Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  27 Rabi' I 1446 Na: 1446/05
M.  Jumatatu, 30 Septemba 2024

Wapambe wa Utawala wa Tunisia Waruhusu Huduma za Kijasusi za Mossad na za Kigeni Kuenea Nchini humu na Kuwatesa Wanawake wa Tunisia Kwa Sababu ya Kuiunga Mkono kwao Gaza!
(Imetafsiriwa)

Matembezi ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia hayajasimama tangu kuzuka kwa Kimbunga cha Al-Aqsa (Tufan Al-Aqsa), huku matembezi yakifanyika kila Ijumaa kuanzia Msikiti wa Al-Fath hadi ukumbi wa michezo wa Manispaa katika mji mkuu yakitoa wito kwa Ummah na majeshi yake kwenda kuinusuru Gaza.

Katika hali inayojitokeza mara kwa mara katika matembezi mengi yanayoandaliwa na Hizb, Mashababu huhangaishwa na usalama, hasa ufuatiliaji wa wale wanaotoa hotuba wanapokuwa njiani wakirudi, ima kwa kuwaita kwenye vituo vya usalama au kuwaitisha vitambulisho vyao kana kwamba wanashukiwa kufanya vitendo vya uhalifu!

Katika kisimamo chetu kilichopita cha Ijumaa, Septemba 27, 2024, ambacho kiliambatana na upanuzi wa mashambulizi ya kihalifu ya umbile la Kiyahudi na kuwajumuisha watu wetu nchini Lebanon pamoja na Gaza, mmoja wa wanawake huru wa Tunisia kutoka kitengo cha wanawake ya Hizb ut Tahrir alitoa hotuba ambayo ndani yake aliamsha hisia za wana wa Ummah na kuwalenga watu wenye nguvu kutoka kwa majeshi na maafisa kwa wito wa uhamasishaji wa jumla, kuwanusuru ndugu zao katika Dini, ili kumfukuza adui katili, na kuzisafisha dhamiri zao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Baada ya hotuba hiyo kukamilika, kundi la wanausalama walimwandama dada huyo na mumewe kwa kilomita moja wakiwa njiani kurudi na kuwasimamisha katika kundi la vijana waliokuwepo kwenye matembezi hayo. Kisha, mmoja wa askari wa usalama akamwendea yule dada katika umati huo, na kumwomba mwongozo kuhusu utambulisho wake, anwani yake, na mada ya hotuba hiyo...nk, katika hali ya kusikitisha, kuhuzunisha inayofanya paji la uso la mtu kuwa na haya!

Hapa tunauliza: Je, ni kwa maslahi ya nani uhangaishaji huu wa mara kwa mara wa kila anayeiunga mkono Gaza na kuyataka majeshi ya Umma kulitokomeza umbile halifu la Kiyahudi linalowaua watu wetu katika nchi kipenzi ya Palestina na kulipua mabomu Lebanon, Yemen na Syria? Je, mtawala wa Tunisia na vyombo vyake vya usalama anataka ukamataji na uwekaji vikwazo hivi ili kupata cheti cha tabia njema kutoka kwa mfumo wa kigaidi wa kihalifu wa kimataifa?!

Sasa hivi vyombo vya usalama na mamlaka yao makubwa viko wapi kutokana na harakati za mhalifu Balozi Mzayuni wa Marekani Joey Hood anayetamba nchini bila uwajibikaji wala usimamizi?! Na wako wapi na idara za kijasusi za nje zinazotamba nchini?! Na wako wapi na Mossad ambayo imekuwa ikizunguka huru nchini Tunisia kwa miaka arobaini, ikiwaua Abu Jihad na Mohamed Zouari, shahidi wa Ummah?! Halafu vipi kuhusu orodha ya wanachama 400 wa Mossad waliojificha nchini Tunisia, ambayo iliandikwa na gazeti la Al-Shorouk la Algeria zaidi ya miaka kumi iliyopita, na orodha inaendelea?!

Udhalilifu na uovu wa utawala wa Tunisia umefikia hatua ya kuwaruhusu maadui wa Ummah kuzurura nchini humu, na wakati huo huo wakiwatesa wanawake wake huru kwa sababu ya uungaji mkono wao kwa Gaza na Palestina,

[قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!” [At-Tawbah 9:30]

Ukamataji, uhangaishaji na kuwekwa kizuizini hakutadhoofisha wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir. Kwao wao, kadhia ya Palestina ni kadhia ya majaaliwa ambayo inahitaji kukusanywa kwa majeshi na kuondolewa viti vya khiyana vya utawala vinavyolinda umbile la Kiyahudi. Juhudi hizi hazitakoma mpaka Mwenyezi Mungu atakapoupa Ummah huu jambo la uongofu, ambalo ndani yake itasimamishwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na moja ya vipaumbele vyake itakuwa ni ushindi wa Gaza na ukombozi wa kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu.” [Ar-Rum 30:4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu