Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  23 Rajab 1445 Na: 1445 / 10
M.  Jumapili, 04 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wajibu wa Serikali ya Uzbekistan kwa Palestina, Gaza na Al-Aqsa
(Imetafsiriwa)

Miezi minne imepita tangu Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Mujahidina wana wa Palestina mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu. Inafahamika kwamba Mayahudi waliolaaniwa hawakuikalia kwa mabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa tu, bali tangu wakati huo wamekuwa wakitekeleza sera ya kikatili ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa huko. Kwa vile jeshi la umbile la Kiyahudi tayari limethibitisha hofu yake ya kukabiliana na mujahidina shupavu katika mapambano ana kwa ana, wanaweza tu kujibu kwa kuwachinja raia wa Gaza, hasa wanawake na watoto, kwa ukatili na unyama usio na kifani... haya yote na huku nchi za dunia hususan watawala wa nchi za Kiislamu wamekuwa watazamaji tu, na mauaji ya kikatili yanayofanywa na jeshi linalokalia kwa mabavu bado yanaendelea kwa msaada wa kijeshi na kifedha wa dola za Kikafiri zinazoongozwa na Marekani. Wanachofanya watawala wa Kiislamu sio tu kuwasaliti watu wa Gaza na Palestina, bali ni uhalifu na uhaini. Usaliti wao umefichuliwa kwa ulimwengu mzima, hata kwa Waislamu wajinga kabisa na wale waliokuwa na ufahamu mdogo wa kisiasa. Cha kusikitisha, serikali ya Uzbekistan ni miongoni mwa walioiacha ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, Gaza, na Al-Aqsa bila ushindi wowote, na bado inachukua msimamo sawa na serikali hizo kuhusu kutatua suala la Palestina. Inaunga mkono suluhisho lake ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa kupitia mazungumzo na njia za kidiplomasia, na inasisitiza mradi wa "raia wawili - dola mbili" kama suluhisho pekee! Lakini ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, kama sehemu ya ardhi za Umma wa Kiislamu, kamwe haitauzwa, na hakuna hata shubiri moja yake itakayopeanwa.

Hakuna suluhisho kwake isipokuwa kwa msingi wa Sharia, na si vyenginevyo. Hukmu ya kisheria ni kuwa ni lazima isafishwe kabisa kutokana na Mayahudi wachafu, na Msikiti wa Al-Aqsa lazima ukombolewe. Uhalisia unaonyesha kwamba ili umbile la Kiyahudi liondolewe katika ardhi ya Palestina, ni lazima majeshi ya Waislamu yakusanywe mara moja kwa mujibu wa hukmu ya Sharia, “Chochote ambacho wajib haikamiliki isipokuwa kwacho pia ni wajibu.” Aidha Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[وَإِنِ ‌اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal 8:72].

Hukmu hii ya Sharia inatekelezeka, bila shaka, kwa Uzbekistan, ambayo ni sehemu ya nchi za Kiislamu. Kwa hiyo, serikali ya Uzbekistan lazima ikusanye jeshi lake ili kuikomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa. Lakini inaweza kusemwa kwamba kuna mipaka kadhaa kati ya Palestina na Uzbekistan, ikimaanisha kuwa haiwezekani kwa vikosi vya Uzbekistan kuwafikia bila vizuizi kutokana na eneo la kijiografia lililopo!

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa hukmu ya Sharia, majeshi ya Kiislamu yaliyo karibu zaidi na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na adui lazima yasonge mbele hadi kupata ushindi kwanza. Kwa hiyo, majeshi lazima yakusanywe na kutumwa kusaidia watu wa Gaza na Palestina, kwanza nchi jirani za Palestina, kama vile Jordan, Saudi Arabia, Misri, Syria na Uturuki.

Hata hivyo, pamoja na hayo, lau serikali ya Uzbekistan ingelikusanya jeshi lake na kufanya juhudi zake kufika Palestina, ingelitekeleza wajibu wake wa Sharia, na sio tu kwamba ingekutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama ikiwa na ushahidi mkononi mwake, bali pia ingepata ushindi mkubwa na endelevu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ingefikia heshima ya jeshi la ushindi katika ulimwengu huu pia. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu huwapa ushindi wale wanaopigana kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ] “Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye.” [Al-Hajj 22:40].

Hata kama serikali ya Uzbekistan itatoa hoja kwamba haiwezi kufanya hivyo kwa sababu ya udhaifu wake, kuna idadi ya hatua ambazo inapaswa kuchukua dhidi ya Mayahudi, na ina uwezo kamili wa kuzitekeleza. Hizi ni:

1. Kutangaza kutolitambua umbile la Kiyahudi.

2. Kutambua kwamba kadhia ya Palestina sio tu kadhia ya Mashariki ya Kati, bali ni kadhia ya ulimwengu mzima wa Kiislamu, na kwamba suluhisho pekee sahihi kwake ni kuregea katika utawala wa Sharia, na kwamba mradi wa “raia wawili - dola mbili” hauna msingi wa kisheria, kwa sababu ni utambuzi wa wazi wa umbile la Kiyahudi linalokalia kimabavu.

3. Kukata mahusiano yoyote ya kidiplomasia na umbile la Kiyahudi, kufunga ubalozi wake katika nchi yetu na kuwafukuza wafanyikazi wake wote, akiwemo balozi, pamoja na kuufunga ubalozi kule na kumrudisha balozi.

4. Kukata mahusiano ya kiuchumi na nyanja nyingine zote ambazo zinasaidia kuimarisha umbile la Kiyahudi, ikiwa ni pamoja na kuwarudisha zaidi ya raia 10,000 nchini Uzbekistan.

5. Kueleza umuhimu wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa kwa Waislamu wa nchi yetu, na kuweka nafasi maalum na hadhira kubwa kwenye vyombo vya habari kwa wanazuoni wa Kiislamu watakaofasiri kwa usahihi kadhia hii kwa mtazamo wa Sharia.

6. Ili kuhakikisha kuwa kadhia ya Palestina haiko mbali na fikra za Waislamu, na kwamba inazingatiwa daima, serikali inapaswa kumwamuru mufti kuwapangia maimamu wa misikiti kazi maalum katika suala hili.

7. Kutoa usaidizi wote unaohitajika kutekeleza mipango binafsi, kama vile maandamano, matembezi, nk., kama ishara ya kuunga mkono ukombozi wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa.

8. Kuzishajiisha nchi jirani za Kiislamu kutekeleza hatua zilizotajwa hapo juu kuhusu kadhia yenye baraka ya Palestina na kuchukua msimamo sahihi wa kisheria katika suala hili.

Serikali ya Uzbekistan, wakiwemo wanazuoni, wanaweza kufanya jambo hilo hilo kuhusiana na ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Kwa kweli, hizi ni hatua za muda, na suluhisho la kweli ni kuhamasisha jeshi, kama tulivyoonyesha hapo juu. Ikiwa serikali ya Uzbekistan itaanza kutekeleza hatua zilizotajwa hapo juu kama wajibu wa Sharia, itapata msaada wa ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa watu wetu wa Kiislamu, Mwenyezi Mungu akipenda. Hakuna shaka kwamba watu wetu watafurahia hatua hizi na wataiunga mkono na kuisaidia serikali kwa kila njia. Mwishowe, serikali ikiwa mwili mmoja na roho moja na watu wake, itaweza kufanya mambo makubwa! Mwenyezi Mungu (swt) hatawadhalilisha waja wake Waislamu wanaofuata amri zake mbele ya wakoloni wa Makafiri kama vile Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China, ambao wanaendelea kuunga mkono umbile la Kiyahudi katika nyanja mbalimbali. Bali Mwenyezi Mungu (swt) ataziimarisha hatua zao na ataharakisha ushindi wao waliokuwa wakiungojea kwa muda mrefu, Mwenyezi Mungu akipenda! Kinachohitajiwa ni kumcha Mwenyezi Mungu Peke Yake, kumtegemea Yeye Peke Yake, na kutafuta msaada kutoka Kwake Peke Yake!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ ‌تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 47:7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu