Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  19 Rabi' I 1444 Na: HTY- 1444 / 04
M.  Jumamosi, 15 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, Watu Huyaamini Matibabu ya Wagonjwa Wao
(Imetafsiriwa)

Mkasa mpya nchini Yemen unaregea na kuibua hali ya hasira na kutaka maafisa wawajibike, baada ya vifo vya watoto 18 wanaougua saratani ya damu katika hospitali ya Kuwait jijini Sana'a, baada ya kupatiwa dawa zilizokwisha muda wake. Vyombo vya habari vya Yemen viliripoti vifo vya watoto 18 katika siku tofauti tofauti baada ya kupewa dawa iliyokwisha muda wake mwishoni mwa Septemba iliyopita katika kitengo cha matibabu ya saratani katika Hospitali ya Kuwait. Bado kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka, huku watoto wengine waliotibiwa kwa dawa ya methotrexate, iliyotengenezwa na kampuni ya India, wakihamishwa na wangali wako katika uangalizi maalum wa hospitali kadhaa za Sana'a, baada ya dawa hizo kusambazwa na mamlaka za matibabu chini ya udhibiti wa Mahouthi baada ya kudungwa dozi hiyo na kuonekana matatizo juu yao.

Ingawa Uislamu umetunza afya na kuiona kuwa ni sehemu ya uchungaji wa nguvu za Waislamu, Uislamu uko makini juu ya usalama wa miili ambayo mishipa ya afya na siha hutiririka ndani yake, na kwa hivyo unapambana na maradhi, ukiitisha madawa, na kubuni mbinu mbalimbali za kuzuia magonjwa; Hivyo basi, Uislamu umeifanya dawa kuwa miongoni mwa maslahi na huduma ambazo dola ni lazima ifanye, kwa sababu ni miongoni mwa mambo ambayo inapasa kuyalea kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Mtawala ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.”

Umeifanya dola ya Kiislamu kusimamia moja kwa moja utengenezaji na uzalishaji wa dawa na kuwapa wagonjwa ima kupitia kununua, au kupitia kuanzisha viwanda vya dawa vinavyozalisha dawa zinazohitajika. Na kwa sababu dawa ni hitaji muhimu ambalo uhaba au hasara yake inaweza kusababisha madhara kwa mtu binafsi na kundi, dola hufanya kila juhudi ili kujitosheleza katika utengenezaji wake, ili isihitaji kuagiza kutoka nje, na hivyo kuanikwa kwa ulaghai kutoka kwa nchi za Kikafiri au mashinikizo yao ya kisiasa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

(وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً)

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisaa‘:141].

Iwapo watu binafsi au serikali itaagiza dawa kutoka nchi nyingine, dawa zilizoagizwa kutoka nje lazima zifanyiwe uchunguzi na uchambuzi na wanafamasia na wanakemia nchini kabla ya kutoa leseni inayoruhusu uagizaji wake, hasa kutokana na kwamba makampuni ya kimataifa ya dawa hayakusita hapo zamani kuuza shehena ya dawa mbaya kwa Waislamu.

Kilichotokea katika Hospitali ya Kuwait kinaonyesha huduma duni, ikiwa sio ukosefu wake. Dawa zilizokwisha muda wake na mbaya ziliingia Yemen kupitia moja ya bandari, iwe ya nchi kavu au baharini. Pia ni kawaida yake kupita katika vyombo na maabara zenye uwezo wa Wizara ya Afya hadi iruhusiwe kuletwa nchini au kuangamizwa. Wale wanaoziagiza kutoka nje wanawajibika, na makampuni hayo yanayozalisha matibabu hayo ni haramu, pamoja na kuruhusu matumizi yake au la.

Enyi Watu wa Yemen: Hii itabaki kuwa hali yenu na hali ya wagonjwa wenu, wazee kwa vijana, wanaofanyiwa majaribio juu yao kama wanyama na panya, na kudungwa dawa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuchambuliwa, na jinai za waliofanya hivi dhidi ya watu wasiojulikana zitarekodiwa. Hasa pale wafanyibiashara wa dawa hizi wanapokuwa ni watu wenye ushawishi au mawakala wao ambao hamu yao tu ni kupata faida ya kimada kwa gharama ya maisha ya wagonjwa, na ni Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume pekee ambayo Hizb ut. Tahrir inafanya kazi kwa ajili yake ndiyo itakayokomesha vitendo hivi na uhalifu na kucheza na maisha ya watu. Pia imeunda sera ya afya na nini kinatakiwa kufanywa, katika kitabu kilichotolewa hivi karibuni kiitwacho “Sera ya Huduma ya Afya katika Dola ya Khilafah,” ambayo itatekelezwa kivitendo pindi Khilafah itakaposimamishwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Kwa hiyo, shirikini katika kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kheri hii kubwa ili kupata furaha ya duniani pamoja na Akhera.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu