Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Katika Historia nzima ya Kijeshi ya Kiislamu, Makamanda wa Kijeshi wa Kiislamu Waligeuza Mawimbi ya Vita katika Hali Mbaya. Wako wapi Warithi wa Waheshimiwa wa Leo?

(Imetafsiriwa)

Mtume Muhammad al-Mustafa (saw), Amiri wa Milele wa Waislamu wote, alijitangaza kuwa Mtume wa Vita Vikali (Malaham) miongoni mwa vyeo vyake vingi vilivyobarikiwa. Sayyiduna Hudhayfah (ra) alisema kwamba nilikutana na Mtume Mtukufu (saw) kwenye barabara moja mjini Madina. Mtume (saw) amesema, «أَنَا مُحَمَّدٌ، وَأَنَا أَحْمَدُ، وَأَنَا نَبِيُّ الرَّحْمَةِ، وَنَبِيُّ التَّوْبَةِ، وَأَنَا الْمُقَفَّى، وَأَنَا الْحَاشِرُ، وَنَبِيُّ الْمَلاحِمِ»  “Mimi ni Muhammad; Mimi ni Ahmad; Mimi ni Mtume wa Rehma na Mtume wa toba; Mimi ni Mfuasi. Mimi ni Mkusanyaji na Nabii wa Vita Vikali.” [الشمائل المحمدية Ash-Shama'il Al-Muhammadiyah].

Mtume wetu (saw) ndiye kielelezo pekee kwa maafisa wetu wa kijeshi katika kubadili wimbi la vita. Pindi idadi kubwa ya Waislamu ilipozidiwa na shambulizi la kushtukiza la adui katika Vita vya Hunain, Waislamu waliangukia chini ya shambulizi hilo katika wakati dhaifu na wakavunja muundo. Wimbi la vita lilibadilika kwa muda mfupi na kushindwa kulianza kuonekana. Maelezo yake katika Quran Tukufu yamekuja kwa maneno haya,

[وَّیَوۡمَ حُنَیۡنٍ ۙ اِذۡ اَعۡجَبَتۡکُمۡ کَثۡرَتُکُمۡ فَلَمۡ تُغۡنِ عَنۡکُمۡ شَیۡئًا وَّ ضَاقَتۡ عَلَیۡکُمُ الۡاَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ ثُمَّ وَلَّیۡتُمۡ مُّدۡبِرِیۡنَ]

“Na siku ya Hunayni ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni kitu. Na ardhi ikawa dhiki kwenu juu ya upana wake. Kisha mkageuka mkarudi nyuma.” [Surah At-Tawbah 9:25]. Imesemwa katika riwaya kwamba hakuna aliyeachwa isipokuwa watu wa familia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na wahajiri wachache (muhajirina). Kwa hiyo, katika tukio hili kamanda wetu wa milele, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alionyesha ujasiri mkubwa na kusonga mbele, akisema, «أنا النبي لا كذب» “Mimi ni Mtume wala si uwongo.” (an-Nawawi). Baada ya kusikia maneno haya, Waislamu walijipanga upya na wimbi la vita likageuka mpaka Mwenyezi Mungu (swt) akampa Nusra yake kwa ushindi wa uhakika.

Katika Vita vya Qadisiyah, huku akisumbuliwa na maumivu ya miguu (sciatica), Saad bin Abi Waqqas (ra), aliwaongoza Waislamu kwenye ushindi dhidi ya jeshi la Wafursi lililowazidi idadi yao mara tano. Katika vita hivyo, mabadiliko yalikuja wakati makamanda wengine walipoitikia kwa uthabiti matumizi ya Wafursi ya jeshi la ndovu. Walilenga na kuwalemaza ndovu hao kimkakati, na hivyo kugeuza mkondo wa vita.

Katika vita vya Yarmouk, ulikuwa ni ushujaa usio na kifani wa Khalid bin Waleed (ra) ambaye alikabiliana na askari 60,000 wa Kirumi akiwa na watu 60 katika makabiliano ya kwanza ya kijeshi, akitumia muundo wa duara wa kiakili. Alitia hofu kubwa nyoyoni mwa adui hivi kwamba vita viliamuliwa kabla hata havijaanza.

Ilikuwa ni Qutuz na Mabaybari, ambao, licha ya uvamizi na ugaidi wa Mongoli, walitoa jibu la kijasiri kwa barua ya vitisho ya Katabagha naibu wa Halaku Khan. Katabagha alikuwa ameandika, “Tumeifanya ardhi kuwa mtumwa, tumewafanya watoto yatima, tumeadhibu na kuua watu, tumevunja heshima ya machifu wao. Je, munafikiri munaweza kutoroka kutoka kwetu? Baada ya muda mutajua kitakachokujieni.” Hivyo, Wamongolia walikuwa wamepuuza sheria na viwango vyote vya maadili, na hivyo kumfanya Qutuz atangaze vita kwa kuwaua hadharani wajumbe wa Mongoli kwenye lango kuu la Cairo, Bab Zweila. Kitendo hiki cha kijasiri sio tu kiliongeza ari ya Waislamu wenye uoga bali pia kilisisitiza dhamira ya Qutuz kwenye Jihad dhidi ya uoga. Katikati ya vita hivyo akiwatandika Wamongolia, Qutuz, akionyesha ushujaa wa ajabu, alitupilia mbali kofia yake ya chuma na kuongoza mashambulizi makali dhidi ya adui. Hatua hii ya maamuzi iligeuza wimbi la vita, na kusababisha ushindi. Mnamo tarehe 3 Septemba, 1260, wiki chache tu baada ya ushindi wa Ain Jalut, Syria ilikombolewa, kuashiria kuvunjika kwa ngome ya Wamongoli.

Huyo ndiye Saad bin Muadh (ra), kamanda wa Waislamu, ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alichukua ushauri kwake kabla ya Vita vya Badr. Jibu la Saad lilionyesha utiifu na ujasiri usiotingishika, kwa maneno yalio wazi wazi, na yenye azma, "فوالذي بعثك، لو استعرضت بنا هذا البحر فخضته لخضناه معك، وما تخلَّف منا رجل واحد، وما نكره أن تلقى بنا عدونا غداً. إنا لصبر في الحرب، صدق في اللقاء. لعل الله يريك منا ما تَقَرُّ به عينك، فسر بنا على بركة الله"" “Naapa kwa yule aliye kutumiliza, lau utatwambia tuvuke bahari hii na wewe ukajitumbukiza ndani yake, tutajitumbukiza pamoja na wewe, hakuna hata mmoja kati yetu sisi atakayebakia nyuma. Sisi tunachukia wazo la kukutana na adui yetu kesho. Sisi ni watu wenye ujuzi wa kivita, wenye uwezo wa kupigana. Huenda Mwenyezi Mungu akakuonyesha kupitia sisi yale yatakayofurahisha macho yako, hivyo twende pamoja nasi kwa baraka za Mwenyezi Mungu.” Mtume (saw) alijawa na furaha, «سيروا وأبشروا، فإن الله تعالى قد وعدني إحدى الطائفتين، والله لكأني الآن أنظر إلى مصارع القوم»  “Nendeni na pokeeni bishara njema, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameniahidi moja ya makundi mawili (ushindi), Wallahi kana kwamba hivi sasa nayatazama mapambano ya watu.” (الطبراني  At-Tabarani).

Wako wapi makamanda wa kijeshi wa leo, ambao wataondoa mateso ya Umma wa Kiislamu na kutetea kusimamishwa kwa Khilafah, tayari kujitolea maisha yao kwa ajili hilo? Chini ya uongozi wa Khalifa, watakabiliana na umbile la Kiyahudi kwa nguvu ya kutisha, hatua ya maamuzi ambayo inaweza kuwafukuza vibaraka wa Magharibi wanaousumbua Umma wa Kiislamu na kukuuza umoja katika safu zake. Ulimwengu wa Kiislamu unasubiri kwa hamu kujitokeza kwa kiongozi wa aina hiyo. Kwa hivyo, nawauliza maafisa wa Jeshi la Pakistan, "Ni nani kati yenu atakayechukua hatua ya kupata heshima hii?"

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imran Yousufzai – Wilayah Pakistan 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu