Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 6 Rabi' II 1442 | Na: HTS 1442 / 32 |
M. Jumamosi, 21 Novemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mapendekezo ya Kongamano Jumuishi Mjini Al-Gadharif!
(Imetafsiriwa)
Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya Kongamano Jumuishi la Wakuu wa Makabila, Viongozi, na Wanachuoni Mashariki mwa Sudan katika Mji wa Gadharif, leo, Jumamosi tarehe 21/11/2020 M, ambapo nyaraka nne ziliwasilishwa, kisha sakafu kufunguliwa kwa michangio ya wahudhuriaji waheshimiwa, na kongamano hilo lilihitimisha yafuatayo:
1- Itikadi (Aqeeda) ya Kiisilamu ndio msingi wa maisha na juu ya msingi wake, na yanayotokana nayo katika hukmu ndio pekee ambayo watu lazima wayaregelee wakati wa kusuluhisha mizozo baina yao, kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Muungu Mwenyezi (swt):
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]
“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema. ” ]An-Nisa: 59[. Na kauli yake (swt):
[وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ]
“Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye narejea.” [Ash-Shura: 10].
2- Uwepo wa watu katika makabila tofauti tofauti ni alama miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu (swt), kujuana na kuunga kizazi, Mungu Mwenyezi (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ]
“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Al-Hujurat: 13[.
3- Kufanya kazi kumaliza wazo la miungano kwa misingi ya kikabila au kikanda na kupiga vita matakwa ya mamlaka na utajiri kwa misingi ya kabila na eneo, na ni juu ya wakuu na viongozi kuwaongoza watu katika wema, ili wawe viongozi wa kimungu, kama walivyokuwa wakuu na viongozi wa makabila katika vizazi vyetu vya mwanzo. Tunaye Abu Dhar al-Ghifari, Saad bin Muadh na wengineo miongoni mwa watangulizi wema, Mwenyezi Mungu awawie radhi, ni kiigizo na mfano mzuri.
4- Mfumo wa serikali katika Uislamu: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ndio mfumo pekee unaohakikisha kushibisha mahitaji ya kimsingi ya kila raia binafsi binafsi; katika upande wa chakula, mavazi na makaazi, kama inavyodhamini usalama, matibabu na elimu kwa jamii, na inasonga mbele kutoa mahitaji ya ziada kwa kadri inavyowezekana, na hivyo kutoa maisha salama na ya utulivu kwa wote.
5- Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ndio dola pekee inayoweza kuyafinyanga makabila, watu na mataifa ndani ya chungu kimoja. Hivi ndivyo ilivyofanya hapo zamani, kwa hivyo Waarabu, Waajemi, Waturuki, Waafrika, na wengine walikuwa ndugu wapenzi, ambao hawaliunganishwa na La Ilaha Illa Allah, na walichunga mambo yao kwa hukmu za Mola wa Walimwengu wote. Na leo pindi Khilafah itakaposimama hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), itakuwa na uwezo wa kufanya hivyo, hadi ifanikisha mshikamano imara kwa kamba ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً وَكُنتُمْ عَلَى شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [Al-i-Imran: 103]
6- Kufanya kazi kuiregesha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ni faradhi kwa Waislamu kufanya kazi kuurejesha, kwa hivyo kila mtu lazima afanye kazi kwa sababu ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu, kwa kufanya kazi ya kuiregesha, na kishajiisho cha hilo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) pindi aliposema:
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55] Na vilevile ni bishara njema ya Mtume (saw) pindi aliposema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”
7- Sudan inamiliki utajiri unaowafanya watu wake kuwa matajiri, lakini kwa bahati mbaya, wanasiasa wanafikiria tu ndani ya mfuko wa mfumo wa kirasilimali ambao unaufanya utajiri wa Sudan kuwa kinyang'anyiro cha makafiri wakoloni, na utajiri huu hautazungushwa kwa ajili ya maslahi ya watu wa Sudan isipokuwa kwa dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee.
8- Ukumbusho wa utakatifu wa mali, heshima na damu, haswa damu ya Muislamu, na ni juu ya viongozi na wakuu wa makabila kufanya kazi kuwaelimisha wafuasi wao na kuwakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu:
[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]
“But whoever kills a believer intentionally - his recompense is Hell, wherein he will abide eternally, and Allah has become angry with him and has cursed him and has prepared for him a great punishment”]An-Nisa: 93[. Na maneno ya Mtume (saw):
«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ»
“Kuangamia kwa dunia ni sahali mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kumuua Muislamu mmoja.” Na maneno yake (saw):
«لَوْ أَجْمَعَ أَهْلُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَلَى قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ، لَأَكَبَّهُمُ اللَّهُ فِي النَّارِ»
“Lau wakaazi wa mbinguni na ardhini watajumuika katika kumuua Muislamu mmoja, Mwenyezi Mungu atawasweka Motoni.”
Na maneno yake (saw):
«مَنْ أَعَانَ عَلَى قَتْلِ مُسْلِمٍ وَلَوْ بِشَطْرِ كَلِمَةٍ، جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَكْتُوبٌ بَيْنَ عَيْنَيْهِ: آيِسٌ مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ»
“Yeyote anayesaidia katika kumuua Muislamu hata kama ni kwa kipande cha neno, atakuja Siku ya Kiyama huku akiwa ameandikwa baina ya macho yake: 'Mkosefu wa tamaa na rehma za Mwenyezi Mungu (swt).”
9- Wanakongamano walipendekeza kusimamishwa kwa hukmu ya Sharia; Kisasi kwa wale waliomwaga damu kinyume cha sheria, na fidia ya uharibifu kwa wale waliosibiwa katika mali zao, au katika makaazi yao, au kitu kingine chochote.
Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |