Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 18 Rabi' I 1443 | Na: 1443/10 |
M. Jumamosi, 02 Oktoba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uingiliaji wa Nje: Uhalifu wa Dola Tete na Mazingira ya Kisiasa Yaliyooza
(Imetafsiriwa)
Katika kivuli cha upuuzi wa kisekula, Tunisia imekuwa zaidi ya hapo awali kitovu cha uingiliaji wa nje na uwanja wa mizozo ya kimataifa. Mnamo siku ya Alhamisi, Oktoba 21, Bunge la Ulaya lilipiga kura juu ya azimio la hali nchini Tunisia, ambapo lilitaka kurejea kwa haraka kwa asasi za serikali na demokrasia, kuanza tena kwa shughuli za bunge, kuheshimu Katiba ya 2014, kutangaza ramani ya utendakazi iliyo wazi, kuzindua upya mazungumzo ya kina ya kitaifa, kumaliza mashtaka ya kijeshi ya raia na kuhakikisha haki sawa kwa wanawake na wanaume katika nyanja zote, ikiwemo urithi.
Ilitanguliwa na kikao cha Alhamisi, 14 Oktoba, katika Bunge la Congress la Amerika, ambapo Kamati Ndogo ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ilikutana katika kikao cha mtandaoni kilichoitwa, "Tunisia: Kuchunguza Hali ya Demokrasia na Hatua Zinazofuata za Sera ya Amerika" ambapo ilionya dhidi ya hali ya demokrasia nchini Tunisia na kusema kuwa "inakabiliwa na hatari," bila kusahau wajumbe wa Amerika na Ulaya wanaotembelea Tunisia bila kukoma na ukiukaji wa mabalozi wa kigeni wa ubwana na uamuzi wa kisiasa wa nchi hii.
Mabwana wajanja wa Kimagharibi hawangeingilia mambo ya ndani ya Tunisia lau si udhaifu wa tabaka la kisiasa (watawala na upinzani), ambalo linaitukuza Magharibi na kutambua utawala wake juu ya nchi na kuweka uwepo wake juu ya msingi huo. Mijumuiko ya umma katika viwanja na watawala ya kabla na baada ya taratibu za tarehe 25 Julai 2021, ni ujumbe kwa duru za Magharibi ili kupata uungwaji mkono wao katika kurejesha chama kimoja au kunusurika kwa kingine madarakani, hata Rais Kais Saied, ambaye alipinga uingilia huu, lakini aliupinga kwa sababu haukuwa katika upendeleo wake. Alikuwa wa kwanza kufuja ubwana wa nchi hiyo alipowaita mabalozi wa Umoja wa Ulaya walioidhinishwa nchini Tunisia tarehe 23 Februari 2021, na kuwaambia kuhusu ukosefu wa utulivu wa kisiasa nchini Tunisia, na akamhakikishia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mnamo Oktoba 2 kwamba serikali mpya itaundwa ndani ya siku chache na kwamba mazungumzo ya kitaifa yatazinduliwa hivi karibuni, ambayo huzingatiwa katika desturi za kidiplomasia kama ufujaji ubwana wa nchi.
Hatua hizi zilifichua mtazamo wa nchi za Magharibi wa Tunisia kama kolono iliyo chini ya ushawishi wake ambayo haipaswi kukengeuka kutoka kwa mstari wa kisiasa uliochorewa. Vile vile walifichua kwamba mzozo baina ya tabaka la kisiasa (watawala na upinzani) si chochote ila ni mvutano wa kimataifa wa kung'ang'ania ushawishi kwa kutumia zana za ndani, hivyo sisi katika Hizb ut Tahrir hatujishughulishi na tabaka hili la kisiasa, liwe ni mfuasi wa nidhamu ya ukoloni ya Ufaransa au mfuasi wa usimamizi wa Kiingereza au Amerika, kwa sababu vita vyetu halisi ni kwa ukoloni wenyewe, na tunafanya kazi ya kuutokomeza kwa kuung'oa, ili kamwe tusirudi tena baada ya hapo, kwa mchakato wa mabadiliko ya kina ambayo yanajumuisha kuubomoa mfumo waliotulazimishia juu yetu, na kusimamisha utawala wa muongofu kwa msingi wa Uislamu. Mabadiliko haya yanaathiri katiba na sera na mabadiliko ya mazingira ya kisiasa ya mteja na vyombo vinavyolinda mfumo huu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]
“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma’ida: 51].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |