Afisi ya Habari
Tanzania
H. 26 Safar 1446 | Na: 1446 / 02 |
M. Ijumaa, 30 Agosti 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miradi Mikubwa katika Nchi Changa Haipo Kuhudumia Raia
(Imetafsiriwa)
Majibu ya karibuni ya serikali Bungeni kupitia Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga kuhusiana na kupunguza gharama za umeme kwa sababu ya kuanza uzalishaji umeme katika Bwawa la Kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) ni kauli ya kuvunja moyo sana.
Majibu ya Naibu Waziri huyo kwamba ati tayari gharama za umeme zilizopo nchini Tanzania ni hafifu ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki kutokana na serikali kuweka ruzuku kwa watumiaji, na ati kwamba bei iliyopo tayari serikali imeingiza ruzuku.
Sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tungependa kutamka yafuatayo:
1. Chini ya mfumo wa kibepari miradi hususan mikubwa kama Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere kamwe haipo kuhudumia ustawi wa raia, bali ipo kwa maslahi ya mabepari na wanasiasa waroho, bila ya kuwa na hisia yoyote ya kuwajali wananchi. Miradi hiyo na mfano wake imepachikwa jina na kuitwa ‘miradi ya kimkakati’ ikisemwa kwamba lengo lake ni kuja kusaidia raia. Tahamaki mambo yapo kinyume kabisa (haisaidii)
2. Ni jambo la aibu sana kwa wanasiasa wa nidhamu ya kidemokrasia ya ubepari namna wanavyocheza ‘tiki taka’ za kisiasa (kufanya ujanja) katika mambo nyeti, wanasiasa hao hutoa kauli za kisanii kwa dhamira ya kubeza maslahi ya Umma. Siasa katika demokrasia sio suala la kuwatumikia raia na kuchunga mambo yao kiuadilifu, bali siasa kwao ni fani ya kujikusanyia utajiri haraka haraka ikiambatana na kauli za kisanii.
3. Katika Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah hali iko tofauti kabisa na ubepari, umeme na mitambo (mikubwa) yote inayozalisha umeme na mfano wake ni mali ya Umma na hairuhusiwi kubinafsishwa, kutaifishwa au kufanywa mali ya serikali.
Kwa hivyo, umeme hupaswa kusambazwa kwa watu wote na jitihada lazima ifanywe ya kupatikana umeme wa kutosha, tena kwa bei rahisi, (kama sio bure) na kamwe hausambazwi umeme kwa msingi wa kibiashara.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |