Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  13 Rabi' II 1444 Na: 06 / 1444
M.  Jumatatu, 07 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Unyang'anyi wa Kombe la Dunia ni Dhihirisho la Mfumo wa Kibepari!

(Imetafsiriwa)

Kombe la Dunia la 2022 linakaribia kuanza na kwa muda sasa vyombo kadhaa vya habari vya Magharibi vimeikashifu Qatar na FIFA kwa sababu nchi hiyo haiheshimu haki za binadamu.

Tangu tangazo la 2010 kwamba Qatar itakuwa nchi mwenyeji kulizuka mabishano mengi kuhusu namna nchi hiyo ilivyochaguliwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022. Kulingana na FBI ya Marekani wanachama kadhaa wa FIFA walihongwa na Qatar ili kushinda uchaguzi huo. Bodi ya FIFA kila mara imekuwa ikikanusha madai ya rushwa lakini pamoja na hayo, mwenyekiti wa FIFA wakati huo alijiuzulu.

Qatar ni nchi tajiri kiasi kutokana na rasilimali zake za mafuta. Idadi kubwa ya watu ni wafanyikazi wahamiaji, asilimia 15 pekee ya watu ndio kiasili wanatoka Qatar. Licha ya utajiri wake mkubwa inajulikana kuwa tangu kuanza kwa ujenzi wa viwanja vya mpira wa kandanda, wafanyikazi wahamiaji hufanya kazi katika mazingira magumu. Kufanya kazi kwa siku nyingi katika joto kali la kiangazi kwa ujira mdogo, wafanyikazi wanatenganishwa na familia zao bila siku za kupumzika, kwa miezi kadhaa. Makao yao ni duni na yakudhalilisha kusema kwa uchache.

Kulingana na mashirika kadhaa ya haki za binadamu unyonyaji wa wahamiaji unaofanywa na Qatar husababisha maelfu ya vifo. Hii ni bila kuzingatia wale wafanyikazi ambao wanakabiliwa na uharibifu wa kudumu wa kimwili na maradhi thakili, ambapo hawapati aina yoyote ya fidia au huduma ya matibabu. Mwitiko wa mwenyekiti wa FIFA Gianni Infantino na Katibu Mkuu Fatma Samoura ni wa kushangaza kusema kwa uchache. Katika barua ya ndani iliyotumwa kwa vyama vya soka vya kitaifa vya nchi 32 zinazoshindana, FIFA ilizitaka nchi hizo "kuzingatia kandanda" na "kutoingiza kandanda katika kila aina ya migogoro ya kisiasa na kifikra".

Ukandamizaji na unyonyaji wa wafanyikazi wahamiaji nchini Qatar si chochote zaidi ya dhihirisho la mfumo wa kibepari ambamo wanadamu wananyonywa ili kupatikana faida ya juu kabisa. Vyombo vya habari vya Magharibi vinajaribu kudokeza wazo kwamba ukandamizaji unahusishwa na Uislamu. Ukweli hata hivyo ni kwamba ukandamizaji huo ni matokeo ya moja kwa moja ya ubepari kwa sababu Qatar haitawaliwi na Uislamu bali na mfumo wa kirasilimali.

Kwa mara nyingine tena ni wazi kwamba maisha ya binadamu katika nchi za Kiislamu hayana thamani kubwa kwa kipote cha mabwenyenye wa Magharibi. Wale wanaohusika na hafla ya kandanda wanayaita maelfu ya vifo kwa urahisi, sehemu ya mzozo ambao haupaswi kuharibu hali ya kupendeza ya kandanda. Ni kwa kuregeshwa tena kwa Khilafah kwa njia ya Utume pekee katika nchi za Kiislamu ndipo heshima na haki za mwanadamu zitalindwa kikweli.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu