Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Afisi Kuu ya Habari, kupitia ukurasa huu, itachapisha mabango kumi ya kuuamsha Umma wa Kiislamu na watu wenye nguvu na ulinzi ndani yake ili wafanye kazi pamoja nayo kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Bango jipya litachapishwa kila Ijumaa asubuhi. Tukimuomba Mwenyezi Mungu afungue haki kati yetu na watu wetu.

Ewe Mwenyezi Mungu ziunganishe nyoyo za Waislamu na utujumuishe chini ya moyo wa mtu mmoja (Khalifa Muongofu) unayempenda na anayekupenda, tunayempenda na anayetupenda, atuhukumu kwa kitabu chako na Sunnah ya Mtume wako, Hakika wewe ni muweza juu ya kila kitu... Allahumma Amin.

Ijumaa, 20 Shawwal 1443 H sawia na 20 Mei 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Kwanza -

Enyi Umma wa Kiislamu: Ni lazima muachane na muzishambulie fikra za Kimagharibi na mupambane na kila anayezikuuza, na mutangaze hadharani kwamba mnataka Uislamu utabikishwe na utekelezwe katika utawala, jamii na dola, na munataka kuunganisha nchi zenu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na munaitaka Hizb ut Tahrir ikuongozeni katika hilo.

Ijumaa, 20 Shawwal 1443 H sawia na 20 Mei 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Pili -

Enyi Umma wa Kiislamu: Ni wajibu juu ya kila mmoja wenu auelewe Uislamu kwa ufahamu sahihi na wenye utambuzi na atende kwa mujibu wa hukmu zake katika yale yanayomhusu yeye binafsi, kundi, watu wenye ujuzi na utaalamu, jeshi, vyombo vya utawala na idara, na katika kila nyanja ya maisha, na kwamba kila mmoja wa watoto wenu wa ajiandae kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha dola ya Khilafah.

Ijumaa, 27 Shawwal 1443 H sawia na 27 Mei 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Tatu -

Enyi Umma mtukufu: Hamna budi juu yenu kufupisha wakati, kwa maana wakati sio tena wa majadiliano, mabishano na uhasama, bali ni wakati wa vitendo vizito na vya makusudio, ili kugeuza uhalisia unaouma na mchungu, na kuweka uhalisia wote chini ya hukmu za sheria ya Uislamu, ili kutibu matatizo na migogoro yote kwa mujibu wake (fikra na njia) na kutafuta msaada wa wataalamu ili kuweka mipango, mbinu na njia zinazohitajika za kuondoa mateso na masaibu ya Umma.

Ijumaa, 04 Dhul Qa’adah 1443 H sawia na 03 Juni 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Nne -

Enyi Umma wa Kiislamu: Hakika Hizb ut Tahrir ni kiongozi mwaminifu, mtambuzi na mwenye uwezo wa kuuongoza Umma na dola na kutatua matatizo yote yaliyotokana na mfumo mbovu wa kirasilimali, na kwa sababu ya dola za kikoloni na zana zao miongoni mwa wasaliti na vibaraka. Basi ni wajibu juu yenu muipe Hizb uongozi mara moja ili ikuongozeni kwenye izza na heshima kwa kusimamisha Khilafah Rashida na kuunganisha nchi na waja.

Ijumaa, 11 Dhul-Qa’adah 1443 H sawia na 10 Juni 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Tano -

Enyi Umma wa Kiislamu: Hakika wakati wenu ni dhahabu, bali ni ghali zaidi kuliko dhahabu, na fursa inapatikana kwa mabadiliko ya kina katika nchi zote za Kiislamu. Hamupaswi kupurukushwa na chochote isipokuwa kufanya kazi ya kuyasukuma majeshi yenu yote yasongee kwa haraka kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Ijumaa, 18 Dhul-Qa’adah 1443 H sawia na 17 Juni 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Sita -

Enyi Watu wenye Nguvu na Ulinzi: lazima muelewe hukmu za kisheria zinazohusiana na jihad ili mpate furaha duniani na akhera. Ni wajibu juu yenu kuinusuru Hizb ut-Tahrir na kuikabidhi utawala ili kutekeleza katiba iliyoitayarisha kivitendo, na kuitegemea katika kuelewa siasa za kimataifa, na katika kuuelewa Uislamu kwa usahihi, na katika utabikishaji wake mzuri.

Ijumaa, 25 Dhul-Qa’adah 1443 H sawia na 24 Juni 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Saba -

Enyi Watu wenye Nguvu na Ulinzi: ni lazima mujiandae kujiepusha na hatari za ndani na nje kutoka kwa Waislamu na nchi zao, kwani mipango muhimu ya ndani na nje lazima ichorwe ili kukabiliana na hatari na kujiandaa kwa vita ikibidi. Ni wajibu juu yenu muelewe hali ya ndani ya nchi na hali ya nje ili kukabiliana na hatari zote kwa nchi na waja.

Ijumaa, 02 Dhul-Hijjah 1443 H sawia na 01 Julai 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Nane –

Enyi Watu wa Nguvu na Ulinzi: Nyinyi ndio mnaojua zaidi hali ya nchi na uingiliaji wa ukoloni katika mambo yake yote, na kwamba vibaraka ndio sababu ya kutawala kwa kafiri mkoloni Magharibi juu ya nchi za Waislamu. Hivyo, ni lazima muwasage sage wasaliti na vibaraka hawa, geuzeni uhalisia na zuieni balozi za kigeni kutokana na kuingilia mambo ya nchi, na tatueni mambo yake na muitakase dola kutokana na wasaliti, vibaraka, taasisi na mashirika yenye uhusiano na Magharibi.

Ijumaa, 09 Dhul-Hijjah 1443 H sawia na 08 Julai 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Tisa -

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi: nyinyi ni Waislamu na mnajua Uislamu unawajibisha nini kuziondoa tawala za kikafiri na watawala wasaliti na duru za kisiasa, kijeshi na nyinginezo zinazohusishwa na makafiri wakoloni, na kuwaleta wenye utambuzi na ikhlasi ili kuwabadilisha na kuuweka Uislamu katika utabikishaji.

Ijumaa, 16 Dhul-Hijjah 1443 H sawia na 15 Julai 2022 M

[Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir]

Hizb ut Tahrir Yawahamasisheni

Kufanya Kazi Nayo ili Kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume

- Bango la Kumi -

Enyi Watu wenye Nguvu na Ulinzi: Umma wa Kiislamu unahitaji pakubwa kuutabikisha na kuutekeleza Uislamu kivitendo, na kwamba njia pekee ya kutoka katika mahandaki ya giza ambayo Umma wa Kiislamu umewekwa ndani yake ni kwa kupatikana Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume itakayounganisha Umma mzima wa Kiislamu, basi inawapasa juu yenu kuweka mipango, mbinu na njia zinazohitajika kwa mifumo ya utawala na kukabidhi utawala kwa kiongozi wa Umma Hizb ut-Tahrir.

Ijumaa, 23 Dhul-Hijjah 1443 H sawia na 22 Julai 2022 M

- Alama Ishara za Kampeni -

#أقيموا_الخلافة

ReturnTheKhilafah#

#YenidenHilafet

#الخلافة_101

- Fuatilia Mabango kwa Lugha Nyenginezo -

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu