Afisi ya Habari
Uingereza
H. 9 Rabi' II 1443 | Na: 1443/02 |
M. Jumapili, 14 Novemba 2021 |
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Visimamo vya Hizb ut Tahrir / Uingereza kwa ajili ya Wauygur Wanaokandamizwa Jijini London na Manchester
(Imetafsiriwa)
Waislamu nchini Uingereza walijitokeza kwa wingi katika Ubalozi wa China jijini London, na Ubalozi mdogo wa China jijini Manchester, kuandamana dhidi ya unyanyasaji wa kinyama wa ndugu zao na dada zao wa Uyghur mikononi mwa serikali katili ya China.
Ukatili mwingi uliofanywa dhidi ya Waislamu wa Turkistan Mashariki ulifichuliwa katika kauli za umati.
Dkt Abdul Wahid, mwenyekiti wa kamati ya tekelezi ya Hizb ut Tahrir Uingereza, alijenga hoja juu ya hili kwa kutoa matumaini na suluhisho la kweli la kumaliza mateso yao.
Aliwakumbusha Waislamu kwamba sisi sote ni sehemu ya Ummah mmoja wa kiulimwengu na kwamba Waislamu hapa walikuwa wakitoa sauti zao, nyoyo na dua zao kwa ajili ya ndugu na dada zao huko Turkestan Mashariki.
Wakati huo huo, alizungumzia kuhusu kutelekezwa kwa watu wa Uyghur na watawala jirani wa ardhi za Kiislamu, ambao walitanguliza maslahi yao binafsi, badala ya kuchukua hatua ya kuwaokoa waliodhulumiwa kutoka kwa madhalimu - na kwamba bila Khalifa anayetawala kwa Uislamu huko, ambapo hakuna ngao kwa Umma wa Kiislamu.
Mtume (saw) ameripotiwa kusema: «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتِلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma na hujihami kwayo.”
Alitoa ujumbe kwa Amerika, Wavamizi wa Kizayuni nchini Palestina, na serikali ya Modi nchini India- ambao wote bila aibu wanatumia mateso ya Uyghur kwa malengo yao wenyewe - kana kwamba tunapaswa kusahau ukandamizaji wao dhidi ya Waislamu katika 'Vita dhidi ya Ugaidi', huko Palestina na Kashmir. Alisema kuwa kimsingi wote ni sawa, na wanatofautiana tu katika mitindo na viwango. Alieleza kuwa Amerika ilifadhili makundi ya upinzani nchini Iraq na Syria kutumia mateso yao - na hatari kwa Waislamu kuingizwa katika ajenda zao. Dkt Abdul Wahid alisema, "Tunajitangaza kuwa huru na ajenda yenu."
Ujumbe wake wa mwisho ulikuwa kwa serikali ya Chama cha Kikomunisti cha China. Alieleza kwamba watawala wasaliti wa ardhi za Kiislamu watakapoondolewa na kusimamishwa tena Khilafah kwa njia ya Utume, hapo ndipo Ummah chini ya Amiri muongofu utakumbuka yote haya - na Wachina wanapaswa kufikiria wakati huo watanunua Mafuta na Gesi wapi; na mradi wao Ukanda na Barabara wakati huo utaenda wapi basi?
Hatimaye ulinganizi ni lazima uwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, ili kufichua madhalimu na kusimamisha mamlaka ambayo yatasimamisha uadilifu na kuzuia dhulma yao.
[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui!”[Yusuf 12:21]
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk |