Afisi ya Habari
Tunisia
H. 13 Muharram 1443 | Na: 1443/02 |
M. Jumamosi, 21 Agosti 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kais Saied na Uhuru wa Uamuzi wa Kisiasa!!
(Imetafsiriwa)
Kwa kuzingatia hatua za kimataifa na za kikanda za kuishawishi hali ya kisiasa ya Tunisia, haswa baada ya maamuzi ya tarehe 25 Julai 2021, Rais Kais Saied alisisitiza uhuru wake katika Kasri la Carthage mnamo Alhamisi, tarehe 19 Agosti 2021, akisema, "Watu hawa wanaozungumza juu ya maamuzi ninayochukua kutegemea vipimo hadaifu vichwani mwao kwa sababu wanaishi kwa uhadaifu pekee, ninayafanya (maamuzi) kulingana na ukinaifu wangu, kwa kuzingatia kuitikia mahitaji ya watu wa Tunisia, na hakuna mtu yeyote atakayeyaingilia, kwa sababu sitashikiliwa mateka na mtu yeyote.”
Sisi katika Hizb ut Tahrir tunafahamu kwamba Rais Kais Saied alianza utawala wake akiwa huru katika ufanyaji maamuzi, lakini hivi karibuni alishawishiwa na hali ya kisiasa inayotukuza Magharibi na kuutambua utawala wake juu ya nchi hii na haja ya kupata msaada wake na utegemezi juu yake. Kwa hivyo, alihamisha mwelekeo wake na kuingia mikononi mwa Ufaransa, ambayo ilimuunga mkono na washirika wake wengine hadi alipoweza kudhibiti serikali na kuwaangusha wapinzani wake, vibaraka wa Uingereza, mnamo Julai 25, 2021, baada ya kuamsha na kufasiri Sura ya 80 ili kuelekea katika kubadilisha muundo wa serikali kutoka kuwa wa nusu bunge kuwa wa uraisi. Tunakumbusha Rais Kais Saied juu ya baadhi ya matakwa ya watu wa Tunisia na maamuzi kadhaa ambayo yanatafsiri uhuru wa uamuzi wa kisiasa, pengine ataonyesha ikhlasi yake katika kile anachodai na atarekebisha kile alichokosa:
1 .Mnamo tarehe 17 Disemba 2010, watu wa Tunisia walitaka kuangushwa kwa mfumo wa serikali wa kisekula wa Kimagharibi uliosababisha shida, mateso, ufisadi na upendeleo ya kikabila, na kuubadilisha na mfumo mpya ambao utafikia haki na maisha bora na kuikomboa nchi kutokana na ushawishi wa Ukoloni wa Magharibi. Kuangushwa kwa mfumo wa serikali wa Magharibi na kujitenga kutokana na pingu za jamii ya kimataifa ambayo ndio shina la msiba, kunaweza kupatikana tu kupitia Uislamu ndani ya muundo wa mradi wa kisiasa ambao unavuka mipaka ya kisiasa, kitaifa na kikanda, huku, kuendelea kulinda mfumo wa kisekula ni ubabaishaji kwa watu wa Tunisia kutokana na kufikia malengo ya mapinduzi yao matukufu ya mabadiliko msingi, na uzalishaji wa serikali ile ile ambayo watu waliasi dhidi yake.
2. Kujitenga na nchi za kikoloni na taasisi zao za kifedha, kukataa kujibu shinikizo za kimataifa, na kukataa misaada na mikopo ya kimataifa kutoka kwa benki zao, ambazo zimeitumbukiza nchi hii katika madeni na kuweka rehani uamuzi wake wa kisiasa. Kwani uhuru kutoka kwa ushawishi wa Magharibi ya kikoloni ndio hatua ya kwanza ya kurudisha tena mamlaka na kumiliki uamuzi..
3. Watu wa Tunisia walitaka kurudishwa kwa utajiri kutoka kwa kampuni za uporaji za kikoloni katika kampeni ya Wino Petrol. Pia walitaka kukomeshwa kwa mikataba iliyoufanya utajiri wetu kufujwa na makafiri, na kutaka kuregeshwa kwa ubwana wao juu ya ardhi yao yote, kamili na usiokoma.
4. Kufutiliwa mbali kwa makubaliano ya kijeshi na nchi za kilafi za kikoloni katika nchi yetu, haswa makubaliano yaliyoifanya Tunisia kuwa mshirika mkubwa wa Amerika nje ya NATO, na ambayo yaliifanya Tunisia kuwa kituo cha juu cha jeshi la Amerika AFRICOM barani Afrika, kwa sababu makubaliano haya yanaathiri ubwana wa nchi hii na kuimarisha ushawishi wa kigeni.
5 .Kukomesha uingiliaji waziwazi wa mabalozi wa kigeni katika maelezo ya kina ya maisha ya kisiasa na kuzuia kuajiri kwao wanasiasa na mashirika ya kijamii.
6. Kufutiliwa mbali kwa makubaliano na Shirika la Kifaransa, ambalo limeifanya Tunisia kuwa kituo cha juu cha nguzo muhimu zaidi za uvamizi wa kifikra eneo la Afrika Kaskazini.
7. Kukomesha uhuru wa Benki Kuu uliolazimishwa na Ulaya na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa juu ya Tunisia.
Hii ndio ncha ya siwa barafu ya kile Rais Kais Saied anaweza kufanya kuonyesha kiwango cha ikhlasi yake katika kile anachodai cha uhuru wa uamuzi wake wa kisiasa, na tunajua kwamba tofauti kati ya kile alichomo ndani yake sasa na kile tunachomlingania kwake ni jambo kuu, lakini mpito kati yao ni rahisi kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu (swt) humrahisishia, na kwa yule aliyetimiza sharti lake moja tu, ambalo ni ikhlasi ya nia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtegemea Yeye sawasawa. Na tunakukumbusha juu ya maneno ya Al-Faruq Omar, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ambaye unamchukulia kama mfano wako: “Hakika, Mwenyezi Mungu ametupa izza kupitia Uislamu. Ikiwa tutatafuta izza kwa kitu chengine kisicho kuwa kile ambacho Mwenyezi Mungu ametupa izza kwacho, basi Mwenyezi Mungu atatudhalilisha”.
]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tunisia |
Address & Website Tel: http://www.ht-tunisia.info/ar/ |