Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 6 Muharram 1442 | Na: HTS 1442 / 04 |
M. Jumanne, 25 Agosti 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Yaandaa Kisimamo cha Kupinga Dhidi ya ziara ya Waziri wa Kigeni wa Amerika nchini Sudan
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa kisimamo cha kupinga, mchana wa siku ya Jumanne, 6 Muharram 1442 H sawia na 25/8/2020 M katikati mwa mji mkuu wa Khartoum, umbali wa mita chache tu kutoka Ikulu ya Jamhuri, kukataa ziara ya Waziri wa Kigeni wa Amerika Pompeo, na mashababu wa Hizb waliinua mabango yaliyo andikwa:
1. Aibu iwe juu yenu, enyi watawala, kwa kugusa mkono wa Pompeo unachuruzika damu ya ndugu zenu Waislamu.
2. Hapana kwa usaliti kwa Ummah; kupitia usawazishaji wa mahusiano na umbile la Kiyahudi.
3. Hakuna kinachostahili kwa umbile la Kiyahudi ila upanga; na hadi katika kaburi la sahau makubaliano yote ya kiusaliti na watawala vibaraka.
4. Serikali ya mpito, Pompeo na umbile la Kiyahudi: "Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao" [Al-Maidah: 52]
1. Serikali ya mpito na watawala wote vibaraka wa Waislamu, kila wanapomaliza usaliti mmoja wanakwenda kwa mwingine, na hakuna litakalo komesha hilo isipokuwa Khilafah Rashida.
2. Palestina ni Ardhi ya Kiislamu iliyo barikiwa, na ni wajibu juu ya Waislamu wote kufanya kazi ya kuikomboa; kupitia kusimamisha Khilafah Rashida.
3. Suluhisho la dola mbili na mpango wa karne ni miradi ya khiyana inayotekelezwa na watawala vibaraka wa Waislamu, na hairuhusiwi kwa Waislamu kunyamazia kimya juu ya khiyana yao.
4. Enyi watu wa Sudan, msikosee kwa kuiruhusu serikali ya mpito ifuate njia ya usaliti kwa kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi.
5. Kusawazisha mahusiano kwa watawala vibaraka na umbile la Kiyahudi ni kusawazisha mahusiano ya mtumishi na bwana wake, na Ummah wa Kiislamu uko mbali na hilo.
6. Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina iko kwenye miadi ya ukombozi, chini ya kivuli cha Dola ya Waislamu Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.
7. Simama Pompeo! Hapana, hukaribishwi, ewe ambaye umejaa damu ya Waislamu, dalali wa kuuza ardhi zao kwa umbile la Kiyahudi, hakuna unachostahiki wewe wala wao isipokuwa upanga.
Ustadh Muhammad Jameh (Abu Ayman), msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, aliwasilisha wakati wa kisimamo hiki kalima aliyoweka wazi ndani yake lengo la kisimamo hiki cha kupinga, na kwamba watawala wa Sudan au wengine miongoni mwa watawala wa Waislamu wanathubutu kuisaliti kwa usaliti kama huu na uhalifu huu mkubwa haki ya Uislamu na Waislamu, lau kama dola ya Waislamu Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume ingekuwepo ingetabikisha Uislamu na kusimamisha hukmu zake, na Abu Ayman akafafanua kwamba kwa kukosekana Khilafah, Ummah unatawaliwa na watawala ambao ni vibaraka wa mkoloni ambao huwasilisha njama zake na kutekeleza ajenda yake; ambapo miongoni mwake ni usawazishaji mahusiano na umbile nyakuzi la Kiyahudi, licha ya ukweli kwamba umbile hili la Kiyahudi bado linaendelea kunyakua ardhi ya Masra; likieneza ufisadi na uharibifu ndani yake, na alihimiza Ummah kuchukua msimamo wa kisheria wa kukataa uhalifu na usaliti wa kusawazisha mahusiano, na kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah ambayo itamaliza uhalifu huu na kukomesha misimamo hii ya fedheha.
Watu walikusanyika karibu na kisimamo hicho, na wapita njia waliokuwa wakipita na magari yao walifanya maingiliano kwa takbir na kuinua mikono yao kuunga mkono.
Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |