Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  9 Jumada II 1438 Na: 1438 / 03
M.  Jumatano, 08 Machi 2017

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Tunakemea Kuteswa kwa Vijana wa Hizb ut Tahrir Zanzibar

Hizb ut Tahrir Tanzania inakemea kwa ukali dhidi ya ukatili, unyama na mauwaji yaliyo fanywa na kundi la watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walio washika na kuwatesa vijana watatu wa Hizb ut Tahrir mnamo 1 Machi katika sehemu ya Kiboje, Eneo la Kusini mwa Zanzibar.

Wanamgambo hao waliojihami (wakiwa na sare) bila ya kuonyesha vitambulisho waliingia kwa nguvu katika kijiji hicho mwendo wa saa nane mchana, baadhi yao waliizunguka nyumba (waliyokuwamo vijana hao) kwa silaha kana kwamba walikuwa ni maadui wa jeshi, kisha kuwakamata Juma Muarab, Ibrahim Silima na Said Mohammed, wakawafunga pingu, kuwaziba nyuso zao, kuwaingiza kwa lazima ndani ya gari hadi eneo lisilojulikana ambapo waliwapa mateso ya kinyama, kihalifu na yasiyo elezeka. Mwishowe waliwaachilia siku hiyo hiyo takriban mwendo wa saa nne usiku na kuwaonya kutojihusisha na kutoshirikiana na Hizb ut Tahrir. 

Kitendo hiki ni cha kikatili, cha aibu na cha uoga kwani wanamgambo hao walitekeleza maovu yao huku wakiwa wamezificha nyuso zao kwa waathiriwa hao na kukosa hata ujasiri wa kujitambulisha. Fauka ya hayo, ni dhihirisho wazi la uadui mbaya dhidi ya Uislamu na Waislamu licha ya kuwa idadi yao ni wengi miongoni mwa wakaazi wa visiwa vya Zanzibar.

Zaidi ya hayo, kuwepo kwa wanamgambo kwa muda mrefu nchini Zanzibar na vitendo vyao vya kinyama na kinyume na sheria mchana peupe bila ya kukemewa au kuhesabiwa kupitia hatua madhubuti za dola kunatia shaka kuwa katika oparesheni zao wanapata baraka kamili kutoka kwa Jeshi la Polisi bila ya kutaja kutumiwa na wanasiasa.

Tunawaomba wote walio na chembe ya utu na hisia ya uadilifu kukemea kwa ukali na kupinga kitendo hiki cha kimgambo cha kinyama ambacho kinavuruga zaidi uwiano wa kijamii.

Tunawakumbusha wanamgambo, wasaidizi wao na wafuasi wao kuwa uovu huu kamwe hautasamehewa wala hautasahaulika.

وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ * مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ﴿

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu.” [Ibrahim: 42-43]

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu