Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 8 Sha'aban 1444 | Na: HTY- 1444 / 15 |
M. Jumanne, 28 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuamiliana na Riba bado Kunafanywa katika Benki za Yemen Badala ya Kuizuia
(Imetafsiriwa)
Mazungumzo kuhusu riba na biashara ya riba katika benki za Yemen yamerejea tena katika kurasa za Gazeti la Al-Thawra, kama ilivyoeleza katika toleo lake la 21278 lililotolewa mnamo Jumanne, 1 Sha'ban 1444 H sawia na 21/02/2023: “Kulingana na imani na uwajibikaji wa kitaifa, kuna mwelekeo mkubwa nchini Yemen katika ngazi ya uongozi wa mapinduzi na kiuchumi kuweka kikomo cha miamala ya riba katika benki na miamala ya kifedha.”
Miaka tisa baada ya Mahouthi kunyakua madaraka jijini Sana'a, bado wanaamiliana na riba, kuchukua na kutoa, kwa mujibu wa mfumo wa kibepari wanaoamiliana nao kama watawala wengine wa nchi za Kiislamu, licha ya tuhma zao kwa mfumo wa kibepari na ufisadi wake, mchana na usiku! Maneno yao pekee, katika mihadhara yao na shughuli za kitamaduni, ndiyo huzuia! Walisema, “Tunahitaji kushughulikia moja ya matatizo hatari na mabaya zaidi ya kiuchumi yanayowakilishwa na riba.” Benki Kuu, Kituo cha Uchumi, na Idara ya Fatwa zilifanya mageuzi na hatua za kukomesha miamala ya riba, kama alivyosema Hashim Ismail, gavana wa Benki Kuu, “Benki imesimamisha karibu 70% ya ukubwa wa deni la umma kwa miamala ya riba, na ni 30% pekee ndilo lililosalia. Na ikiwa tutakubaliana, kwa ajili ya hoja, kwamba miamala ya riba katika benki za Yemen ipunguzwe, je, miamala ya riba katika deni la nje kutoka kwa benki na mifuko ya kikanda na kimataifa, zinazoongozwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki, zitasimamishwa?
Aina na miundo yote ya miamala ya riba haiishii kwa utabikishaji wa hatua kwa hatua wa Uislamu, kwa kutekeleza sehemu moja na kuacha sehemu nyengine, haijuzu kwa mujibu wa Sharia, na dalili ya hilo ni uthibitisho wa kukatikiwa, dalili ya kukatikiwa, kama ilivyo dhahiri katika kauli yake Mola Mtukufu:
[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ]
“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’idah 5:49]. Mtume Mtukufu (saw) alikataa miito ya viongozi wa Maquraish ya kumtaka akubali hata baadhi ya hukmu za Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo katika uharamu wa riba na kuamiliana nayo. Hakuna daraja, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Kitabu chake cha Kihakika:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِنْ تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ]
“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Al-Baqara 2: 278-279]. Bali ni haramu kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu moja kwa moja, nayo ni kwa kuuondoa mfumo mzima wa uchumi wa kibepari, kuanzia katika kubainisha tatizo la kiuchumi na kumalizia na masuluhisho ya kiuchumi, na kutumia hukmu za Uislamu katika nyanja zote za maisha, ambapo tunajua fika kwamba serikali za Sana'a na Aden hazitasubutu kuchukua uamuzi wa kutabikisha Uislamu; kwa sababu uamuzi si wao, kwa sababu wao si chochote ila tu vibaraka wa Magharibi kafiri katika utabikishaji wa mifumo ya kibepari sio hivi karibuni. Ingawa kuacha kuamiliana na riba haimaanishi kwamba wametabikisha Uislamu, kwa sababu utabikishaji Uislamu unaweza kufanywa kwa mpigo mmoja tu na katika nyanja zote za maisha.
Wenye wazo la utabikishaji wa hatua kwa hatua wa Sharia ndio njia ya mwisho kwa dola kuu za makafiri kuwawasilisha kwa umma baada ya barakoa kupomoka kutoka kwenye nyuso za kisekula, wakati mahitaji muhimu zaidi ya Umma yamekuwa ni utabikishaji wa Uislamu. Kupitia fikra hiyo ovu, Waislamu wanahakikishiwa kwamba utawala huo umekuwa katika mikono ya kuaminika inayotamani Uislamu kwa sababu sura yao ni ya Kiislamu! Hivyo basi, wazo la utabikishaji wa hatua kwa hatua halina thamani, na mabadiliko ya hatua kwa hatua kamwe hayatawahi kuleta mabadiliko yanayotarajiwa, na mabadiliko ya kweli yatakuwa tu kupitia mabadiliko msingi, ya kina na kamili, na hii itakuwa tu chini ya kivuli cha Khilafah inayotabikisha Uislamu kama mfumo na katiba ya maisha; Hizb ut-Tahrir haizungumzii suluhisho hili kifikra pekee, bali inafanya kazi usiku na mchana baina ya Ummah na pamoja nao, na imetayarisha ala zinazofaa kwa hilo, ikiwemo mwelekeo kamili wa dola kuanzia na rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah, ambayo ina vifungu vya dola vilivyovuliwa kutokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake (saw) na kwa nguvu ya dalili. Tunamuomba (swt) tuwe miongoni mwa mashahidi na wanajeshi wake.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |