Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Rajab 1444 Na: HTS 1444 / 33
M.  Jumapili, 19 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Udhibiti wa Mihadarati na Wasaidizi wake
(Imetafsiriwa)

Leo Jumapili tarehe 19/02/2023 ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ukiongozwa na Ustadh Nasir Ridha Muhammad Othman - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, ukiandamana na Wakili Ahmad Abkar - Mjumbe wa Kamati ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, na Ustadh Abdul Qadir Abdul Rahman - Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano/Wilaya ya Sudan, walikutana na Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Kudhibiti Mihadarati, mbele ya uwepo wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Mkurugenzi wa Idara ya Kiufundi, na Mkurugenzi wa Idara ya Operesheni.

Baada ya kuukaribisha ujumbe hao, mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Nasir, alitoa utangulizi mfupi wa Hizb ut Tahrir, na kuwatambulisha wanachama wa ujumbe huo. Kisha akaeleza kuwa ziara hiyo inajiri ndani ya wigo wa kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ya kupambana na mihadarati, ambayo iliizindua kupitia mkutano na waandishi wa habari katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) mnamo tarehe 22/1/2023, ambayo inajumuisha semina, mihadhara, hotuba, na mikutano na viongozi wa serikali, kila mmoja kulingana na utaalamu wake. Hii ni kuihisabu familia pamoja na serikali ambayo inabeba mzigo mkubwa zaidi, lakini inazembea katika dori hii, lakini badala yake inataka kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na inakaribisha wajumbe wake, katika wakati ambapo umbile hili limeijaza Sudan kwa dawa za kulevya; haliichukulii kuwa biashara pekee, bali linalenga kuharibu jamii, hasa sehemu ya vijana, inayowategemea kwa mabadiliko ya kweli. Madawa ya kulevya - huzingatiwa ni miongoni mwa vita vya kisasa au kile kinachojulikana kama vita vya kizazi cha tano.

Na kwamba suluhisho msingi la kutokomeza mihadarati na vitu vyengine vya haramu ni kwa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Baada ya hapo, Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Kudhibiti Mihadarati alizungumza, akithamini nafasi ya Hizb ut Tahrir katika suala hili hatari, na kupongeza kampeni yake ya kupambana na mihadarati, na akasema: “Nyinyi ni chama cha kwanza cha kisiasa kukutana nasi,” na kwamba hawana pingamizi yoyote ya kushiriki katika amali yoyote ambayo hizb inaiandaa. Aliitaka Hizb ifanye kongamano kuhusu kadhia ya mihadarati, na kusema kuwa watashiriki ndani yake kwa utaalamu wao katika kupambana na dawa za kulevya.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu