Afisi ya Habari
Tunisia
H. 1 Jumada I 1442 | Na: 1442/23 |
M. Ijumaa, 18 Disemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Maadhimisho ya Miaka Kumi ya Mapinduzi, Mamlaka Inatenda Ujambazi!
(Imetafsiriwa)
Kama kawaida, katika kufuatilia harakati za Hizb ut-Tahrir na kuzuia amali zake, tangu asubuhi ya Alhamisi, 17 Disemba 2020 M, vyombo vya usalama mjini Sidi Bouzid zimefuatilia makao makuu ya Hizb na kufuatilia nyendo za mashababu kupitia mawakala waliovaa nguo za raia na wakaifanya kuwa shughuli yao iliyo washughulisha mno ya kuikabili Hizb na kuidhibiti.
Mara tu mashababu hao wawili, Muhammad al-Ahmadi na Saber Jabili, walipoondoka makao makuu, walifuatiliwa na kuripotiwa kwa kikundi kingine, ambacho kwa haraka kiliwasimamisha na kuwakamata bila ya sababu yoyote, kisha kuwapeleka katika eneo la usalama, ambapo walifanyiwa uchunguzi, na kisha wakawekwa chini ya ulinzi ili kuwasilishwa kwa mwendesha mashtaka ya umma mnamo siku ya Ijumaa.
Hakika sera ya uonevu na kubuni mashtaka zinazofuatwa na dola ya kiaskari, ambapo imekuwa ndio njia yake ya kuamiliana kwa njia ya kudumu na Hizb ut-Tahrir, inaonyesha kutokuwa na uwezo kwake na kufeli mbele ya fikra ya wakati wake na chama cha kimfumo ambacho kinasukuma hatua zake kufikia lengo lake, ambalo ni kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume; Ahadi na bishara njema, hili halitaiongezea Hizb isipokuwa nguvu tu, na kwa mashababu wake isipokuwa uthabiti tu na azma, na kwamba namna itakavyofanyiwa unyonge na kuzibwa pumzi, mashababu wa Hizb wamemuahidi Mwenyezi Mungu kusonga mbele kufikia radhi za Mwenyezi Mungu, na hakuna kizuizi chochote kitakachowazuia kufikia lengo ambalo wamekula kiapo kujitolea kwalo.
Tunaikumbusha mamlaka na mawakala wake kwamba dhulma ni giza Siku ya Kiyama na kwamba ni bora kwao kutubu mikononi mwa Mola wao na kuunga mkono mradi wa Ummah ambao Hizb ut-Tahrir inaubeba, na kujiepusha na miradi ya Magharibi na wafuasi wao.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal : 24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tunisia |
Address & Website Tel: http://www.ht-tunisia.info/ar/ |