- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Uchomaji kwa Nguvu wa Maiti za Waathiriwa wa Kiislamu wa COVID-19 Nchini Sri Lanka; Vipi Tunapaswa Kujibu?!
Majadiliano ya Paneli
Mnamo Aprili mwaka huu, serikali ya Sri Lanka ilitoa kanuni inayoamuru kwamba wale wote wanaokufa kutokana na Covid-19 au ambao walipatikana na virusi hivyo baada ya kifo wanapaswa kuchomwa moto, bila kujali imani zao za kidini, wakitaja wasiwasi usio na msingi wa afya ya umma kama sababu yao ya sera hii. Tangu Aprili, Waislamu kadhaa nchini Sri Lanka wamechomwa moto. Inaeleweka, kuna hofu kubwa ndani ya jamii ya Waislamu nchini Sri Lanka leo, ambao wamekabiliwa na vurugu, uchafuzi wa majina na ubaguzi ndani ya jamii kwa miaka mingi. Sasa, hawawezi hata kutekeleza ibada za mwisho za kidini za wapendwa wao kwa amani. Majadiliano haya ya paneli yanazungumzia jinsi Waislamu wanapaswa kujibu sera hii dhidi ya Waislamu na vile vile aina anuwai za dhulma ambazo Waislamu nchini Sri Lanka wamekuwa wakiteseka kwa miaka mingi.
Jumamosi, 04 Jumada al-Awwal 1442 H - 19 Disemba 2020 M