Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marufuku ya Hijab ya Ubelgiji: Kutopendelea upande wowote kama Haki mpya ya Kimungu (Droit Divin)

(Imetafsiriwa)

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) imeidhinisha marufuku ya Ubelgiji ya kuvaa hijab shuleni, uamuzi ambao umezusha mijadala kuhusu uhuru wa kidini na usekula barani Ulaya. Mahakama ilipata kwamba marufuku hiyo, iliyokusudiwa kuhakikisha ‘kutopendelea upande wowote’ katika elimu ya umma, haikiuki Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu. Kesi hiyo ilianzishwa na mwanafunzi mmoja Muislamu ambaye alidai kuwa sera hiyo inakiuka haki zake za uhuru wa dini na elimu. Hata hivyo, ECHR iliamua kwamba marufuku hiyo ilihalalishwa na haja ya kudumisha ‘kutopendelea upande wowote,’ kama ilivyotarajiwa.

Utekelezaji huu wa kibaguzi wa kutoegemea upande wowote ni wa kinafiki. Ingawa hijab, nembo ya kitambulisho cha Muslima, imepigwa marufuku kwa jina la kutoegemea upande wowote, nembo au matendo mengine ya kidini hayakabiliani na kiwango kama hicho cha uchunguzi au marufuku. Kwa mfano, sikukuu na nembo za Kikristo bado zinaweza kuadhimishwa na kuonyeshwa katika muktadha mbalimbali wa umma bila vikwazo sawia. Tofauti hii inafichua kwamba sera hizo hazihusiani na kutoegemea upande wowote na zaidi zinakuhusu kuyalenga makundi maalum ya kidini, Waislamu, kuendeleza aina ya upendeleo na ubaguzi wa kithaqafa. Marufuku hiyo inawaathiri vibaya wanawake wa Kiislamu, ikizidhibiti fursa zao za elimu na machaguo yao ya kibinafsi.

Hijab ina umuhimu mkubwa kwa wanawake wa Kiislamu, ikitumika kama kipengee muhimu cha kitambulisho chao na kujieleza kidini. Kuivaa ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran:

[وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِن...َّ]

“Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao...” [Al-Nur: 31]

Haishangazi kwamba ECHR ilitoa uamuzi dhidi ya hijab na kuunga mkono marufuku hiyo. Hijab imekuwa ikishambuliwa kwa miaka mingi sasa, ikisifiwa kuwa ni ushamba na ukandamizaji. Ufaransa imefikia hatua ya kupiga marufuku abaya kwa jina la 'kutopendelea upande wowote' ili kulinda "laïcité" (usekula), utengananishaji kanisa na serikali. Kanuni hii iitwayo usekula imeibuka kama mwitikio kwa droit divin (haki ya kimungu), itikadi inayofafanua fikra kwamba mamlaka ya mfalme ya kutawala yamepeanwa moja kwa moja na Mungu, badala ya kuvuliwa kutoka kwa idhini ya watu au ya mfumo wowote wa kisheria wa kisekula.

Hata hivyo, ukweli kwamba ‘kutopendelea upande wowote’ hujadiliwa tu inapohusu Uislamu na mwonekano wa Uislamu katika maeneo ya umma unaonyesha kwamba usekula sio tu umeshindwa kuondoa dhulma ya kimsingi ya haki ya kimungu (droit divin) kutoka Enzi za Kati. Watetezi wake sasa wanatenda sawasawa kabisa na watetezi wa haki ya kimungu katika siku za nyuma. Kwa maana nyengine, sawasawa na wasomi wa zama za kati (medievalists).

Kwa sababu ni kwa nini tunatakiwa kutopendelea upande wowote inapohusu hijab, abaya, swala, Quran na mengine yote yanayohusiana na Uislamu na kitambulisho chetu cha Kiislamu, lakini sio wakati inapohusu sikukuu za Kikristo, upigaji wa kengele za kanisa, kuwepo kwa shule na vyuo vikuu vya Kikatoliki, mitandio ya kichwa ya wanawake wa Kiyahudi, na kippah. Orodha inaendelea na kuendelea.

Hatimaye, shambulizi la hijab, na mwanamke wa Kiislamu kwa jumla, ni shambulizi la moja kwa moja na la kukusudia kwa shakhsia yake ya Kiislamu. Ni shambulizi dhidi ya Uislamu wenyewe.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sumaya Bint Khayyat

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu