Jumanne, 24 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa kutenganisha Darfur, Hizb ilifanya Visimamo katika miji kadhaa ya Sudan

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa Marekani wa kuichana nchi hii kwa kuitenganisha Darfur na Sudan, hizb ilifanya kisimamo katika Msikiti wa Al-Aqit mjini Gadharef mnamo siku ya Alhamisi, Septemba 11, 2025 baada ya swala ya Ijumaa Septemba 12, 2025, miji kadhaa mikubwa ya Sudan ilifanyika visimamo, pamoja na misikiti mikuu ya Sudan yote. Shawak, Singa, Rabak, Madani, Abbasiya, Taqli, Khartoum (Kalakila na Dukhainat), na misikiti miwili mjini Omdurman.

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Sudan Wilayah – Mji wa Kosti, Jimbo la White Nile Wakutana na Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party katika Jimbo la White Nile

Mnamo Ijumaa, 12 Septemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ulimtembelea Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party, katika Uwanja wa Azraq Taiba huko Kosti.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Mkakati wa Amerika na Suluhisho la Dola Mbili

Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai?

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”

Mnamo Ijumaa, 22 Agosti 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia chini ya kichwa, “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”

Soma zaidi...

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari mnamo Jumamosi, 22 Safar 1447 H sawia na 16/08/2025 M, yenye kichwa: “Wito kwa Watu wa Sudan... Ikamateni Darfur Ili Isiungane na Kusini”

Mnamo Jumamosi, 26/7/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilitangaza kuundwa kwa serikali sambamba na serikali iliyopo nchini Sudan, katika mji mkuu wa Darfur Kusini (Nyala). Hatua hii ya RSF ni hatua ya juu katika kutenganisha eneo la Darfur, ambalo inalidhibiti, isipokuwa sehemu za mji wa El Fasher, ambao mzingiro wa kukandamiza umewekwa juu yake kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kuanzisha mashambulizi mfululizo dhidi yake ili kuuangusha, ili eneo zima la Darfur liwe chini ya udhibiti wake.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Matukio nchini Armenia na Azerbaijan

Uwepo wa Urusi katika Caucasus Kusini umetikiswa “kufuatia Armenia na Azerbaijan kutia saini tamko la pamoja na Marekani juu ya suluhisho la amani na makubaliano katika maeneo ya biashara na usalama baada ya mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka 35 kati ya nchi hizo mbili jirani...” (Al Jazeera, 15/8/2025). Azerbaijan na Armenia zilitoa taarifa ya pamoja mnamo tarehe 11/8/2025, kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini kati yao jijini Washington mnamo tarehe 8/8/2025, yakizitaka pande nyingine kufunga Kundi la Minsk lililoundwa mwaka 1992 ili kutatua masuala kati ya nchi hizo mbili.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu