Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 29 Jumada II 1444 | Na: HTS 1444 / 26 |
M. Jumapili, 22 Januari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanywa na Shirika la Habari la Sudan (SUNA)
kwa Anwani: Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Yazindua Kampeni ya Kupambana na Mihadarati
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametukirimu kwa akili, na ametufadhilisha juu ya wengi walioumbwa kwa upendeleo, basi akatuongoza kwenye Uislamu, na akatujaalia kutoka katika Ummah wa watu bora zaidi, na swala na amani zimshukie mjumbe kama rehma kwa walimwengu wote, imamu wa wachamungu na bwana wa mitume bwana wetu, kipenzi chetu, na faraja ya macho yetu, Muhammad bin Abdullah, swala na salamu za Mola wangu Mlezi zimshukie, na juu ya jamaa zake na maswahaba zake na mwenye kufuata njia yake mpaka Siku ya Kiyama.
Ndugu wapendwa, Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu:
Baada ya sisi kusikiliza hotuba ya kwanza, na kutambua jinsi mpango wa kuwalenga vijana wa nchi hii ulivyofikia wa kutisha kupitia vita vya dawa za kulevya, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan tunafafanua mambo yafuatayo:
Kwanza: Mwenyezi Mungu Mtukufu amembariki mwanadamu kwa neema ya akili, na amemfadhilisha juu ya viumbe vyake vingi kwa upendeleo, na Uislamu umeifanya akili kuwa moja ya malengo ya juu ya jamii ambayo lazima yahifadhiwe.
Pili: Tangu mwaka 2013, kumekuwepo na ongezeko kubwa la dawa za kulevya zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dolari zikianza kuingia nchini zikiwa kwenye makontena makubwa, kupitia bandari, viwanja vya ndege, vivuko vya ardhini na mipakani mwa nchi, huku idadi kubwa ya nchi zikiwa zile zinazoizunguka Sudan.
Tatu: Kuifurisha Sudan kwa madawa ya kulevya ni moja ya silaha madhubuti katika vita vya kisasa vya kisiasa, ambavyo vinazozaniwa. Vimeainishwa ndani ya vita vya kizazi cha nne, au kizazi cha tano, na kwa hakika ni vita vilivyokusudiwa kumwangusha adui mlengwa kwa ndani, sio kuiangamiza, bali kuitiisha dola yake, kuinyang'anya utashi wake, na sio kuiondoa, na vita hivi havina uwanja maalum wa vita, Bali, jamii yote inayolengwa na adui itakuwa uwanja wake, na ni vita vinavyotegemea raia zaidi kuliko jeshi.
Nne: Sudan inakaribia kuzama chini ya uzito wa vita hivi vya kisasa vya kisiasa, na hii inawakilishwa katika yafuatayo:
- Kulenga fikra na thaqafa ya watu wa nchi hii, kupitia kuulenga Uislamu mtukufu; ambao ni Dini na kutokana nayo dola, na kupandikiza fikra za usekula na ustaarabu, na ni pande mbili za sarafu moja yaani kutenganisha dini na dola, na fikra za demokrasia ambazo zinamaanisha sheria ya wanadamu, na kuacha thamani ya kushikamana na hukmu za kisheria na mifumo ya maisha, na kusonga mbele katika kuwatenga wanawake, na ufisadi wa vijana, yote haya yanapelekea kuanguka kwa ukuta wa ulinzi wa jamii, kwa hivyo inakiukwa na itaanguka.
- Kuifurisha nchini kwa tani nyingi za mihadarati, ambayo ya hivi punde zaidi ilitangazwa Alhamisi iliyopita kuhusu ghala katika eneo la Salih, ambapo tembe bilioni 10 za mihadarati zilipatikana. Ikiwa zitagawanywa kati ya wakaazi milioni 40 wa Sudan, hisa ya kila mtu itakuwa tembe 250! Huu ni ukamataji mmoja tu na yaliyofichwa ni mabaya zaidi!
- Kulenga uungaji mkono wa serikali na misimamo yake, mgawanyiko wa jamii na kuzuia kwake sera za serikali na kufeli kwake.
- Kuanzisha harakati za kisilaha zinazopigana na serikali na kuvuruga mwili wake.
- Kumteua Volcker kama gavana mkuu wa Sudan, kwa kuchora misingi ya masuluhisho yake ya kisiasa, sifa za katiba na sheria zake, na kuwateua watawala wake.
- Balozi za Kimagharibi na mashirika ya kimataifa yamekuwa halali nchini, kuingilia mambo yake ya ndani, kukutana na vyama vya kisiasa na majeshi, yakiwalipa pesa vijana kwa ajili ya madawa ya kulevya, na kilichofichwa ni kibaya zaidi!
- Shughuli ya mashirika ya kiraia ambayo wakoloni makafiri wa Magharibi iliyaunda kwa ufahamu, ili kueneza kuwayeyusha, na kuwaharibu vijana kwa madawa ya kulevya kama mojawapo ya vinara wa vita vya kisasa.
Haya ndio madhihirisho ya vita vya kisasa vya kisiasa vinavyolenga Sudan, ambayo zana zake ni mapango ya adui kutoka kwa balozi za Kimagharibi, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia, na baadhi ya vikosi vya kisiasa, yote haya pamoja na ushiriki kutoka kwa viongozi wa kijeshi.
Na ili taifa letu lifahamu ukweli huu, na hatari ya kuilenga nchi kwa dawa za kulevya, Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan inazindua, kupitia mkutano huu na waandishi wa habari, kampeni kuu ya kupambana na mihadarati chini ya kichwa:
“Mihadarati ni vita na kupitia Khilafah, tutashinda.” Na kampeni hii itaendelea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, katika mwezi wa Rajab Al-Fard, ikiwalenga vijana katika sehemu zao za mikusanyiko, pamoja na semina, khutba za Ijumaa, mihadhara, hotuba za mitaani na Furqan, mikusanyiko ya watu katika sehemu za umma, video, mabango, na mengineyo.
Hatutakuwa washindi katika kukabiliana na vita hivi isipokuwa kwa kuwasili kwa Uislamu safi kwenye utawala hapo ndipo mwili wa umma utakapoanza kufufua mambo yake yenye kinga otamatiki, ili kufukuza uovu wa hadhara ya Kimagharibi, na jamii itaimarishwa kwa kufufua maadili ya kushikamana na kanuni ya Sharia, na kwa kuitekeleza mifumo na sheria za Kiislamu, kujenga ua wa ulinzi dhidi ya njama za adui mjanja.
Na sasa, kabla ya kutangaza Khilafah kwa njia ya Utume, watu katika ngazi ya vyombo vya usalama na kijeshi vya dola, na familia. Baba na mama, vijana, na nguvu hai za jamii, lazima watambue uzito wa jambo hili, na kukabiliana nalo kwa yafuatayo:
Kwanza: Kuwafichua wale wote wanaohusika na kazi hii chafu, bila kujali hadhi zao, kuwahisabu, na kuwawekea adhabu kali zaidi juu yao, ili wawe mfano kwa yeyote anayejijaribu kuingia katika uwanja huu hatari.
Pili: Kushughulika kwa uthabiti unaohitajika na azma kwa bandari, viwanja vya ndege, vivuko, mipaka, nk., na kutokuwa na huruma katika kumwadhibu yeyote anayechangia au kusaidia kuleta dawa za kulevya nchini.
Tatu: Kuweka adhabu za nidhamu za kuzuia, ili kamwe kusiwe na mtu yeyote atakayewahi kufikiria kukuza au kushughulika na dawa za kulevya.
Nne: Utambuzi wa hatari za madawa ya kulevya na ufafanuzi wa Hukm ash-Shari’ kupitia njia zote zilizoko na vyombo vya habari vinapaswa kushiriki katika utambuzi huu.
Enyi vijana wa Ummah, na mashekhe wake, wanaume na wanawake, fanyeni kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwa sababu kwa kukosekana Khilafah, mkoloni kafiri Magharibi imekiuka matukufu yote ya Waislamu, mpaka ikafika kwenye nyoyo na akili za watoto wetu.
Enyi watu wenye nguvu na ulinzi: fanyeni hima kuipa nusra Hizb ut Tahrir ili isimamishe Khilafah na kuikomboa nchi hii kutokana na uchafu wa Kafiri mkoloni, thaqafa yake, na njama zake.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]
Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |