb) wenu (swt) atakapokuulizeni kwa nini mlisimama tisti na hali Ummah wenu ulikuwa ukiuliwa kwa halaiki, dada zenu wakivunjiwa heshima na ardhi ya Al-Aqsa ikinajisiwa, na hali Yeye ameweka faradhi ya Kiislamu juu ya shingo zenu ya kuulinda Ummah wenu na kukomboa ardhi zake? What will you say when He (swt) asks you, ﴿وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa: 75]? Basi mcheni Mwenyezi Mungu (swt) kabla hamjachelewa, na jiandaeni kwa ajili ya siku mtakayosimama mbele ya Mola wenu Mlezi, na mlalamishi wenu ni mtoto wa Gaza au miongoni mwa wanawake wake watukufu, akisema: Ewe Mola Mlezi, watu hawa waliniangusha ilhali walikuwa na uwezo wa kunisaidia!’

Enyi Maafisa Wanyofu wa Majeshi ya Waislamu! Mumeona kuwa hakuna dola, hakuna uongozi, hakuna mtawala, hakuna taasisi ya kimataifa leo ambayo ina utashi wa kisiasa wa kulinda damu za Waislamu au kusimama kwa maslahi yetu. Ndugu zetu wa Palestina pia wametelekezwa na tawala saliti za ardhi za Kiislamu ambazo zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kizayuni kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki, hata kulipatia mafuta kuwakisha mashini yake ya vita na kulisambazia chakula huku watoto wa Gaza wakiwa na njaa. Watawala na tawala hizi vibaraka zilizopandikizwa na nchi za Magharibi na zenye kutumikia Magharibi zimetumika kama walinzi wa mstari wa mbele kwa umbile hili la mauaji na kuzuia harakati zozote dhidi yake. Vile vile wamesimama kama walinzi wa mipaka bandia ya kitaifa iliyowekwa na serikali za kikoloni juu ya ardhi zetu za Kiislamu ili kuwagawanya Waislamu na kuwazuia kwenda kuwasaidia ndugu zenu na dada zenu wanaokaa katika ardhi tofauti na yenu, ilhali Mwenyezi Mungu (swt) anasema, ﴿إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya: 92].

Enyi Wana wa Majeshi ya Waislamu! Mnawezaje kukubali kuwatumikia watawala hawa wanaowaunga mkono Mayahudi ambao wameifanya kazi yao kuwa kuwasaliti Waislamu, na ambao wameutelekeza Ummah wenu na Dini yenu? Vipi mutawapa utiifu wale ambao walikuwa na mazoea ya kuwafedhehesha Waislamu na kulivunjia heshima jina lenu kwa kukufungeni minyororo kwenye kambi zenu huku Ummah wenu ukivuja damu? Je, ni kiasi gani cha uoga na usaliti wao muko tayari kuuvumilia wakati wameonyesha wazi uaminifu wao kwa umbile la Kiyahudi na wafadhili wake wa kikoloni wa Magharibi? Watawala na tawala hizi zimekutumieni kuegemeza viti vyao vya utawala au kupigana vita kwa niaba ya mabwana zao wa Magharibi na maslahi yao huku wakikataa kuhamasisha askari hata mmoja kuwatetea Waislamu wanaodhulumiwa! Hawajawahi na kamwe hawatatoa amri kwenu kuutetea Ummah wenu! Kamwe hatutapata ushindi huko Palestina au dhidi ya adui yetu yeyote chini ya utawala unaoendelea wa watawala na tawala hizi saliti na mifumo yao fisadi ya kitaifa iliyobuniwa na mwanadamu ambayo inaambukiza ardhi zetu na kumomonyoa fungamano la udugu wa Kiislamu. Wanahitaji kuondolewa na badala yake kubadilishwa kwa uongozi wa Kiislamu na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) - Khilafah kwa njia ya Utume ambayo ni mchungaji, mlinzi na ngao ya Waislamu, kama ilivyoelezwa na Mtume wetu kipenzi (saw) aliyesema, «الْإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam (Khalifa) ni mchungaji na anawajibikia raia wake,” na «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam pekee (Khalifah) ni ngao ambayo nyuma yake mnapigana na mnajilinda kwaye.”

Ni Khilafah pekee ndiyo itakayokuhamasisheni kutekeleza dori yenu ya kweli kama watetezi, wakombozi na walinzi wa Umma na Dini yenu kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyokuamrisheni. Ni chini ya dola hii ambapo jenerali mtukufu wa Kiislamu wa karne ya 8 Muhammad ibn Qasim (RH) alitumwa kwenda kuwaokoa kundi la wanawake wa Kiislamu waliotekwa mateka na mfalme dhalimu wa Kibaniani, Raja Dahir, na kuiweka Sind chini ya utawala wa Uislamu katika mchakato huo. Ni chini ya dola hii ambapo Khalifa wa karne ya 9, al-Mutassim bi’llah alituma jeshi kubwa kwenda kumuokoa mwanamke mmoja wa Kiislamu huko Amuriyah, Uturuki ambaye alitekwa na Warumi. Ni chini ya dola hii ambapo ardhi ya al-Sham ilikombolewa kutoka kwa makruseda na kamanda mtukutu Salahuddin Ayyubi. Na ni chini ya Khilafah ambapo Ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina itakombolewa kwa mara nyingine tena, na bendera ya Uislamu itapandishwa juu ya Al-Quds kama mji mkuu wa Khilafah Rashida ya pili Biidhnillah!

Enyi Watu Wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu! Kama wanawake wa Umma huu mtukufu wa Kiislamu, tunatoa wito kwenu, tukisihi Imani yenu na hali ya heshima! Inukeni na mupindue viti vya watawala hawa wasaliti waoga na futeni mipaka hii batili ya ukoloni yenye kugawanya kati ya ardhi zetu, na tembeeni hadi Al Quds kwa ajili ya kuwalinda mama zenu na watoto wenu wa Palestina. Igeni matendo ya kamanda mkuu wa Khilafah ya Umayyah, Qutayba ibn Muslim, ambaye aliwakamata wale waliowatia hofu wanawake wa Kiislamu na kukataa hazina za dhahabu na fedha zilizotolewa na wakosaji kama fidia ya maisha yao, akitangaza maneno yake maarufu: “Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, je mwanamke wa Kiislamu atahangaishwa kwa ajili yenu”! Tunakulinganieni muwaondoe watawala hawa dhalimu na tawala ambazo hazijaleta chochote isipokuwa kukata tamaa na uhdalilifu kwa Ummah huu na kukuzuieni kutekeleza dori yenu ya kweli ya watetezi wa Waislamu. Kateni minyororo ya utawala wao dhalimu na toeni Nusrah yako (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha uongozi wa Kiislamu na mfumo wa Khilafah ambao utawaunganisha Waislamu chini ya mfumo na dola moja inayotekeleza Amri za Mola (Rabb) wenu (swt). Itakuhamasisheni kukomboa kila shubiri ya ardhi ya Waislamu inayokaliwa kwa mabavu na kuwalinda Waislamu, bila kujali wanaishi wapi, na kukufanyeni mashujaa wa Ummah wenu na kuleta heshima kwa jina lenu.

Enyi Askari Wanyoofu wa Majeshi ya Waislamu! Ni nini kinakuzuieni musinyanyuke kwenye wajibu wenu, na hali ima ni ushindi au Shahada tu yanayomngoja yule anayepigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt)? Tunakuombeni mutafakari yale yatakayoandikwa kukuhusuni katika kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na yale yatakayoandikwa kukuhusuni katika kurasa za historia? Je, mtatajwa kuwa ni wenye nyoyo dhaifu na wasio na heshima, au mtakuwa miongoni mwa wale walioiga mashujaa watukufu na viongozi wa Kiislamu, wakikumbatia urithi wa kupata ushindi mkubwa kwa Ummah wenu na Dini yenu?

Enyi Wana Wanyoofu wa Majeshi ya Waislamu! Wakati umefika wa nyinyi kusimama pamoja na Ummah wenu na dhidi ya maadui zake! Wakati umefika wa kuchukua msimamo dhidi ya watawala hawa wasaliti waliochafua jina lenu! Wakati umefika wa kuchukua nafasi yenu kama watetezi wa Waislamu na Dini yenu. Utiifu wenu ni kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), Dini yenu na Waislamu - sio kwa tawala hizi ambazo zimeuza nafsi zao kwa mabwana zao wa Magharibi! Kinachotokea Palestina leo ni vita dhidi ya Aqidah yenu, vita vya msalaba dhidi ya Uislamu na Ummah wenu ambapo mataifa ya Ukafiri yameungana kuunga mkono umbile hili poraji. Kwa hivyo ni vita vyenu! Kwa hiyo mumetoa nini kwa ajili ya Dini yenu?!! Tunakuulizeni, ni nani kati yenu anayetaka kukumbatia heshima kubwa duniani na malipo matukufu kesho Akhera ya kuwa ndiye aliyeikomboa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina? Tunakuulizeni, ni yupi kati yenu anayetaka kuwa Answari wa leo kwa kutoa Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili, na kupata utukufu wa Saad bin Muadh (ra) Biidhnillah, ambaye Malaika 70,000 walihudhuria Janaza yake - hadhi kubwa aliyopewa yule ambaye alitoa nusra yake ya kijeshi kwa ajili ya kusimamisha dola ya Kiislamu mjini Madina al-Munawwarah?

Matarajio ya Ummah huu yako juu yenu! Tuko nyuma yenu! Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nanyi. Basi itikieni Amri ya Mola (Rabb) wenu (swt), na ni ushindi unaokungojeni, Biidhnillah. Kwa hiyo, ni kipi mnachokisubiri? Msichelewe! Wakati wa kuchukua hatua ni sasa!

﴿وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاء وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ * وَعْدَ اللهِ لَا يُخْلِفُ اللهُ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui.” [Ar-Rum: 4-6]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu