Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 24 Sha'aban 1442 | Na: HTS 1442 / 64 |
M. Jumanne, 06 Aprili 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ndugu Mheshimiwa / Mhariri Mkuu wa Gazeti la Al-Mawakib
Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,
Maudhui: Majibu ya Habari
(Imetafsiriwa)
Tumesoma katika gazeti lenu, Toleo la (271), la Jumatatu 23 Shaban 1442 H, sawia na 05 Aprili 2021 M, makala ya mwandishi Ezz El-Din Saghiroun chini ya anwani: "Kwa mantiki ya Kiislamu: Sudan ni Wilayah ya Kiislamu? Upuuzi gani huu!!", akitoa maoni juu ya taarifa ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan kwa anwani: "Itifaki ya Al-Burhan na al-Hilu juu ya kutenganisha dini kutoka na dola (ambayo kiasili imeshatenganishwa) ni uthibitisho wa utawala wa Amerika juu ya kile kinachoitwa faili ya amani", ambapo makala hayo yaliishambulia Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, na kuchochea serikali dhidi yake, kwa kuongezea matumizi ya maneno ambayo hayafai kwa mwandishi anayetaka kueneza ukweli na haki, kama vile neno (upuuzi) ambalo amelitumia kwenye kichwa cha makala yake ... na kwa mujibu wa haki ya kujibu uzushi na uongo uliokuja katika makala hayo, tunatumai kwa ukarimu na fadhila zenu mtachapisha jibu lifuatalo kwa makala hayo:
Kwanza: Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho kinatokana na itikadi ya Umma; itikadi ya Uislamu mtukufu, na ujasiri wake, sio, kama mwandishi alivyo sema, imetokana na udhaifu wa serikali, bali imetokana na nguvu ya fikra ya Kiislamu, na haogopi serikali wala wale walio nyuma yake katika nguvu za ukafiri zinazoiongoza, na inaonekana kwamba mwandishi haijui Hizb ut Tahrir. Na lengo ambalo Hizb ut Tahrir analilenga ni lengo la kila Muislamu mwenye ikhlasi kwa dini yake na Mola wake. Uislamu umetuamuru tuwe na umoja kwa msingi wake:
﴾إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ﴿
“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya: 92]. Na Mtume wetu mtukufu ni mmoja ametuamrisha tuwe chini ya kivuli cha Khilafah moja:
«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فَتَكْثُرُ»، قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ، فَالْأَوَّلِ، وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»
“Bani Israel siasa zao zikiendeshwa na mitume wao, kila mtume mmoja akiondoka, alifuatiwa na mtume mwengine. Na kwa hakika yake hakutakuwa na mtume wengine baada yangu, kutakuwepo na makhalifa na watakuwa ni wengi. (Maswahaba) wakauliza: watuamrisha nini? Mtume akasema: mpeni ahadi ya utiifu (bay'ah) mmoja baada ya mmoja, na muwape haki yao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya majukumu yao.” (Imepokewa na Muslim). Na sio chini ya kutelekezwa na vijidola vya kitaifa ambavyo mkoloni kafiri alituundia, kuvifanya vidola vinavyo fanya kazi kutumikia ajenda yake, kupora utajiri wa Umma ili makafiri wakoloni waishi kwa raha, na watu katika vidola hivi vya kitaifa wanaishi katika ugumu wa maisha, na vile tunavyoishi Sudan licha ya utajiri wake mkubwa juu ya ardhi na chini ya ardhi ni dalili ya sera hii ya kihalifu.
Pili: Hakuna fungamano linalowaunganisha watu wa jamii na thaqafa tofauti tofauti (kama mwandishi alivyosema) zaidi ya Uislamu mtukufu, ambao umewayeyusha watu na mataifa ndani ya chungu kimoja, na thaqafa moja ambayo ni thaqafa ya Kiislamu, na watu wa Sudan wa makabila tofauti tofauti hawana thaqafa zaidi ya thaqafa ya Uislamu, kwani wao ni Waislamu, na Uislamu ndio unaowaunganisha. Lakini Magharibi Mkoloni kafiri ndio inayotaka kuwarudisha Waislamu kwenye zama za mwanzo za ujinga, ambapo watu hujitofautisha kwa misingi ya rangi na kabila, na kwa bahati mbaya baadhi ya Waislamu wameangukia kuwa windo kwa udanganyifu huu, na wanaimba misemo hii bila ufahamu!
Tatu: Mwandishi anakusudia kuwadanganya wasomaji kwamba Khilafah ipo, na kwamba Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ni sehemu ya Khilafah hii, kisha mwandishi anajiuliza: "Ikiwa Khilafah hii ni katika Astana ya zamani ... au ni Khilafah mpya inayo kwenda pamoja na Abu Bakr al-Baghdadi", kisha anahitimisha kwa kusema: "... ni upuuzi gani huu!!"
Tunamwambia mwandishi kuwa Khilafah haipo ardhini, na kwamba Hizb ut Tahrir, ambayo inafanya kazi ulimwenguni kote kama inavyofanya nchini Sudan, inatafuta miongoni mwa Ummah na pamoja nayo ili kurudisha tena maisha ya Kiislamu, ambayo hayatawezekana isipokuwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ama cha kusikitisha na sio kejeli (kama mwandishi alivyo sema), ni mmoja katika watoto wa Umma wa Kiislamu kuzungumzia Khilafah kwa njia hii ambayo haifai, ambayo ni faradhi wakati wa kukosekana kwake, ambayo huweka ufaradhi kwenye shingo yake na shingo ya kila Mwislamu, kama vile Mtume alivyo sema:
«مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ، لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»
“Yeyote mwenye kuuondoa mkono wake katika utiifu, atakutana na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama akiwa hana hoja, na atakaye kufa na hana shingoni mwake ahadi ya utiifu (bay'ah), amekufa kifo cha kijahilia.” (Imepokewa na Muslim).
Nne: Mwandishi haoni chochote kibaya kwa watu wa batili kufanya raha dhidi ya Uislamu, wakilingania batili yao, huku akishangazwa na kubughudhiwa na kazi ya Hizb ut Tahrir, ambayo inataka kuleta pamoja Umma uliogawanywa na mkoloni kafiri katika vijidola vikaragosi dhaifu, wakati Sykes na Picot walipochora mipaka yao na bendera zao, na kisha wakawaweka juu ya waangalizi ambao dhamira yao ni kutekeleza njama za makafiri wa kikoloni kwa gharama ya Umma. Mnahukumu vipi nyie?!
Kwa kumalizia: Tunamwambia mwandishi na wale wote ambao wanakerwa na Uislamu na wabebaji ulinganizi wake: Hakika Khilafah inakuja licha ya kafiri mkoloni na wasaidizi wake katika nchi za Kiislamu kuchukizwa, kwani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) aliye sema:
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao,” [An-Nur: 55] Na ni bishara njema ya mpendwa, Al-Mustafa (saw) ambaye alitoa bishara njema ya kurudi kwake Rashida kwa njia ya utume baada ya utawala wa kiimla tunaoishi ndani yake kwa zaidi ya miaka mia moja, pindi aliposema:
«... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ» ثُمَّ سَكَتَ
“…. Kisha utakuwepo utawala wa kiimla, utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu atataka uwepo kisha atauondoa anapotaka kuundoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha akanyamaza.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |