Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Sweden

H.  27 Dhu al-Hijjah 1439 Na: 1439 / 09
M.  Ijumaa, 07 Septemba 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kampeni ya Hizb ut Tahrir Nchini Sweden: Tumia sauti yako, lakini sio katika uchaguzi!

Hizb ut Tahrir / Scandinavia imeanzisha kampeni “Tumia sauti yako, lakini sio katika uchaguzi!” nchini Sweden wakati wa msimu wa kiangazi. Ilijumuisha msururu wa amali kama video, ugawanyaji vijitabu vya kampeni, mikusanyiko na maingiliano pamoja na Waislamu.

Risala msingi ya kampeni hii imekuwa ni namna gani Waislamu wanavyo weza kuchangamka katika jamii pasi na kulegeza msimamo wa kitambulisho chao cha Kiislamu.  Kampeni hii na yaliyomo ndani yake imezungumziwa kwa hamu miongoni mwa Waislamu pamoja na mitandao ya kijamii. Imefaulu kuwasilisha barabara mtazamo wa Kiislamu na kuathiri mdahalo kuhusu uchaguzi nchini Sweden na harakati ya kisiasa ya Kiislamu. Kampeni hii pia iliifikia tanabahi kubwa ya vyombo vya habari na imekashifiwa kwa kufanya kazi dhidi ya demokrasia.

Kutokana na hivyo, sisi, Hizb ut Tahrir Scandinavia, tungependa kusisitiza yafuatayo:

1. Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa, kilichojengwa pekee juu ya msingi wa Uislamu, kinachofanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu. Waislamu walioko Magharibi wameanikwa peupe katika shinikizo kubwa la kithaqafa na kisiasa, linalolenga kuwafinyanga Waislamu na kufuta kitambulisho chao cha Kiislamu.

Hivyo basi Hizb ut Tahrir inafanya kazi katika nchi za Kimagharibi kulinda kitambulisho cha Waislamu kupitia kuwaangaza na kuwakuza Waislamu kwa fikra za Kiislamu, pamoja na kuwaunganisha na jamii ya kiulimwengu ya Waislamu na kadhia zao muhimu. Kwa hivyo, Hizb ut Tahrir haifanyi kazi ya kupindua serikali ya Sweden au ya nchi nyengine yoyote ya Kimagharibi.

2. Hizb ut Tahrir haikubali demokrasia kama nidhamu ya utawala, kwa kuwa imejengwa juu ya msingi wa usekula, unaogongana na Uislamu. Demokrasia hupitisha kuwa mwanadamu atunge sheria, huku kwa mujibu wa Uislamu, Allah pekee, Muumba Mwenye nguvu, ndiye aliye na haki ya kutunga sheria. Zaidi ya hayo, tunaizingatia demokrasia kuwa ni nidhamu inayohudumia pakubwa warasilimali na maslahi ya biashara kubwa kupitia ubadilishaji wa serikali. Uvunjaji kiapo ni jambo la kawaida, pindi wanasiasa wanapoenda kinyume na matakwa na matarajio ya wapiga kura wao ili kuwaridhisha mabwenyenye. Uislamu unamiliki nidhamu yake ya kipekee, kamilifu na adilifu, ambayo sisi, katika Hizb ut Tahrir, tunafanya kazi ili kuisimamisha tena katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwalingania Waislamu wote kufanya kazi kwa ajili yake.   

3. Sisi tunayashutumu mazingira yaliyo tawala, ambayo ndani yake Waislamu daima wananyanyaswa, na Uislamu kuoneshwa kama tishio kwa watu. Sisi pia tunapinga jaribio la kinafiki la wanasiasa la kuitumia jamii ya Waislamu, kila wakati wa uchaguzi unapowadia, ili kupata nukta za umaarufu.

4. Kuipinga nidhamu ya Kidemokrasia kamwe haimaanishi kuunga mkono udikteta au kupigia debe kujitenga katika mujtamaa. Hizb ut Tahrir ni mpinzani mkubwa wa udikteta. Maelfu ya wanachama wake wamedhalilishwa, kuteswa na kuuwawa na serikali za kidikteta katika ulimwengu wa Kiislamu.

Hizb ut Tahrir iko dhidi ya kujitenga pamoja na kufinyangwa. Sisi tuko dhidi ya kujitenga, kwa sababu Uislamu unaharamisha Waislamu kutokana na kujitenga kwao katika mujtamaa. Sisi tuko dhidi ya kufinyangwa vile vile, kwani humaanisha kuwa Waislamu waachane na maadili ya Kiislamu. Hili huonekana pindi utiifu unapoitishwa kutoka kwa Waislamu kwa maadili huru ya Kimagharibi; au pindi kwa mfano hijab, matangamano ya kijinsia katika kuogelea, malezi ya watoto ya Kiislamu, na swala katika taasisi za kielimu ima yanapigwa marufuku au kuoneshwa kuwa matatizo kisiasa.

Hizb ut Tahrir hujadili kuwa Waislamu ni lazima wachukue dori ya ujenzi katika mujtamaa, kupitia kujihusisha katika midahalo na Waislamu pamoja na wasiokuwa Waislamu, na kusimama dhidi ya sera na matendo yanayoupiga Uislamu.

                                  Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Scandinavia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Sweden
Address & Website
Tel: 
https://hizb-ut-tahrir.se/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu