Mvua ni Baraka na Rehema, lakini bila Uchungaji imekuwa ni Laana!
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni huzuni na pia inasikitisha kwamba msimu wa mvua hauji kwa ghafla, bali ni kipindi cha taarifa ambacho hurudiwa kila mwaka. Kinachoshangaza zaidi ni kwamba vituo vingi vya uchunguzi wa hali ya hewa vilionya kuhusu mvua kubwa, lakini asasi za serikali hazikuchukua hatua yoyote kuzuia madhara yake, ambayo yalikuwa mabaya zaidi kwa vijiji vya Jimbo la Mto Nile, mashariki mwa Sudan na hata Kordofan, miongoni mwa kwengine.