Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 23 Dhu al-Hijjah 1443 | Na: 1443/31 |
M. Ijumaa, 22 Julai 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Haina Haja na Kura ya Maoni na Inapinga Mchakato wa Kisiasa Unaoendeshwa na Ukoloni
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Alhamisi, Julai 21, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia ilisisitiza msimamo wa kimfumo wa Hizb ut Tahrir unaopinga katiba zilizotungwa na mwanadamu zinazotawala kinyume na yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu. Hakuna tofauti kati ya katiba ya 2014 na katiba ya 2022, ambayo Rais Qais Saeed aliwasilisha kwenye kura ya maoni mnamo Julai 25, 2022, na akasema kupitia video iliyorekodiwa kuwa Hizb ut Tahrir haina haja na suala la kura ya maoni na haijali kuhusu rai ya vyama vya kisiasa vinavyoiunga mkono au kuikataa, kwani haitaki kusimamisha utawala wa kiumbe kwa viumbe, bali kwa kuthibitisha utawala wa Muumba, Aliyetukuka, ambao ndio inayoendelea kuufanyia kazi tangu kuanzishwa kwake hadi leo.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia imeeleza kuwa kanuni msingi ya katiba kwa Waislamu ni kuwa ni katiba ya Kiislamu inayotokana na Quran na Sunnah kwa ajili ya dola ya Kiislamu ambayo itikadi yake ya Kiislamu ndio msingi wake na msingi wa katiba na sheria zake. Sheria ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, Mwenye nguvu na Mtukufu, na si kwa kiumbe, namna itakavyokuwa hadhi, cheo au wadhifa wake. Amewakumbusha Waislamu kwa jumla na watu wa Tunisia hasa wajibu wao wa kufanya kazi ya kutabikisha sheria ya Mola wa walimwengu wote na kuwaunga mkono wale wanaotabanni katiba ya Kiislamu kwa dola ya Kiislamu yenye kutabikisha Uislamu.
Hizb ut Tahrir hapo awali itoa onyo mnamo mwaka 2014 dhidi ya katiba ya Bunge Maalum la Katiba, ambayo iliwaacha watu wake bila chochote isipokuwa taabu na dhiki, na kisha kutoka kwa uchaguzi wa rais na wabunge wa 2019, ambapo ilionyesha kuwa kushiriki kwao ni uhalifu na upaji nguvu ukoloni kupitia kuunda tabaka la wanasiasa linalotumikia maslahi ya dola za Kimagharibi, na kuonya dhidi ya kuchaguliwa kwa Qais Saeed Kabla ya raundi ya pili ya uchaguzi wa rais, na ilimwona kuwa uso uliopambwa wa utawala huu wa kisekula. Inatoa wito upya leo wa kukataa mchakato wa kisiasa unaosimamiwa na ukoloni na inaolenga kuuondoa Uislamu kutoka kwa utawala na sheria, na kuweka mfumo wa kisasa wa kisekula na kubadili ushawishi wa kigeni kwa ushawishi mwingine wa kigeni. Kwa upande mwingine, inatoa wito wa kutekelezwa na kutabikishwa katiba ya Hizb ut Tahrir kivitendo, ambayo inatokana na Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume (saw) kama suluhisho pekee la matatizo yote yanayoikumba Tunisia ili watu wake waweze kuwa na furaha duniani na Akhera.
Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]
“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah: 50].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |