Afisi ya Habari
Tanzania
H. 11 Dhu al-Hijjah 1439 | Na: 1439/04 |
M. Jumatano, 22 Agosti 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Tanzania ilituma Ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan Jijini Dar es Salaam
Kufuatia utekaji nyara wa aibu kwa dada yetu Romana na Dada Roshan pamoja na mumewe kulikotekelezwa na Mamlaka ya Pakistan kwa sababu tu wanaunga mkono ulinganizi (da'wah) wa Kiislamu kupitia Hizb ut Tahrir, Hizb ut Tahrir / Tanzania mnamo 20 Agosti 2018 ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan nchini Tanzania kuukabidhi taarifa mbili kwa vyombo vya habari kuhusiana na suala hilo hasa.
Ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Tanzania ulijumuisha Masoud Msellem, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir nchini Tanzania, na Kaema Juma, Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Tanzania.
Mkuu wa Ubalozi huo (Bw. Amir Khan) alizipokea taarifa hizo, na kuzisoma kidogo tu wakati wa kuzipokea, na kuahidi kuzifikisha kwa serikali yake nchini Pakistan.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) katika siku hizi tukufu kuwaondolea mateso na kuwaadhibu wale walio wakosea Dada zetu Romana na Roshan na mume wake na Waislamu wote wanao dhulumiwa Mashariki na Magharibi.
Ni wakati sasa kwa madhalimu ikiwemo mamlaka ya Pakistan kuzingatia kwa uangalifu na kuwa makini na onyo kali la Quran Tukufu:
﴾وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ * مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ﴿
“Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim: 42-43]
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |