Afisi ya Habari
Tanzania
H. 5 Jumada II 1444 | Na: 1444 / 03 |
M. Alhamisi, 29 Disemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nidhamu ya Elimu ya Kibepari Kamwe Haitoleta Maendeleo Yoyote
(Imetafsiriwa)
Karibuni Shirika la International Development Association (IDA) liliipatia Zanzibar kiasi cha dolari $50 millioni (takriban Sh116.7 billioni) kwa dhamira ya kuboresha uwezo wa ufundishaji na kusaidia kuziba pengo la kijinsia katika mchakato wa kutoka darasa moja kwenda jengine.
Kutokana na mradi huo, imedaiwa kuwa wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 400,000 watapata mazingira mwanana ya kujifunza kupitia taasisi ya kuboresha kiwango cha elimu ya Zanzibar (Zanzibar Improving Quality of Basic Education Project (ZIQUE) inayofadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia.
Zanzibar imeshajaribu hatua mbalimbali kwa lengo la kuboresha elimu, kama kuweka sera mpya ya elimu na mafunzo iliyopitishwa mwaka 2006 inayoitwa “Zanzibar Basic Education Improvement Project”. Pia ndani ya mwaka 2015 serikali iliondoa malipo msingi ya elimu kwa elimu ya awali na elimu ya msingi, na mwaka 2018 ikaondoa malipo hayo kwa shule za sekondari. Hali hiyo ilipelekea kuongezeka kwa usajili wa wanafunzi wapya, ambapo kwa sasa mpango huo unatumikia zaidi ya wanafunzi 467,000.
Hata hivyo, tatizo la Zanzibar na nchi zote zinazoendelea kwa jumla katika suala la elimu ni kukosekana uhuru wa kweli na msukumo wa kimfumo nyuma ya nidhamu zao za kielimu. Kwa hivyo, kuongezeka wanafunzi, kuboresha mbinu za ufundishaji na kutoa inayoitwa elimu yenye kiwango haina faida yoyote kwa kuwa nidhamu ya kielimu yenyewe ni ya kikoloni, kisekula, na ya kibepari yenye lengo la kuzalisha tabaka la vibaraka wa Magharibi na kundi lenye dhamira ya kupapia tu viajira ajira na utumishi kwa malengo binafsi na sio kwa lengo la maendeleo ya Umma.
Nidhamu ya sasa ya kielimu inayotumika katika nchi zinazoendelea ikiwemo Zanzibar haina msukumo thabiti katika upande wa uvumbuzi na ubunifu kuwasaidia watu na kuboresha maendeleo badala yake ni mrundikano wa fikra za Kimagharibi (hadhara) ambazo huwachosha wanafunzi kuhifadhi maarifa yasio na tija, zaidi ya kumakinisha ukoloni mamboleo na hadhara (fikra) za Kimagharibi.
Kinyume na nidhamu ya kielimu ya kibepari, nidhamu ya elimu ya dola ya Khilafah itakuwa na lengo kuu moja tu la kufinyanga shakhisiya/utambulisho wa Kiislamu kwa fikra na matendo. Kwa hivyo, masomo yote na mitaala itawekwa kufikia lengo hilo. Pia dola itamsomesha kila mtu mwanamume na mwanamke yale yote ambayo ni lazima katika maisha jumla, na kutoa elimu bure katika viwango vya msingi na sekondari, na kutoa fursa kuendelea elimu ya juu bure kwa kila mtu kwa kadiri ya uweza wake (dola).
Zaidi ya hayo, dola ya Khilafah itaweka maktaba na maabara na kila mbinu nje kando na skuli za kawaida na vyuo vikuu kuwawezesha wale wote wanaotaka kuendelea na tafiti zao, uvumbuzi na ubunifu katika sekta mbalimbali za kielimu na sayansi ili kuuwezesha Umma kuzalisha mujtahidina (wabobezi) wa kutosha na wanasayansi wa kiwango cha juu.
Muda umefika kufanya kazi ya kurejesha tena Khilafah inayopaswa kuanzia katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuwa ndio dola pekee yenye uwezo wa kimfumo kubadilisha nidhamu iliyopo ya kielimu ambayo ni ya kikoloni na kibepari kwa mbadala wa nidhamu ya Kiislamu.
Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |