Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  23 Jumada I 1442 Na: HTY- 1442 / 17
M.  Alhamisi, 07 Januari 2021

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

            Mahdi Al-Mashat Aliota!!

Na Pindi alipoamka, Alikataa Mchana Peupe Kubeba Mas'uliya kwa Wale Aliowateuwa Yeye Mwenyewe kama Mtawala Wao
(Imetafsiriwa)

Yule anayeitwa Mkuu wa Afisi ya Upeo ya Kisiasa jijini Sanaa, Mahdi Al-Mashat, katika ujumbe aliamuru viongozi wa Wizara ya Afya kuitambua hospitali ambayo inajumuisha utaalamu maarufu zaidi katika kila vitengo vya magatuzi yaliyo chini ya udhibiti wa wanamgambo wake, na pia alimwita, kwa kumuelekeza afungue maduka ya dawa katika kila kituo cha afya ili kutoa dawa kwa raia kwa bei ya gharama ya kununulia. (Gazeti la Al-Thawra 05/01/2021). Haya yamejiri katika mkutano mpana wa ushauri wa viongozi wa Wizara ya Afya mnamo 04/01/2021, mbele ya Waziri wa Afya, Taha Al-Mutawakel, aliyedai mwaka jana kuwa janga la virusi vya Korona, endapo litaingia Yemen, litaathiri watu milioni 28.

Ni kipi kinachomtofautisha Mahdi Al-Mashat kutoka kwa Ali Saleh na Abd Rabbu Hadi? Yeye ni kama wale waliomtangulia madarakani. Hawakujenga na hawatajenga hospitali hata moja, na walipokwisha kuchoshwa na kutafuta njia, waliachana na jukumu hilo na kulibandikiza kwenye sekta ya kibinafsi. Hospitali zote nchini, haswa hospitali za "Al-Jumhuri, Al-Thawra, Al-Sab'een, na Kuwait" katika mji mkuu, Sanaa, hazikujengwa na watawala mtawalia au serikali mtawalia kutoka 1962 hadi leo, zote ni michango, na hospitali zote nchini Yemen ni kiwango chao. Aidha, hospitali hizi haziwapi watu Utunzaji unaohitajika, kwani maelfu ya watu huenda nje ya nchi kupata matibabu!

Ewe Mashat! Hustahili kuwajali wale walioruka juu ya vichwa vyao kwa nguvu kupitiaa baraka na msaada wa Amerika, na ulidai kuwa unatawala kwa Uislamu. Maagizo yako yalibeba ndani yake ruhusa kwa dori ya sekta ya kibinafsi katika kuanzisha vituo vya afya, ambao ndio msingi, na ilitajwa katika gazeti lenyewe, "Alidokeza kuwa agizo hilo litasimamisha ufadhili wowote kutoka kwa fedha za umma kwa nyanja yoyote katika jimbo ambayo inalingana na uwekezaji uliofanikiwa katika sekta ya kibinafsi kwa ujumla na haswa hospitali. Kuelezea umuhimu wa kuandaa mkakati wa kuendesha hospitali kutokana na mapato yao. "Ni jambo la kusikitisha lakini pia la kuchekesha." Hospitali za Saleh zilikuwa uwekezaji wa Uingereza, wakati hospitali za Al-Mashat bila shaka itakuwa ni uwekezaji wa Amerika. Watu nchini Yemen ni Waislamu, na wanahitaji huduma ya afya iliyowekwa na Uislamu, sio kama katika urasilimali ambao maoni yako hupitishwa, Mashat! Mawazo haya yako katika urasilimali, ndio katika urasilimali. Je! Hujui, Mashat, kwamba dawa ni jukumu la serikali katika Uislamu, kama elimu na usalama, ambayo inapaswa kutoa kwa raia wake wote? Tuna hakika kuwa hujui au kwamba mabwana zako wanakuchorea mstari ambao hutauvuka. Mtume wa Mwenyei Mungu (saw) alipewa daktari kama zawadi, na yeye (saw) akampeana kwa Waislamu, pindi alipoipokea zawadi hiyo, hakuitumia wala kuichukua, lakini aliijaaliya kwa Waislamu. Huu ni ushahidi kwamba daktari ni miongoni mwa maslahi ya Waislamu, kisha angalia historia ya Waislamu katika siku ambazo tulikuwa na khalifa na Khilafah na jinsi walivyokuwa wakitafuta matibabu huko bimaristan. Yako wapi mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi ewe Mahdi, kama unavyosema?! Au jambo hilo sio zaidi ya maneno tu bila ya vitendo?! Mwenyezi Mungu (swt) asema:          

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لا تَفْعَلُونَ * كَبُرَ مَقْتاً عِنْدَ اللَّهِ أَنْ تَقُولُوا مَا لا تَفْعَلُونَ]

“Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda? *Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.” [As-Saff: 2-3].

Hakika Mahdi Al-Mashat anaota, kama kawaida, kwa sababu jana alizungumza juu ya kulipa nusu ya mshahara kwa wafanyikazi wa sekta ya umma mara kwa mara kila baada ya miezi miwili, na alipoamka, alirudi nyuma na akajuta, kwa hivyo alitoa nyudhuru na kuomba msamaha, na yeye pia anafanyo vivyo hivyo katika kuainisha hospitali katika kila wilaya ya Yemen, na ilhali hajui jumla ya wilaya za Yemen! Na alipogundua idadi ni kubwa, alikataa jukumu hilo na kuliweka kwenye sekta ya kibinafsi, ambayo sehemu nzuri yake kubwa, kwa kweli, sio ya eneo hilo! Wacha watu wa Yemen wajue kuwa watawala hawa ni vibaraka wasaliti ambao lazima wapinduliwe na kwamba Khilafah Rashida ya pili ambayo Hizb ut-Tahrir inafanya kazi kuisimamisha ndiyo itakayo watibu watu. Mtume (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” [Imesimuliwa na Ahmad kutoka kwa Nu`man bin Bashir]. Kwa hivyo, fanyeni kazi pamoja na wale wanaofanya kazi ya kuisimamisha.

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu