Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Wanazuoni katika Jimbo la White Nile
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jana, Jumatatu, tarehe 8/9/2025, huko Rabak, mji mkuu wa Jimbo la White Nile, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ulikutana na Sheikh Abdullah Al-Nur Tutu, Imam na Khatib wa Msikiti Mkuu wa Asalaya na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Wanazuoni wa Sudan, Tawi la White Nile, nyumbani kwake katika kitongoji cha Asalaya. Ujumbe huo uliongozwa na wafuatao Dkt. Ahmad Mohammad, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, akifuatana na Ustadh Faisal Madani, Abdul Majeed Osman Abu Hajar, na Al-Zein Abdul Rahman, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Mkutano huo ulikuwa sehemu ya kampeni ya Hizb ut Tahrir ya kuzuia kujitenga kwa Darfur.



