Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  6 Rabi' II 1445 Na: 1444 H / 04
M.  Jumamosi, 21 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa nini Tunaandamana kwa ajili ya Palestina Nje ya Ubalozi wa Misri na Uturuki?

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Uingereza ilifanya maandamano nje ya ubalozi wa Misri na Uturuki jijini London leo (21 Oktoba 2023).

Bango letu la kuu linafanya mukhtasari ni nini maandamano haya yanahusu - "Majeshi ya Waislamu! Waokoeni watu wa Palestina”.

Wazayuni wameikalia kimabavu Palestina kinyume cha sheria kwa miaka 75, wakiungwa mkono na kipote cha wakoloni wa Magharibi. Wapalestina wamekuwa chini ya ukandamizwaji wa kikatili, kuzingirwa, utekaji nyara na mauaji ya wanaume, wanawake, watoto, na wazee wao kwa wakati huu wote.

Tunatoa wito kwa jeshi jirani la Misri kupuuza maagizo ya Marekani na kibaraka wao Sisi; kusonga kuelekea kwenye mpaka na kuwaokoa kaka na dada zao wa Palestina kutoka kwa ugaidi wa serikali dhalimu ya Wazayuni.

Tunatoa wito kwa jeshi jirani la Uturuki kurekebisha mapuuza ya msaliti Erdogan; Ili kuwasaidia ndugu zao wa Jeshi la Misri katika kuwaokoa kaka na dada zao wa Palestina, na wasiruhusu mtoto mwengine asiye na hatia kuuawa na wanyakuzi na walowezi haramu tena.

Tunatoa wito zaidi kwa watu waaadilifu ulimwenguni kudai kuondoka wa majeshi yote ya Magharibi kutoka kanda hiyo, kuondolewa msaada wote wa kifedha kwa Wazayuni, pamoja na watawala wa Waislamu pambizoni ambao ni watetezi wao wakubwa. Wakati umewadia wa kumaliza uvamizi huu wa kihalifu ambao ni chukizo dhidi ya wanadamu. Wakati umefika kwa Waislamu wa kanda hiyo kuregesha Khilafah kwa njia ya Utume (saw), kuleta amani na uadilifu wa kudumu katika kanda hiyo na ulimwengu kwa mara nyingine tena.

Kwa habari zaidi kuhusu ulinganisi wetu tafadhali tembelea tovuti yetu  www.hizb.org.uk

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uingereza

Video ya Amali

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu