Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa nini Ubakie Pakistan, Meli Inayozama?

(Imetafsiriwa)

Mjadala mkuu sasa ni jinsi ya kuondoka Pakistan, haraka iwezekanavyo. Pakistan inazama kwa kasi, kiuchumi na kiusalama. Kwa nini tusiruke meli, sasa, kabla hatujazama?

Ni gharama kifedha kuondoka kwani kuna ada za ushauri, ada za kisheria na gharama za usafiri. Elimu ng’ambo ni ghali. Gharama ya maisha inapanda kila mahali na ukosefu wa ajira na madeni pia yanaongezeka. Mishahara haipandi kwa haraka vya kutosha. Aidha, Rizq iko Mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Tunaweza kuwa na nyakati ngumu na nyakati nyepesi nchini Pakistan, au popote kwengine.

Mbali na mifuko yetu, vipi kuhusu wapendwa wetu? Tunawaacha wazazi na babu na nyanya zetu wanaohitaji msaada wetu. Tunawaacha marafiki na jamii zetu zinazotusaidia. Zaidi ya hayo, elimu ya Magharibi ni hatari kwa Dini ya watoto wetu. Kuna ongezeko la uadui kwa wahamiaji pia.

Sio kila mtu anaweza kuruka nje ya meli. Wengi wetu tunapoteza pesa tukijaribu. Kuruka nje ya meli inaweza kuwa suluhisho kwa laki chache, lakini hakika sio kwa milioni 250.

Sasa, ni vipi lau kungekuwa na njia ya kuiokoa meli inayozama?!

Meli yetu inazama kwa sababu ya mfumo wa sasa. Pakistan ina rasilimali nyingi sana. Pakistan inafanywa kuwa maskini kwa sababu ya mfumo wa sasa. Hadithi ni hii hii katika kote katika ulimwengu unaoendelea.

Ili kuokoa meli yetu, tunahitaji kuondoka kutoka kwa mfumo wa sasa. Tunahitaji kuhamia kwa Uislamu na mfumo wake wa utawala, Khilafah. Khilafah ilihakikisha Umma wa Kiislamu unaongoza duniani kwa karne nyingi. Tulikuwa na ustawi pamoja na usalama.

Itatuhitaji sote kufanya kazi ili kusimamisha tena Khilafah. Ni kazi ngumu na iahitaji kujitolea, lakini ni kwa sababu bora zaidi duniani, radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu