Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mifumo Iliyoundwa na Wanaadamu ni yenye Kushindwa katika Azma Zao Hivyo Kasoro zao Zimefichuka

Baada ya mataifa ya kikafiri kuungana dhidi ya Dola ya Khilafah na kuiondosha mwaka 1924 Miladi, na kugawanya ardhi za Waislamu katika vijinchi vidogo vidogo, Ummah umeathiriwa na tawala ambazo bila ya kuwa na mamlaka kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), tawala za kifisadi zilizo buniwa na wanaadamu, ambazo watawala wake ni vibaraka na walinzi wa Mashariki na Magharibi, wakitawala Waislamu kwa nidhamu za kisekula zilizo patikana kutoka katika nidhamu za Makafiri Wamaghribi. Tokea muda huo, heshima ya Ummah wa Kiislamu imepotea na haikupatikana siku ya furaha au ushindi wa kweli. Zaidi ya hayo, Waislamu wamepoteza maana zote za furaha na wameishi katika maisha ya udhalili; utajiri wao umeporwa na heshima yao imekiukwa, na hivyo, Ummah umeanguka na kushuka kutoka kuwa dola kiongozi yenye mamlaka na kuishia kwenye Utwaghuut, ikishikilia kamba dhaifu za ukafiri, ukiiwacha kamba imara ya Mwenyezi Mungu (swt). Amesema (swt):

  (‏أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيداً)

“Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na shetani anataka kuwapotezelea mbali.” [An-Nisa: 60].

Mifumo hiyo iliyooza iliyoundwa na binadamu ni viraka vya itikadi ya kirasilimali iliyoingizwa kwa watu, ambayo imejengwa juu ya kuitenganisha dini na dola, ikawa kwa kupitiwa na muda ni mtenganisho wa dini, mila na maadili kutokana na maisha. Hivyo ndivyo vima na fahamu ambazo huthamini kima cha kimada pekee maishani. Wanadamu wamekosa utulivu na usalama chini ya kivuli chake, na kuwepo badala yake udhalilifu katika nyanja tofauti za maisha ya kijamii, uchumi na siasa, hadi maisha kuwa ni moto usiobebeka.  

Ifuatayo ni mifano mitatu ya kikweli zaidi ya kufeli kwa mifumo hii iliyoundwa na mwanadamu katika kufikia haki na maisha bora kwa wanadamu:

1. Kufuatana kwa migogoro ya kiuchumi: Utekelezaji wa mifumo hii ya kirasilimali ni sababu kuu ya hali zote za kiuchumi ambazo dunia inakumbana nazo, ambazo zinawakilishwa na serikali katika kupanda kwa bei kwa namna haribifu, kushuka kwa thamani ya sarafu za nchi, mgogoro wa fedha na ukwasi, na vizuizi katika kazi za watu kupitia kodi zinazopita mpaka, pamoja na ukosefu wa ajira. Lakini pindi Waislamu wa mwanzo walipokuwa wanatumia mfumo wa Wahyi, uadilifu ulifikia kileleni, mbwa mwitu alikuwa akila pamoja na mbuzi, ngano zikienea juu ya milima kwa ajili ya kula ndege, na Khalifah akisimama kuliambia wingu: “Nenda, kokote unyesheko, nitakusanya kodi yako”, hivyo maisha yalikuwa yamejaa faraja, amani na utulivu.

2. Kunyimwa kwa hifadhi na usalama: ambazo ni miongoni mwa misingi na mahitaji muhimu ya maisha, lakini hatuhitaji dalili nyingi na uhakikisho kuthibitisha kufeli kwa mataifa ya kisekula katika kutoa usalama na hifadhi kwa raia wake, kwa sababu maisha ya watu ni rahisi na hayana thamani kutokana na sheria zilizoharibika na kuoza na taratibu ambazo hazihifadhi heshima na maadili ya mwaadamu. Huku katika Mfumo wa Kiislamu, usalama ni kipaumbele kikuu cha dola, Mtume (saw) amesema:

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، آمِناً فِي سِرْبِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا بِحَذَافِيرِهَا»

“Yeyote anaye amka miongoni mwenu hali ya kuwa ni mwenye afya, mwenye amani na hifadhi, mwenye chakula cha siku yake, basi huwa kana kwamba ameipata dunia yote.”

3. Huduma mbovu za afya: ambapo zimefichuka hivi karibuni kwa virusi vya Korona, kwa idadi ya visa vilivyo thibitishwa ikizidi milioni tatu, huku ikiacha vifo angalau 208,973 kote duniani. Haya ni mbali na kusambaratika kwa maisha ya watu kutokana na maamuzi ya ovyo ovyo bila kutumia hatua muhimu na sahihi hadi kufikia nukta hii ya kuzorota kwa hali za kiuchumi; kwa hivyo basi, mifumo hii haiwezi kutatua matatizo ya msingi kwa kuwa haijali kuhusu watu wala kuwahofia. Hata hivyo, afya katika Uislamu ni hitajio la msingi ambapo serikali lazima iwapatie watu wote, hii ni kwa sababu afya ya mwili ni moja ya masuala makubwa zaidi kwa raia, na kushughulikia juu ya masuala ya watu ni wajibu kwa dola kwa mujibu wa Hadith:

«  الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِه  »

“Kiongozi ni mchunga nae ataulizwa juu ya raia wake”. Hivyo, kuwapatia watu dawa ni wajibu kwa dola na kutowapatia watu hupelekea katika madhara, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

  «  لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ  »

“Hakuna kudhuru wala kudhuriana.”

Katika muktadha huu, vilevile, dola ni lazima iwadhamini matibabu raia wake, na dhamana hii unajitokeza katika dola kwa kutumia nguvu zake zote katika kutekeleza kile kinachohusiana na kufadhili miradi yake na uangalizi wake.

Yote haya na mengine zaidi ni kutokana na utekelezaji wa mifumo ya kibinadamu na kutenganishwa kwake na muundo wa Mwenyezi Mungu katika utawala chini ya jina la demokrasia na Urasilimali, kuvuka mipaka juu ya haki ya Uungu kwa Muumbaji wa mbingu na ardhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu na atukuzwe.

Ustawi wa kweli, utulivu, na maisha ya starehe yatapatikana tu katika utekelezaji wa mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), kwa kuwa Yeye ni Ndiye Muumbaji wa watu wote. Uislamu ndio mfumo pekee wenye uwezo wa kutatua matatizo ya watu kiuchumi, kijamii, kisiasa na matatizo ya kiafya, unaotekelezwa ndani ya dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ambayo inajenga taasisi zake zote, miundo, mifumo, na katiba kwa hukmu za sheria zinazotokana na Itikadi ya Kiislamu ambao ndio mfumo wa Ummah, mahala pake pa heshima na chanzo cha izza yake, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ)

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndio Dini iliyo nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 40]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Rana Mustafa

#كورونا             #Covid19           #Korona          

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 02 Juni 2020 17:42

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu