Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

#WaacheniHuruDadaZetu #MwacheniHuruDadaRomana #MwacheniHuruDktRoshan

Watawala waovu wa Pakistan wanaendelea kuwalazimisha vibaraka wa Amerika nchini Pakistan na kuwalazimisha juu ya shingo za Waislamu, hususan wanachama na wafuasi wa Hizb ut Tahrir, sasa imechukua hatua kakamavu zaidi katika mbinu zao ovu kuteka nyara wanawake!

Jana, Dada Romana Hussein, mwalimu maarufu aliye na shahada ya uzamifu katika masomo ya Kiislamu, alitekwa nyara. Mnamo usiku wa Jumatatu 13/08/2018 asasi za usalama za Pakistan zilivamia nyumba ya Dkt. Roshan na kumteka nyara yeye na mumewe, yote haya ni kwa sababu tu anasema Mola wetu ni Allah … ambapo wamesahahu au kujifanya kusahau maneno ya Allah Al-Aziz:

 [إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

Hakika wale waliowafitini Waumini wa kiume na waumini wa kike kisha wasitubie, basi hao watapata adhabu ya Moto wa Jahannam na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al-Buruj 85:10]. RasulAllah (saw) asema, «ومن عادى أولياء الله فقد بارز الله بالمحاربة» “Na yeyote anaye onyesha uadui kwa vipenzi (Awliya) vya Allah basi hakika ametangaza vita na Allah.” (Hakim ameisimulia kuwa Sahih kutoka kwa Mu'adh bin Jabal. Na katika Hadith Qudsi, imesimuliwa,

“Amesema Mtume wa Allah (saw) kwamba Allah amesema, '‘Yeyote anaye onyesha uadui kwa kipenzi changu basi Mimi nimemtangazia vita …” [Bukhari].

Twambuomba Allah amwachilie #DadaRomana na #DadaRoshan na mumewe, twamuomba Allah awaadhibu madhalimu wao!

Kutokana na vitendo hivi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imeanzisha kampeni ya kimataifa kwa anwani: #WaacheniHuruDadaZetu #MwacheniHuruDadaRomana #MwacheniHuruDktRoshan katika kujibisha vitendo vya wahalifu hao wa serikali ya Pakistan dhidi ya wanawake hawa dhaifu wa Kiislamu na kufanya kazi kwa bidii pamoja na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Enyi Waislamu, tunawakaribisha kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kwa njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha Dola, hii ndio njia ya haki ya kupata radhi na Ridhwan ya Allah (swt). Allah (swt) asema: 

 [ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini, muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume wake anapo kuiteni jambo la kukupeni uzima wa milele.    Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa” [Al-Anfal: 24]

Ewe Allah, tunakuomba nusra yako na ulinzi wako kwa Dada yetu Romana na Dada yetu Roshan na mumewe katika hifadhi yako na wafungwa wote wa Kiislamu walio magerezani mwa madhalimu. Ewe Allah, tunakuomba uilete ile siku ambayo Waislamu watakuwa na utawala wa Kiislamu duniani na kuwaadhibu wale waliowashambulia vijana na mabinti wa Ummah wetu, Ameen.

 Fuatilia Kampeni kwa Lugha Nyingine

 


Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 01 Agosti 2020 13:37

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu