Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa nini Hatuna Jumuiya ya Waislamu?

(Imetafsiriwa)

Mkutano wa karibuni wa wakuu wa nchi za jumuiya ya BRICs na G20 unaonyesha jumuiya hizo mbili zinaibuka ikiwa sehemu kubwa ya dunia karibuni tu itakuwa yenye kuhitaji kufanya maamuzi juu ya upande upi watahitaji kuwepo nao. Kwa kipindi kirefu mfumo wa kiliberali na taasisi zake zimehodhi maendeleo ya kifedha, kiuchumi na kijamii, lakini baada ya vita vya Marekani na Iraq na Afghanistan kudhoofisha nafasi yake na baada ya mgogoro wa uchumi wa dunia wa 2008 mfumo wa kiliberali wa kilimwengu umepata pigo kubwa, na hili limezifanya Urusi na China kuchukua fursa hiyo kwa kushauri mpango mbadala kwa nchi za Kusini. Ulimwengu wa Kiislamu ima utakuwa kwenye G20 au BRICS itategemea ipi itaibuka mshindi.

Mataifa ya BRICs yalikutana Afrika Kusini mnamo Agosti na suala kuu katika ajenda lilikuwa ni kutanua jumuiya hiyo na kuingiza mataifa mapya. Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia, na Imarati zote zimejiunga na jumuiya hiyo na kinadharia ni jumuiya imara. Jumuiya ina asilimia 60 ya akiba ya mafuta duniani, yenye sehemu kubwa ya madini muhimu, asilimia 40 ya watu wote duniani ikiwemo Indonesia ambayo pia ipo tayari kujiunga. Jumuiya hii ni kubwa mara tatu zaidi ya NATO na hivi sasa ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa nchi zisizo za Magharibi. Kwa miaka sasa China na Urusi zimekuwa na hamu ya kuzipata nchi muhimu za Waislamu kujiunga na jumuiya kwa kuwa itaifanya kuaminika na kuwa na upeo.

Mataifa ya G20 yalipokutana India tamko kuu lilikuwa ni kuhusu ukanda mpya wa kiuchumi utakaounganisha India na Ulaya kupitia Mashariki ya Kati. Marekani, India, Saudi Arabia na nchi nyenginezo zilisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha mtandao wa njia za baharini na reli kuunganisha bara dogo la India pamoja na Ulaya kupitia Mashariki ya Kati. Huku maelezo yakiwa machache, pindi mradi ukimalizika utapunguza kwa thuluthi moja muda wa safari. Kwa mara nyengine, mataifa ya Waislamu ya Mashariki ya Kati yapo katikati ya mradi huu. Raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ili asionyeshe kushindwa, amesema kuwa hakuwezi kuwepo ukanda huo bila ushiriki wa Uturuki na bila ya kutumia mpango wa Maendeleo ya Barabara, ambao ni njia ya reli ya 1.175-km itayotokea bandari ya kusini ya Faw nchini Iraq hadi bandari ya Uturuki ya Mersin, kwenye Bahari ya Kati.   

Mataifa ya Waislamu ni muhimu kwa kuzifanikisha G20 na BRICS na jumuiya zote mbili zinataka kushinda kwa upande wa kifedha na uungaji mkono wa watawala wa Waislamu. Magharibi na Mashariki zinafahamu wazi dori muhimu ya kuchezwa na ulimwengu wa Kiislamu duniani na utajiri wao wa madini na unyeti wa eneo lao kuwa ni muhimu kwa jumuiya zote mbili. Hasa kwa hivi sasa ambapo Urusi na China zinajaribu kutoa changamoto na ikiwezekana kuchukua nafasi ya taasisi za Kimagharibi. 

Wakati Mashariki na Magharibi zinauangalia ulimwengu wa Kiislamu kuwa muhimu, mtu anaweza kufikiria kwa nini watawala wa Kiislamu hawatambui hili na kuweza kuanzisha jumuiya yao wenyewe. Badala ya kuunga mkono ajenda za Wamagharibi na Wamashariki, kwa nini hawatumii uwezo wao na kusimamisha jumuiya yao na kuifanya dunia kuwa katika maslahi yao. Hapa watawala wa Waislamu wameshindwa kwa kuwa wao hatimaye hushughulika na viti vyao vya utawala tu na hawana malengo kama hayo ya kilimwengu. Wakati inatambulika kwa Wamashariki na Wamagharibi kuwa wanao uwezo, wao hawaangalii ambo kwa namna hiyo. Matokeo yake muda wote wanaungana na mataifa mengine katika jumuiya zao na kutia nguvu ajenda zao, wakati wangeweza kupata zaidi.

Mtume (saw) wakati aliposimamisha dola changa ya Kiislamu Madina, licha ya kuwa kwake dhaifu na kukosa rasilimali, alifanya kazi ya kujenga nguvu ya nchi kwa miungano, kusaini mikataba na kupigana na maadui zake. Mtume (saw) alikuwa akifuatilizia hali ya kimataifa iliyokuwa imetawaliwa na Warumi na Wafursi, na kwa haya alitumia werevu wa kuipatia fursa dola ya Kiislamu na kujilinda na kila aina ya vitisho. Kwa namna hii, baada yake, Maswahaba (ra) waliibeba kazi hii na baada ya kipindi fulani iliweza kuzipiku dola zote mbili kubwa. Ujumbe ambao Mtume (saw) alikuwa nao ulitambuliwa na Maswahaba (ra), lakini Maswahaba walichangia jitihada hizi huku wakijua kwamba haikuwa rahisi kufanikisha katika kipindi cha maisha yao. Licha ya hayo walifanya kazi ya kuimarisha dola ya Kiislamu na hivi leo tuna Waislamu bilioni 2 duniani.

Hivi leo, mataifa ya Kiislamu ni muhimu kwa Mashariki na Magharibi, lakini watawala wetu hawatumii fursa hii kufikia kwenye ajenda za Kiislamu. Tutakapokuwa na watawala wanaolenga ajenda za Kiislamu, uzani wa nguvu ya kilimwengu utageuka na zama mpya zitaanza.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu