Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  15 Rabi' I 1443 Na: 1443 / 06
M.  Ijumaa, 22 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hukmu ya Kushiriki katika Uchaguzi wa Uraisi wa Jamhuri
(Imetafsiriwa)

Kushiriki katika uchaguzi wa urais mnamo 24 Oktoba ni haramu kwa Waislamu. Na dalili ni: mfumo uliowekwa katika Shariah ni mfumo wa Khilafah. Mfumo wa kijamhuri ambao msingi wake ni mfumo wa kidemokrasia sio mfumo wa serikali katika Uislamu. Mtu atakaye kuwa kiongozi wa dola lazima atimize matakwa saba: awe ni Muislamu, mwanamume, aliye baleghe, mwenye akili timamu, huru na mwadilifu, na kwamba pia awe na uwezo wa kutekeleza majukumu ya serikali. Iwapo sharti lolote kati ya haya halikutimizwa ndani ya mtu, kwa mujibu wa hukmu za Shariah ya Kiislamu, basi mtu huyo huenda asiwe mkuu wa dola. Ama mfumo ni lazima atabikishe mfumo wa Uislamu na hukmu zake kwa sababu utekelezaji ni dori ya mkuu wa dola na dori ya watu ni kuhakikisha kuwa sheria ya Mwenyezi Mungu inatekelezwa kikamilifu. Iwapo atatangaza waziwazi na bila kusita kwamba atatabikisha hukmu za Uislamu, anaweza kuchaguliwa. Sheria za Uislamu ambazo ni lazima zitabikishwe ni pamoja na kutangaza mfumo wa Khilafah, kuziunganisha nchi za Kiislamu chini ya dola ya Khilafah, kuzikomboa ardhi za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu na makafiri kutoka kwa uvamizi na ushawishi wao katika nyanja zote za maisha, na kuubeba Uislamu duniani.

Ikiwa tutamtazama Rais wa sasa Shavkat Mirziyoyev na wagombea wengine wa urais, ni wazi kwamba hakuna hata mmoja wao anayetangaza wazi kwamba anataka kutabikisha hukmu za Uislamu na kusimamisha Khilafah kwa mara nyingine tena, ambayo ni wajibu kutoka kwa Mola wetu na chanzo cha nguvu zetu. Au wanataka kuzitakasa nchi za Kiislamu kutokana na ushawishi wa kigeni na kuregesha utulivu, umoja na utajiri wao. Kwa hivyo, hakuna hata mmoja wao anayepaswa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa dola. Maadamu wagombea hawa wanalenga kushikamana na katiba ya kisekula na kutetea mfumo wa kijamhuri wa kisekula na kula kiapo cha utiifu kwake, kushiriki katika uchaguzi wao kunamaanisha kulinda katiba hii isiyo ya Kiislamu, ushawishi wa nchi za kigeni za makafiri, ufisadi uliokithiri nchini, nk na kuwasaidia watawala kuhukumu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremsha, na Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha Waislamu kuhukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [Yusuf: 40].

Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma’ida: 49].

Na mtawala aliye Muislamu lakini hahukumu kwa Uislamu ni dhalimu na fasiki:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Ma’ida: 45].

Na Yeye (swt) asema:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” [Al-Ma’ida: 47]. Lakini kukanusha na kukataa kutawaliwa na Uislamu na kuuona kuwa haufai, ni ukafiri, tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu (kutokana na hilo). Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“a wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Al-Ma’ida: 44].

Enyi Waislamu wa Uzbekistan: Jiepusheni na dhambi kubwa la kushiriki katika chaguzi hizi, na acheni kutumaini kwamba kupitia mabadiliko tu ya watu walio madarakani kutakuwa na mabadiliko ya kweli. Kama mnavyojionea wenyewe katika uhalisia maadamu mfumo wa demokrasia unabaki - hata marais na watawala wabadilike kiasi gani - haitawaletea manufaa yoyote. Kinyume chake, hali yenu inazidi kuwa mbaya kila uchao. Ni wakati sasa wa kutambua kwamba njia pekee ya wokovu ni kuachana kabisa na mfumo potofu na wa kidhalimu wa leo na kufanya kazi ya kurudisha uhai wa mfumo wa Uislamu.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu