Ijumaa, 08 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

SSG Ina Pupa ya Kusubiria Amri ya Kuikomboa Kashmir

(Imetafsiriwa)

Maafisa na askari wa Kikosi Maalum (Special Services Group/SSG) ni miongoni mwa kikosi bora zaidi duniani. Heshima yao imejengwa katika mashindano ya kimataifa na pia katika medani ya mapambano. Wanatia hofu katika nyoyo za maadui wa Uislamu.

Mashujaa wa SSG wana mazoezi ya nguvu. Wanapigana kushinda. Wanatenda kila kinachowezekana. Wenye kufikiria kwa upana na kwa haraka. Hata hivyo, kile kinachowapa fursa dhidi ya kila adui ni hamu yao ya kufa shahidi. Kwa hakika, imani ndio silaha yao kuu katika uwanja wa mapambano.

Imani hiyo haiishii tu kwa SSG wetu, bali ipo katika nyoyo za maafisa na askari wetu wote. Wanatamani kupigania ushindi na kufa shahidi. Wanajua kuwa maelfu ya wanawake watwahirifu wa Kiislamu wametekwa nyara Kashmir. Wanajua kuwa watoto wasio na hatia wanapofuliwa macho kwa marisau. Wanajua wanaume wenye heshima zao wanateswa na kudhalilishwa.

Hata hivyo, ni nani atawapa amri ya kutoka kwa ajili ya Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt)?

Demokrasia iliyofungiwa ndani ya mfumo wa dunia, haitotoa amri namna hiyo. Hakuna namna yoyote ya demokrasia itakayoweza hilo. Mifumo iliyoundwa na binadamu haitotekeleza amri za Mwenyezi Mungu (swt). Ni Khalifah ndiye atakayeongoza vikosi vyetu kwenye ushindi katika ardhi ya Kashmir iliyokaliwa kimabavu.

Mtiini Mwenyezi Mungu (swt) juu ya kila kitu, simamisheni Khilafah. Ikomboeni Kashmir. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[إِن يَنصُرۡكُمُ ٱللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمۡۖ وَإِن يَخۡذُلۡكُمۡ فَمَن ذَا ٱلَّذِي يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani basi, baada yake Yeye atakayekunusuruni? Na waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Aali-Imran 3:160].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu