Afisi ya Habari
Tanzania
H. 19 Safar 1446 | Na: 1446 / 01 |
M. Jumamosi, 24 Agosti 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kadhia ya Ngorongoro:
Changamoto ni Ubepari sio Jamii ya Wamasai
(Imetafsiriwa)
Kufuatia hatua ya serikali za kuwahamisha jamii ya wafugaji wa kimasai katika maeneo ya Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro, sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunalaani hatua hiyo na hatukubaliani na kitendo hicho kiovu. Na zaidi tunapenda kufafanua yafuatayo:
1. Mgogoro wa Ngorongoro baina ya serikali na jamii ya Wamasai ni matokeo ya sera za kibepari za kikoloni ndani ya nchi changa ikiwemo Tanzania ambazo zimezitumbukiza nchi hizo katika dimbwi la migogoro isiyokwisha, iwe ya kiuchumi kama huu, bali pia migogoro ya kisiasa na kijamii. Nchi changa kibubusa huiga fikra za kibepari kwa mashinikizo ya nchi kubwa za kibepari, matokeo yake nchi hizo huingia katika mivutano na raia wao.
2. Fikra ya kibepari ya ‘maslahi’ huchukulia kuongezeka idadi ya wafugaji na mifugo yao (katika mbuga) kwamba ni tatizo, ilhali kiukweli hilo sio tatizo. Kwa kuwa uhai wa mwanadamu hulazimu kutangulizwa kwanza kabla ya wanyama pori.
3. Mfumo wa kibepari umechanganyikiwa katika misingi yake na katika masuluhisho yake. Na kwa muktadha wa jambo hili, umejikoroga katika suala la milki za kiuchumi, ambapo huruhusu milki binafsi za mali za Umma kama mbuga za wanyama, mito mikubwa, maziwa, fukwe nk. ambazo kimaumbile ni kwa ajili ya matumizi ya Umma mzima.
4. Kwa kupitia fikra ya kibepari ya ‘uhuru wa kumiliki,’ mali za Umma huporwa kwa kisingizio cha uwekezaji wa nje na humilikishwa watu binafsi, makampuni au hata kumilikishwa serikali.
5. Dhana ya ‘uhuru wa kumiliki’ na ‘uwekezaji wa nje’ ni fikra zenye sumu kali, hatari na za kinyonyaji kwa wanadamu hususan kwa nchi changa. Kwa kuwa, sio tu hupelekea kumilikisha binafsi rasilmali nyeti za kimaisha ambazo kukosekana kwake hupelekea watu kutawanyika kuzitafuta. Bali pia dhana hizo hupelekea kutiwa vitanzi nchi changa kwa kuingiliwa mambo yao ya ndani, na pia makampuni makubwa ya kibepari huhodhi rasilmali nyeti za nchi kwa msaada wa maafisa waovu wa serikali.
6. Wanaokosoa hatua ya serikali ya kuwaondosha jamii ya Wamasai katika mbuga ya Ngorongoro miongoni mwa wanasiasa hususan wa upinzani na wanaharakati wanafanya ujanja, usanii na kuhadaa Umma, kwa sababu upande mmoja wanajifanya kutokubaliana na hatua za kuhamishwa wamasai, lakini upande wa pili wanaunga mkono, kupigia debe na kukalidi mfumo wa kibepari na demokrasia yake unaohamasisha ubinafsishaji binafsi (wa mali za Umma) na uwekezaji wa nje.
Kwa kumalizia, Hizb ut Tahrir Tanzania tunatoa mwito kwa kila mtu makini kujiweka mbali na mfumo wa kibepari kiukamilifu, na kuweka badala yake mfumo wa Uislamu chini ya dola yake Khilafah.
Masuluhisho ya uadilifu ya Kiislamu yalitekelezwa zama zote za nyuma (Khilafah zilizopita) na yatatekelezwa tena mara Khilafah itakaposimama punde InshaaAllah.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa
Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |