Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Muharram 1446 Na: 1446 / 04
M.  Ijumaa, 02 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umbile la Mayahudi wa Kizayuni Linakiuka Matukufu Yetu Lipendavyo, Huku Watawala wa Waislamu Wakiyafungia Majeshi Yetu kwenye Kambi Zao

(Imetafsiriwa)

Mnamo asubuhi ya tarehe 31 Julai 2024, umbile la Kiyahudi lilimuua shahidi kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulizi la kombora jijini Tehran, mji mkuu wa Iran. Siku moja kabla, umbile hilo la Kiyahudi lilimuua shahidi kamanda wa Hezbollah kwa kushambulia jengo la makaazi jijini Beirut, Lebanon. Hapo awali, umbile la Kiyahudi lilishambulia vituo mbalimbali katika bandari ya Hodeida nchini Yemen kwa ndege za kivita. Hii ni huku Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ikiwa imegeuzwa kuwa magofu katika kipindi cha miezi kumi iliyopita, ambapo makadirio ya kupoteza maisha sasa yamefikia karibu laki mbili. Kwa hivyo ni sababu gani inayofanya kwamba mipaka ya kitaifa iwe haina maana yoyote kwa umbile la Kiyahudi? Umbile hilo linazurura popote linapotaka, linawaua shahidi Waislamu, linamwaga damu, na linanajisi matukufu. Hata hivyo, pindi wito unapotolewa wa kuhamasisha majeshi ya Waislamu, watawala wa Waislamu wanakataa kufikiri nje ya mipaka ya kitaifa. Wameyazuia majeshi yetu yenye uwezo mkubwa ndani ya kambi zao!

Mwenyezi Mungu (swt) aikubali shahada Ismail Haniyeh. Yeye sio shahidi wa kwanza wa vita hivi, wala sio wa mwisho. Shahada ni matamanio ya kila Muislamu na ushindi mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Hata hivyo, sasa kupuuzwa na dhambi zimevuka mipaka yote. Uongozi wa kijeshi na kisiasa unakataa kupeleka vikosi vyetu vyenye uwezo katika mipaka ya kitaifa ili kuwatetea Waislamu kwa vyovyote vile. Watakataa hata kama Mwenyezi Mungu (swt) aepushie mbali, al-Masjid Al-Aqsa itavunjwa, al-Makkah al-Mukarramah na al-Madinah al-Munnawara itashambuliwa, mamilioni ya Waislamu watauawa shahidi na kukiukwa matukufu mengine. Watawala wameweka wazi dhambi la kutotenda kwao. Kwa hivyo, Enyi Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan! Sasa jambo hili liko mikononi mwenu. Ni ujinga kutarajia hatua yoyote ya heshima kutoka kwa watawala hawa. Mistari yote mekundu imevuka. Sasa munapaswa kuamua msimamo wenu. Je, mtasimama pamoja na watawala hawa, au pamoja na Ummah? Mkisonga mbele pamoja na Ummah, Waislamu Waarabu na Wasiokuwa Waarabu watatoa kafara damu zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) badala yenu. Waislamu wote watasimama nanyi mtakapobomoa makasri ya watawala hawa. Hawatawaacha watoroke, wakiwahesabu kwa uhalifu wao wote. Zaidi ya yote, Mwenyezi Mungu (swt) atakuwa pamoja nawe. Amesema Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya Qur’an Tukufu,

[إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلآئِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُواْ الَّذِينَ آمَنُواْ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُواْ الرَّعْبَ فَاضْرِبُواْ فَوْقَ الأَعْنَاقِ وَاضْرِبُواْ مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ]

“Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.’” [Surah Al-Anfal 8:12]. Lakini mkiendelea kuwatii watawala hawa wanapokuamrisheni kumuasi Mwenyezi Mungu, basi Siku ya Kiyama mtafuatana nao Motoni,

[وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا * رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا]

“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa.” [Surah Al-Ahzab, 67-68].

Kwa hivyo, Enyi Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan! Kutotenda kwenu kumewafanya Waislamu kuwa shabaha ya makafiri. Kutotenda kwenu ni kualika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, ambayo hapana pa kuiepuka. Kwa kushirikiana na watawala vibaraka, Magharibi imekufungieni ndani ya mipaka ya kitaifa. Imeyafanya majeshi kuwa walinzi tu wa vibaraka wa wakoloni katika ardhi za Waislamu. Imeyashirikisha majeshi ya Waislamu katika vita na Waislamu. Vibaraka wa wakoloni wanayachoma majeshi katika vita vya Fitna kati ya Waislamu, huku watu waoga zaidi kuliko watu wote, Mayahudi, wanakiuka damu na heshima ya kaka na dada zetu. Lazima muchukue hatua mara moja. Muwaondoe watawala hawa wahalifu. Ni lazima mutoe ahadi ya utiifu (Ba’yah) ya Nusrah kwa uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. InshaAllah, itakuwa ni Amiri wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, ambaye atakuhamasisheni katika Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Khalifa Rashid atawawajibisha Mayahudi kwa uovu wao nchini Syria, Lebanon, Yemen, Iran, na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Khilafah Rashida ndiyo itakayounganisha Ummah mzima wa Kiislamu tena kama dola moja yenye nguvu. Kwa hivyo Enyi Majeshi ya Pakistan, jitokezeni!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu