Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 10 Muharram 1446 | Na: 1446/01 |
M. Jumanne, 16 Julai 2024 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza nchini Tunisia
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir ya Wilaya ya Tunisia inaomboleza kifo cha mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir, mbebaji Da’wah kutoka kizazi cha kwanza katika safu zake, mwanachuoni wa lugha, Mwenyezi Mungu amrehemu, inshaAllah:
Al Arousi Bin Amara
Ambaye alifariki kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu (swt) mnamo siku ya Jumapili tarehe 14 Julai 2024, akiwa na umri wa miaka 84. Ami yetu Al-Arousi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alijiunga na dawah mwanzoni mwa miaka ya sabiini. Alikuwa mbebaji dawah ya Uislamu popote aliposafiri na kuishi, akifanya kazi kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Alikuwa mwalimu na khatibu kwa watu katika misikiti, hafla, na mikusanyiko. Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa mmoja wa mishale ya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu.
Aliishi kwa kutimiza ahadi yake na Mwenyezi Mungu (swt) hadi dakika za mwisho za maisha yake na akafa ipasavyo. Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu maiti zetu na azijaalie Mabustani Mapana kuwa makazi yake. Inna lillah wa Inna Ilaihi Rajiun (Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutarejea). Mwenyezi Mungu awalipe mema familia na jamaa zake na awape subira na faraja. Tunasema tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt). Ni cha Mwenyezi Mungu anachotoa, na ni Chake anachokichukua, na kila kitu amekadiria majaaliwa yake.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |