Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uislamu Unapinga Dola ya Kitaifa

Uislamu Unaunganisha Ummah wa Kiislamu Kuwa Dola Moja ya Khilafah Iliyo na Nguvu

(Imetafsiriwa)

Utangulizi: Uunganishaji na kuwa Khilafah Moja Unatafautiana na Mgawanyiko wa Dola Nyingi za Kitaifa

Huku Ulimwengu wa Kiislamu ukiporomoka katika uchumi na usalama, Waislamu wanatafuta njia ya kutokea. Hivi sasa Waislamu wamegawanyika katika dola za kitaifa hamsini na saba, ambapo hali hiyo imewadhoofisha. Hivi sasa kuna mjadala unaoenea kuhusiana na umoja baina ya Waislamu kuuimarisha Ummah. Ummah uliyoungana utaokuwa na dola moja iliyo kubwa zaidi ya nchi nyengine yoyote duniani, iliyo na hazina moja, jeshi moja na bila mipaka baina ya wilaya zake. Khilafah itakuwa na idadi kubwa ya vijana, jeshi kubwa zaidi, uzalishaji mkubwa zaidi wa bidhaa za kilimo, iliyo na rasilimali za madini kwa kiwango kikubwa na nishati za aina tafauti na udhibiti wa njia kuu zote za biashara na bahari duniani.

Uislamu ni kiunganishi kinachoweza kufikisha aina maalum ya umoja. Inawaelezea Waislamu kuwa ni watu wamoja, waliotafauti na wengine wote. Unakataa mgawanyiko wowote baina ya Waislamu kulingana na asili, rangi, kabila au utaifa. Unaweka mamlaka moja juu ya Ummah wote wa Kiislamu, Khalifah. Unalazimisha dola moja kwa Ummah wa Kiislamu, Khilafah. Unakataza mgawanyiko wa dola na mamlaka ya Waislamu, licha ya kuwepo (tafauti katika) asili, makabila na mataifa. Kwa namna hiyo, Uislamu uko mbali na fikra ya dola ya kitaifa.

Dola ya Kitaifa na Utaifa ni kitu kigeni kwa Uislamu Katika Uasili wake

Fahamu ya dola ya kitaifa imezalikana na historia na imani za Ukristo wa Ulaya. Ni kitu kigeni kabisa katika Uislamu. Vita Vya Miaka Thalathini barani Ulaya vilipiganwa baina ya dola za Kikristo. Viliendelea hadi 1648, mwaka ambao mikataba iliyounda makubaliano ya Amani ya Westphalia ilianza kusainiwa, ikimaliza vita vya kidini. Ikawa ni mwanzo wa kuzuka dola mpya za kitaifa, ikiwa ni jaribio la kumaliza mizozo baina ya dola za kidini.

Dola katika nchi za kibepari za Wamagharibi zimeegemea juu ya fahamu ya dola za kitaifa. Ardhi na serikali yake inakuwa ni ya dola hiyo ya kitaifa na inatafsiriwa juu ya msingi huu. Watu ndio wanaotafsiri dola ya kitaifa kulingana na mipaka yao iliyokubaliwa. Watu wanatambulika kulingana na jambo au mambo kadhaa, kama jografia, historia, asili na urithi wa lugha.

Fahamu ya dola ya kitaifa ni fahamu ovu kuanzia msingi wake. Imejengwa juu ya ufahamu wa kimakosa wa kile kinachowajenga wanadamu. Kwa kweli, taifa linakuwa kama ni mtu mmoja katika maisha ikiwa tu lina fikra ya pamoja, imani na vigezo kuelekea masuala ya maisha. Ama kwa upande wa historia, jografia, asili na urithi wa lugha kuwa navyo ni vipengele, (hivi) vinachangia tu katika kujenga sifa za pamoja miongoni mwa watu.

Hata hivyo, haviwezi kuwaunganisha watu juu ya mtazamo mmoja kuhusu maisha. Hivyo, njia pekee ya kutafsiri taifa inategemea juu ya itikadi ya pamoja. Pia, dola ya kitaifa haimalizi mzozo. Zinaunda aina mpya ya mzozo, ambao ni mzozo baina ya dola za kitaifa. Imetishia dunia nzima kwa mivutano, ushindani, ugomvi, vita na vita vya dunia.

Hatari ya Utaifa na Dola ya Kitaifa

Kinyume na madai ya Wamagharibi, dola ya kitaifa imezidisha ugomvi na vita. Dola ya kitaifa imesababisha vita vyote vikuu vya dunia na imekuwa ni mharibifu mkubwa kwa dunia. Fahamu ya dola ya kitaifa inachochea fikra ya ubora wa jamii moja dhidi ya nyengine zote. Inaweka ubwana wa jamii moja dhidi ya nyengine zote. Hivi ndivyo zilivyofanya Ujerumani, Ufaransa, Urusi, Uingereza na nchi nyengine za kikoloni za Kimagharibi katika historia zao. Ugomvi wa dola ya kitaifa ndio msingi wa vita vya uharibifu baina ya Urusi na Ukraine, pamoja na mivutano baina ya Marekani na China.

Dola ya kitaifa pia imezidisha hitajio la utanuzi wa kikoloni wa kibeberu. Dola za kitaifa zilizoibuka katika Ulaya zimejikuta haziwezi kujitanua kieneo. Hivyo zimegeukia utanuzi wa kikoloni. Zimeharibu sehemu kubwa ya dunia, ikiwemo Ulimwengu wa Kiislamu. Ukoloni upo hata sasa ukiwa ni ukoloni mambo leo, ambao unaegemea zaidi kwenye ukoloni wa kiuchumi na kisiasa, kuliko kuwa ni uvamizi wa moja kwa moja wa kijeshi. Kwa kweli, huenda ukoloni mambo leo hivi sasa umefikia kiwango kikubwa zaidi na kuenea zaidi kuliko katika zama zilizopita za historia ya Wamagharibi.

Mbali na ukoloni, dola ya kitaifa imeharibu Ummah wa Kiislamu kupitia migawanyiko. Hii japokuwa Waislamu walidhani dola ya kitaifa itawapatia uhuru kutoka katika ukoloni. Ummah ulibomolewa kwa sababu ya utaifa wa Waturuki na Waarabu. Waarabu waliasi na Waturuki walijivua jukumu la Ummah. Ndipo hatimaye Mwenyezi Mungu akawapatia Makafiri uwezo juu ya mambo yetu. Wabalkan walijitenga kutoka Khilafah Uthmani, kwa msingi wa utaifa. Kisha kukawa na historia ya sasa ya utaifa. Pakistan iliisaidia Marekani dhidi ya Afghanistan, kwa msingi wa maslahi ya utaifa. Saudi Arabia, Syria, Uturuki, Kuwait, Imarati zilisaidia uvamizi wa Marekani nchini Iraq juu ya msingi wa maslahi ya utaifa. Watawala wa sasa wanakataa kupigana kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na Palestina kwa msingi wa utaifa. Binadamu wameteseka vya kutosha kutokana na fahamu hii ya dola ya kitaifa. Ni juu ya wanadamu kuzingatia fikra ya kipekee ya watu, udugu, muungano na dola ambayo Uislamu unatoa. Harakati za kuzingatia Uislamu kuwa ni mfumo mpya wa dunia lazima ziongozwe na Waislamu.

Waislamu ni Ummah Mmoja Uliounganishwa na Iman

Waislamu sio watu waliokuja pamoja kwa msingi wa ardhi, kabila, asili, utaifa au lugha. Uislamu uko mbali na fikra za Kimagharibi za utaifa, udugu wa kitaifa, taifa na dola ya kitaifa. Waislamu ni Ummah mmoja, uliounganishwa na Uislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا]

“Na shikamaneni na Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Surah Aali Imran 3:103]. Ibn Kathir ameeleza katika Tafsiri yake, أمرهم بالجماعة ونهاهم عن التفرقة  “Yeye (saw) amewaamrisha Waislamu kuwa jamii moja na amewakataza kugawanyika.” Aya hii ni dalili kuwa Waislamu wanalazimishwa kuwa pamoja, kuungana, ndani ya umbo moja. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]

“Hakika Waumini ni ndugu.” [Surah Al-Hujurat 49:10]. Imam Qurtubi amesema katika Tafsiri yake, أي في الدين والحرمة لا في النَّسَبِ ، وَلِهَذَا قِيلَ أُخُوَّةُ الدِّينِ أَثْبَتُ مِنْ أُخُوَّةِ النَّسَبِ ، فإن أُخُوَّة النَّسَبِ تنْقَطِع بِمُخَالَفَةِ الدِّينِ ، وَأُخُوَّة الدِّينِ لَا تنْقَطِع بِمُخَالَفَةِ النَّسَبِ “Yaani, katika Dini na matukufu, na sio katika nasaba. Na kwa sababu hii, imesemwa, ‘Udugu katika Dini ni wa kudumu zaidi kuliko udugu wa nasaba, kwani udugu wa nasaba unakatika kwa kutafautiana dini, wakati udugu katika dini haukatiki kwa kutafautiana nasaba.”

Mtume (saw) amesema, «هَذَا كِتَابٌ مِنْ مُحَمَّدٍ النَّبِىِّ ﷺ بَيْنَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُؤْمِنِينَ مِنْ قُرَيْشٍ وَيَثْرِبَ وَمَنْ تَبِعَهُمْ فَلَحِقَ بِهِمْ وَجَاهَدَ مَعَهُمْ أَنَّهُمْ أُمَّةٌ وَاحِدَةٌ دُونَ النَّاسِ» “Haya ni maafikiano ya Mtume Muhammad (saw) baina ya Waislamu na Waumini miongoni mwa Maquraish na Yathrib, na wanaowafuata, wakaungana nao nawakapigana jihad pamoja nao. Kwamba wao ni Ummah mmoja, walio tafauti na wengine.” [Imepokewa na Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra.] Ummah wa Kiislamu ni Ummah mmoja na umoja wa Kiislamu lazima upatikane kivitendo ndani yake. Kwa upande wa umoja huu wa kisiasa, umejumuishwa katika usimamishaji wa Khilafah.

Hivyo, Dola ya Kiislamu katika Madinah Al-Munawwarah haikuwa ni dola ya kitaifa. Ilikuwa ni mamlaka ya watu wamoja, waumini, waliounganishwa na imani yao, licha ya kutafautiana kwao katika makabila na asili zao. Historia inashuhudia namna UislamU ulivyowaunganisha watu wa mabara matatu kwa imani. Umewayayusha kuwa Ummah mmoja ulio muaminifu kwa Uislamu.

Waislamu Wasigawanywe na Ukabila na Utaifa

Uislamu unapinga aina zote za migawanyiko na ubaguzi unaojengwa juu ya nasaba, kabila, utaifa na lugha.

Mtume (saw) amesema katika Hijja ya Kuaga, «يَا أَيُّها النَّاسُ أَلا إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ، وَإِنَّ أَباكُمْ وَاحِدٌ، أَلا لا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ على عَجَمِيٍّ، وَلا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ، وَلَا أَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ، ولا أَسْوَدَ على أَحْمَرَ، إِلَّا بِالتَّقْوَى» “Enyi watu, tambueni kuwa, Mola wenu ni mmoja, na baba yenu (Adam) ni mmoja. Tambueni kuwa hakuna ubora kwa Muarabu juu ya asiye Muarabu, wala kwa asiye Muarabu juu ya Muarabu, wala kwa mweupe juu ya mweusi, wala kwa mweusi juu ya mweupe, isipokuwa kwa uchamungu.” [Ahmad]

«إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَفَخْرَهَا بِالآبَاءِ مُؤْمِنٌ تَقِيٌّ وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ أَنْتُمْ بَنُو آدَمَ وَآدَمُ مِنْ تُرَابٍ لَيَدَعَنَّ رِجَالٌ فَخْرَهُمْ بِأَقْوَامٍ إِنَّمَا هُمْ فَحْمٌ مِنْ فَحْمِ جَهَنَّمَ أَوْ لَيَكُونُنَّ أَهْوَنَ عَلَى اللَّهِ مِنَ الْجِعْلاَنِ الَّتِي تَدْفَعُ بِأَنْفِهَا النَّتْنَ» “Mwenyezi Mungu (swt) ameondoa kwenu majivuno ya zama za kijahiliya na fakhari za mababu zake. Mtu huwa muumini mchamungu au muovu mwenye dhambi. Nyote ni wana wa Adam na Adam anatokana na udongo. Watu wasijifakharishe kwa kaumu zao. Hakika hiyo ni makaa katika makaa ya Jahannam, au watakuwa waduni sana mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mende anayevingirisha kinyesi kwa pua yake.” [Abu Daud]

Mwenyezi Mungu (swt) amewaumba wanaadamu wakiwa makabila na asili tafauti ili watambuane. Na sio watengane na kujifakharisha baadhi kwa baadhi yao. Ubora ni kulingana na uchamungu, jambo ambalo linatambulikana na Mwenyezi Mungu pekee. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَـٰكُم مِّن ذَكَرࣲ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَـٰكُمۡ شُعُوبࣰا وَقَبَاۤىِٕلَ لِتَعَارَفُوۤا۟ إِنَّ أَكۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَىٰكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِیمٌ خَبِیرٌ]

“Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari.”  [Surah Al-Ḥujurāt 49: 13].

Ni Dhambi Kubwa Kulingania Mshikamano juu ya Msingi Usiokuwa Udugu wa Kiislamu

Uislamu unapinga miito ya ukabila au utaifa. Ni wito hatari unaowagawa Waislamu na kuwadhoofisha. Umefungwa kwenye kifo juu ya ukafiri, kutokea siku za ujahilia kabla ya Uislamu.

Mtume (saw) amesema, «مَنْ قُتِلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ يَدْعُو عَصَبِيَّةً أَوْ يَنْصُرُ عَصَبِيَّةً فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ» “Anaeuawa chini ya bendera ya ujahiliya, akilingania uasabiya au kuunga mkono uasabiya, basi amekufa kifo cha kijahiliya” [Muslim]. Kuhusiana na Hadithi hii, Imam An-Nawawi amesema katika Sharhi yake, وَإِنَّمَا يَغْضَبُ لِعَصَبِيَّةٍ لَا لِنُصْرَةِ الدِّينِ، وَالْعَصَبِيَّةُ إِعَانَةُ قَوْمِهِ عَلَى الظُّلْمِ  “Kwa hakika, anakasirika kwa ajili ya uasabiya na wala sio katika kuinusuru dini. Na uasabiya ni kusaidia kaumu yake juu ya dhulma.” Hivyo Waislamu na wakatae wito wowote wa ukabila au utaifa na washikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt), kwani huo ni ufumbuzi wa nguvu zetu.

Mtume (saw) amekemea kila ufadhilishaji wa asili ya ukabila. Muslim amenukuu kuwa vijana wawili, mmoja kutoka Muhajirin na mwengine kutoka Ansar, walikuwa wakipigana. Muhajir aliita Muhajir wenziwe, na Ansar aliita Ansar wenziwe. Mtume (saw) alikuja na akasema,«مَا هَذَا دَعْوَى أَهْلِ الْجَاهِلِيَّةِ» “Wito gani huu wa kijahiliya?” [Muslim]. Kuhusiana na Hadithi hii, Imam An-Nawawi amesema katika Sharh yake,” وَأَمَّا تَسْمِيَته ﷺ ذَلِكَ دَعْوَى الْجَاهِلِيَّة فَهُوَ كَرَاهَة مِنْهُ لِذَلِكَ،  فَإِنَّهُ مِمَّا كَانَتْ عَلَيْهِ الْجَاهِلِيَّة مِنْ التَّعَاضُد بِالْقَبَائِلِ فِي أُمُور الدُّنْيَا وَمُتَعَلِّقَاتهَا ، وَكَانَتْ الْجَاهِلِيَّة تَأْخُذ حُقُوقهَا بِالْعَصَبَاتِ وَالْقَبَائِل ، فَجَاءَ الْإِسْلَام بِإِبْطَالِ ذَلِكَ،  وَفَصَلَ الْقَضَايَا بِالْأَحْكَامِ الشَّرْعِيَّة  “Ama kwa kuutaja kwake SAW wito huu kuwa ni wa kijahiliya hiyo ni kwa kuuchukia. Kwani wito huo ni katika tabia za kijahiliya kuunga mkono ukabila, katika mambo yanayohusiana na dunia. Ni katika ujahiliya kuchukua haki zake kwa misingi ya nasaba na kabila. Uislamu ukaja kubatilisha hayo, na ukaamua kesi kwa hukumu za kisharia.”

Kile kilicho yaunganisha makabila hasimu katika Bara Arabu haikuwa nasaba, bali ni Uislamu pekee. Mtume (saw) amekemea uasabiya kwa kauli kali. Mtume (saw) amesema, «مَنْ تَعَزَّى عَلَيْكُمْ بِعَزَاءِ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَعِضُّوهُ بِهَنِّ أَبِيهِ وَلَا تُكَنُّوا» “Atakayejisifia kwa sifa za kijahiliya, basi na atafune uume wa baba yake, na msiseme kiistiari.” [Imepokewa na Ahmad]. Kuhusiana na Hadithi hii, Mulla Ali Al-Qari amesema katika Sharhi yake, من تعزى أي انتسب بعزاء الجاهلية بفتح العين أي نسب أهلها وافتخر بآبائه وأجداده  “Yule anayejisifia binafsi humaanisha anasifia ukabila kama ulivyosifiwa ujahiliya kama alivyokulia utotoni, yaani kujinasibisha na watu wake kwa kujifakharisha kwa mababa na mababu zake.”

Hadhara ya Kiislamu Inakataza Uasabiya juu ya Msingi wa Uasili, Ukabila, na Utaifa

Swahaba mkubwa, Abdullah ibn Mas’ud (ra) amesema, مَنْ نَصَرَ قَوْمَهُ عَلَى غَيْرِ الْحَقِّ فَهُوَ كَالْبَعِيرِ الَّذِى رُدِّيَ فَهُوَ  يُنْزَعُ بِذَنَبِهِ  “Yule anayesaidia watu wake kwa jambo lisilo la haki, ni kama ngamia aliyeanguka kisimani na kutolewa kwa mkia wake.” [Abu Daud]. Kuhusiana na kauli hii ya Swahaba (ra), Imam Al-Khatabi amesema katika Ma’alim as-Sunan, مَعْنَاهُ أَنَّهُ قَدْ وَقَعَ فِي الْإِثْم وَهَلَكَ كَالْبَعِيرِ إِذَا تَرَدَّى فِي بِئْر فَصَارَ يُنْزَع بِذَنَبِهِ وَلَا يَقْدِر عَلَى الْخَلَاص  “Maana yake ni kuwa ameangukia kwenye madhambi na ameangamia kama ngamia alipoingia kisimani. Anakuwa amenyimwa kwa sababu ya dhambi zake, na hawezi kuokolewa.”

Imam Shafi amesema, مَنْ أَظْهَرَ الْعَصَبِيَّةَ بِالْكَلَامِ، وَتَأَلَّفَ عَلَيْهَا، وَدَعَا إِلَيْهَا، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ يُشْهِرُ نَفْسَهُ بِقِتَالٍ فِيهَا فَهُوَ مَرْدُودُ الشَّهَادَةِ، لِأَنَّهُ أَتَى مُحَرَّمًا، لَا اخْتِلَافَ فِيهِ بَيْنَ عُلَمَاءِ الْمُسْلِمِينَ فِيمَا عَلِمْتُهُ، وَاحْتَجَّ بِقَوْلِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ ﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴾ وَبُقُولِ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ وَكُونُوا عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا  “Yule anayedhihirisha uasabiya kwa maneno na akauzoesha, na akaulingania, hata kama hakujidhihirisha kwa kuupigania, basi ushahidi wake ni wenye kukataliwa, kwani ametenda jambo la haramu. Hakuna ikhtilafu baina ya wanazuoni Waislamu juu ya hilo kwa kadiri nijuavyo. Na dalili ni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt), ﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ“Kwa hakika Waumini ni ndugu” na pia kwa kauli ya Mtume (saw), وَكُونُوا عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا  “Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu mlio ndugu.” [Imepokewa na Bayhaqi katika As-Sunan As-Saghir]

Badr ud Din Al-Ayni Al-Hanafi, aliyekufa mwaka 855 H, amesema katika “Umdat al-Qari Sharh Sahih ul-Bukhari” kuwa, قَوْله، (مَا بَال دَعْوَى الْجَاهِلِيَّة؟) يَعْنِي، لَا تداعوا بالقبائل بل تداعوا بدعوة وَاحِدَة بِالْإِسْلَامِ، ثمَّ قَالَ، مَا شَأْنهمْ؟ أَي، مَا جرى لَهُم وَمَا الْمُوجب فِي ذَلِك؟ قَوْله، (دَعُوهَا) ، أَي، دعوا هَذِه الْمقَالة، أَي، اتركوها أَو، دعوا هَذِه الدَّعْوَى، ثمَّ بيَّن حِكْمَة التّرْك بقوله، (فَإِنَّهَا خبيثة) أَي، فَإِن هَذِه الدعْوَة خبيثة أَي قبيحة مُنكرَة كريهة مؤذية لِأَنَّهَا تثير الْغَضَب على غير الْحق، والتقاتل على الْبَاطِل، وَتُؤَدِّي إِلَى النَّار. كَمَا جَاءَ فِي الحَدِيث، (من دَعَا بِدَعْوَى الْجَاهِلِيَّة فَلَيْسَ منا وليتبوأ مَقْعَده من النَّار) “Ama kwa kauli yake Mtume (saw), Kwa nini uitie wito wa kijahiliya? Yaani, usilinganie kwa msingi wa ukabila bali itia wito wa umoja wa Uislamu. Kisha akaulizwa, wana nini wao? Yaani nini kimetokea kwao, na nini sababu ya hayo. Ama kwa kauli yake, “Acheni” yaani acha msimamo huu, yaani achana nao, au acha ulinganizi huu, kisha akataja hikma ya kuacha kwa kauli yake, kwani huo ni uvundo.” Yaani ni mbaya wenye kulaumiwa, kuchukiza na kudhuru, kwani unachochea hasira juu ya kile kisicho cha haki, na kupigania juu ya batili, na kuongoza kwenye moto. Kama ilivyokuja katika Hadith, “Mwenye kulingania ulinganizi wa kijahiliya si katika sisi, na ajiwekee makaazi yake motoni.”

Waislamu Lazima wawe na Khalifah Mmoja tu Mwenye Mamlaka juu yao

Ummah wa Kiislamu sio tu ni watu tafauti na wengine. Ni wenye Khalifah mmoja, ndani ya dola moja.

Mtume (saw) amesema, «وَإِنَّهُ لاَ نَبِيٌ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فَتَكْثُرُ» “Hakuna Mtume baada yangu, kutakuwa na Makhalifah watakuwa wengi.” Maswahaba wake (ra) wakasema, فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ “Basi unatuamuru nini?” Akasema, «فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ» “Wapeni bay’ah mmoja baada ya mmoja.” [Muslim]. Kuhusiana na Hadithi hii Imam An-Nawawi amesema katika Sharhi kuwa, وَمَعْنَى هَذَا الْحَدِيثِ إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَةٍ بَعْدَ خَلِيفَةٍ فَبَيْعَةُ الْأَوَّلِ صَحِيحَةٌ يَجِبُ الْوَفَاءُ بِهَا وَبَيْعَةُ الثَّانِي بَاطِلَةٌ يَحْرُمُ الْوَفَاءُ بِهَا وَيَحْرُمُ عَلَيْهِ طَلَبُهَا وَسَوَاءٌ عَقَدُوا لِلثَّانِي عَالِمِينَ بِعَقْدِ الأول جَاهِلِينَ وَسَوَاءٌ كَانَا فِي بَلَدَيْنِ أَوْ بَلَدٍ أَوْ أَحَدُهُمَا فِي بَلَدِ الْإِمَامِ الْمُنْفَصِلِ “Pindi Khalifah atakapopewa bay’ah baada ya Khalifah mwengine kupewa bay’ah, basi bay’ah ya kwanza ndio sahihi na inapaswa kutekelezwa, na bay’ah ya pili ni batili na ni haramu kutekelezwa. Hii haijalishi kwa Waislamu kuwa walijua juu ya bay’ah ya mwanzo ama la, wala haijalishi kama wapo katika mji mmoja au miji tafauti, au kuwa mmoja wao yupo katika ardhi iliyo tafauti na nyengine.”

Ibn Is-haq (ra) amenukuu kwamba katika Khutba yake, Khalifah Rashid wa mwanzo Abu Bakar (ra), amesema, وَإِنَّهُ لَا يَحِلُّ أَنْ يَكُونَ لِلْمُسْلِمِينَ أَمِيرَانِ، فَإِنَّهُ مَهْمَا يَكُنْ ذَلِكَ يَخْتَلِفْ أَمَرُهُمْ وَأَحْكَامُهُمْ، وَتَتَفَرَّقُ جَمَاعَتُهُمْ، وَيَتَنَازَعُوا فِيمَا بَيْنَهُمْ، هُنَالِكَ تُتْرَكُ السُّنَّةُ، وَتَظْهَرُ الْبِدْعَةُ، وَتَعْظُمُ الْفِتْنَةُ، وَلَيْسَ لِأَحَدٍ عَلَى ذَلِكَ صَلَاحٌ  “Kwa hakika, hairuhusiwi kwa Waislamu kuwa na Amiri wawili. Kama itatokea hivyo, hakutakuwa na makubaliano juu ya masuala yao na hukumu zao, jamii ya Waislamu itafarikiana, na watazozana baina yao. Hilo litapelekea kuwachwa kwa Sunnah na kudhihiri bida’a na kuenea fitna, na kwa hilo hakutakuwa na wema kwa yeyote.”

Ndipo Khalifah Umar (ra) alikuwa Khalifah wa Waislamu walioishi katika mabara matatu. Hilo lilipatikana katika zama ambapo ujumbe ulipelekwa kwa wapanda farasi na kusafiri kupitia njia za ardhini na baharini. Basi kwa nini isiwezekane leo, katika zama za mawasiliano na usafiri wa anga?

Hadhara ya Kiislamu Inakataza Makhalifah Wawili Juu ya Waislamu Mahala popote duniani

Imam Shafi, aliyefariki mnamo 204 H amesema katika Al-Risalah kuwa, وما أجمَعَ المُسْلِمونَ عليه مِن أن يَكونَ الخَليفةُ واحِدًا، والقاضي واحِدًا والأميرُ واحِدًا، والإمامُ  “Na kile ambacho Waislamu wamekubaliana ni kuwa, kuwepo na Khalifah mmoja, kadhi mmoja na amiri mmoja na imamu mmoja.”

Imam Mawardi, aliyekufa mwaka 450 H amesema katika kitabu chake, Al-Ahkam as-Sultaniya, kuwa, وَإِذَا عُقِدَتِ الْإِمَامَةُ لِإِمَامَيْنِ فِي بَلَدَيْنِ لَمْ تَنْعَقِدْ إمَامَتُهُمَا؛ لِأَنَّهُ لَا يَجُوزُ أَنْ يَكُونَ لِلْأُمَّةِ إمَامَانِ فِي وَقْتٍ وَاحِدٍ”. “Pindi maimamu wawili wakichaguliwa katika miji miwili tafauti uteuzi wao hautotimia. Kwani haijuzu kupatikana maimamu (makhalifah) wawili katika Ummah katika wakati mmoja”.

Ibn Hazm aliyefariki mwaka 458 H, amesema katika “Maraatib al-Ijmaa kuwa, وَاتَّفَقُوا انه لَا يجوز أَن يكون على الْمُسلمين فِي وَقت وَاحِد فِي جَمِيع الدُّنْيَا امامان لَا متفقان وَلَا مفترقان وَلَا فِي مكانين وَلَا فِي مَكَان وَاحِد  “Wameafikiana (Ijma’a) kuwa haijuzu kupatikana juu ya Waislamu Maimamu wawili katika wakati mmoja duniani, ima wataafikiana au hawatawafikiana wala wakiwa katika eneo moja au maeneo tafauti.”

Hii ni katika kuwa na Makhalifah wawili wanaowatawala Waislamu kwa Uislam. Je, vipi basi katika kuwepo makumi ya watawala wanaotawala kinyume na Uislamu na kuwagawa Waislamu?!

Kuigawanya Mamlaka moja ya Waislamu ni Jambo lililokatazwa Kabisa

Waislamu wanatakiwa wawe na Khalifah mmoja na ni kosa kubwa kuugawanya umoja wao. Ni jambo nyeti katika Uislamu kuudhibiti umoja wa mamlaka, kiasi cha kuwa damu ya Muislamu inaruhusiwa kumwagwa kwa ajili yake.

Mtume (saw) amesema, «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الآخَرَ مِنْهُمَا» “Watakapopewa Bay’ah Makhalifah wawili basi muuweni wa pili kati yao.” [Muslim]. Kuhusiana na Hadithi hii, Imam An-Nawawi amesema katika maelezo yake kuwa, وَاتَّفَقَ الْعُلَمَاءُ عَلَى أَنَّهُ لَا يَجُوزُ أَنْ يُعْقَدَ لِخَلِيفَتَيْنِ فِي عَصْرٍ وَاحِدٍ سَوَاءٌ اتَّسَعَتْ دَارُ الْإِسْلَامِ أَمْ لَا  “Maulamaa wameafikiana kuwa hairuhusiki kwa Makhalifah wawili kuchaguliwa katika kipindi kimoja, ima Dola ya Kiislamu iwe ishaenea au la.” Imam Al-Haramain (Al-Juwaini) amesema katika kitabu chake Al-Irshad kuwa, قَالَ أصحابنا لا يجوز عقدها شخصين قَالَ وَعِنْدِي أَنَّهُ لَا يَجُوزُ عَقْدُهَا لِاثْنَيْنِ فِي صُقْعٍ وَاحِدٍ وَهَذَا مُجْمَعٌ عَلَيْهِ  “Watu wetu wamesema haijuzu kwa watu wawili kuchaguliwa kuwa Makhalifah katika wakati mmoja. Akasema, na rai yangu ni kuwa haijuzu kwa watu wawili kuchaguliwa katika ardhi moja. Na hii imeafikiwa juu yake.”

Mtume (saw) amesema, «فَمَنْ أَرَادَ أَنْ يُفَرِّقَ أَمْرَ هَذِهِ الْأُمَّةِ وَهِيَ جَمِيعٌ، فَاضْرِبُوهُ بِالسَّيْفِ كَائِنًا مَنْ كَانَ» “Yeyote anayetaka kufarikisha mambo ya Ummah huu wakati umeungana, basi muuweni kwa upanga, yeyote awaye.” [Muslim]. Kuhusiana na Hadithi hii, An-Nawawi amesema katika Sharhi yake, فِيهِ الْأَمْرُ بِقِتَالِ مَنْ خَرَجَ عَلَى الْإِمَامِ أَوْ أَرَادَ تَفْرِيقَ كَلِمَةِ الْمُسْلِمِينَ وَنَحْوَ ذَلِكَ وَيُنْهَى عَنْ ذَلِكَ فَإِنْ لَمْ يَنْتَهِ قُوتِلَ وَإِنْ لَمْ يَنْدَفِعْ شَرُّهُ إِلَّا بِقَتْلِهِ فَقُتِلَ  “Hapa kuna amri ya kumpiga vita anayetoka kwenye utiifu wa Imam au anayetaka kufarikisha mambo ya Waislamu na mfano wake. Amekatazwa hilo, na kama hatakoma atauliwa, na kama shari yake haitoweza kuzuiwa ila kwa kuuliwa basi atauliwa.” Kiasili, Ummah huu wa Kiislamu hutakiwa kuunganishwa, chini ya mamlaka moja-Khilafah. Adhabu ya kisheria kwa yeyote anayetaka kuigawa na kuikata vipande vipande na kuwa vijidola vidogo vidogo, anauliwa.

Hitimisho: Khilafah ni Njia ya Kivitendo ya Kuunganisha Ummah wa Kiislamu

Ni Dini hii tukufu ya Kiislamu pekee iwezayo kumaliza migogoro inayoendelea inayozushwa na dola za kitaifa. Uislamu umeweka udugu wenye nguvu unaoegemea juu ya lengo sahihi la mwanadamu, kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt). Inachukulia mgawanyiko baina ya watu juu ya msingi wa nasaba, ukabila na utaifa kwa ukali wa hisia za imani. Uislamu umeweka mamlaka moja juu ya Ummah wa Kiislamu na kukataza mgawanyiko wake.

Khilafah ambayo itarejea karibuni inshaAllah katika wakati ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameuridhia kutanua Nusra Yake, kutuunganisha kivitendo. Itasimama katika moja ya maeneo ya Waislamu, juu ya msingi wa Uislamu na sio juu ya msingi wa utaifa. Khilafah kwa Njia ya Utume itafanya kazi ya kuunganisha maeneo yote ya Ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola moja iliyo na nguvu. Itawalingania Waislamu wote, kutoka Indonesia hadi Morocco, kama Uislamu unavyowalingania wakiwa waumini, katika udugu mmoja. Itafanya kazi kuondoa mipaka ya dola za kitaifa ambayo imewagawa na kuwadhoofisha Waislamu kwa muda mrefu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu