Jumanne, 07 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Sha'aban 1445 Na: 1445 / 36
M.  Jumatano, 06 Machi 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Mpya ya Pakistan Itaisagasaga Pakistan kwa Baraka za Marekani na Vibaraka wake katika Uongozi wa Kijeshi wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 4 Machi 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema, “Pakistan ya kidemokrasia ni muhimu kwa maslahi katika ya Marekani na Pakistan, na ushirikiano wetu na Waziri Mkuu mpya Shehbaz Sharif na serikali yake utaendelea kuzingatia kuendeleza maslahi haya ya pamoja.” Kwa hivyo, Marekani inasalia katika udhibiti kamili wa Pakistan kupitia vibaraka wake katika uongozi wa kijeshi. Pakistan itakandamizwa kiuchumi na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), ikiwa na malipo makubwa ya riba, kutoza ushuru na mfumko wa bei unaolemaza. Pakistan itadhalilishwa kuhusiana na usalama wake, kupitia kusawazisha mahusiano na Dola ya Kibaniani, ili kuhakikisha utawala wa kitamaduni, kiuchumi na kijeshi wa kikanda wa India. Serikali hii mpya ni sawa na kila serikali tangu Marekani ilipopata vibaraka ndani ya uongozi wa kijeshi. Mistari mekundu ya serikali mpya ni kuasi amri za Marekani, na mzozo na watawala halisi wa nchi hii, kundi teule la majenerali wafisadi sana ambao wameiuza nchi na Akhera yao, kwa ajili ya Dunia yao.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Sasa tunajua maana kamili ya maneno “Toa heshima kwa kura.” Upigaji kura katika demokrasia ni kuruhusu tu kuendelea kwa ukoloni wa Marekani nchini Pakistan. Hakuna matumaini ya mabadiliko kupitia Demokrasia. Kufeli kwa dhahiri kwa “kura ya kulaani” ni ushahidi wa wazi wa hilo. Hakutakuwa na mabadiliko maadamu tunatawaliwa na Demokrasia. Hakutakuwa na mabadiliko maadamu kuna vibaraka katika jeshi, wanaochagua kwa uangalifu viongozi wa kisiasa ambao wataungana nao katika uhaini na usaliti. Kuhusu kukimbia nchi, sio suluhisho kwa watu milioni 250. Kwa hivyo, tuwe wazi juu ya njia ya mabadiliko. Mabadiliko yanatokana na kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Mabadiliko ni kwa wale wanaofanya kazi ya kuhukumu kwa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Mabadiliko ni kwa kupata msaada wa kimada kutoka kwa watu wenye nguvu kwa ajili ya Dini. Hebu natuondoe huzuni zetu na kuzingatia njia ya mabadiliko. Kila mmoja wetu lazima awatake watoto wetu katika jeshi wang'oe wasaliti katika uongozi wao na waipe Nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan!

Pakistan inasumbuliwa na uongozi fisadi wa kijeshi kwa miongo kadhaa sasa, kama ilivyo kwa Umma wote wa Kiislamu. Tazameni hali ya watu mlioapa kuwalinda. Tazameni hali ya Umma wa Muhammad (saw) kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amekukirimuni, kwa kuwa sehemu yake. Wakati munasubiri amri ambazo kamwe hazitakuja, Umma wa Kiislamu unakandamizwa na kudhalilishwa na maadui zake. Vita vimeanza na bado hamjajiunga navyo. Sio wakati wa kuchambua au kutabiri yajayo. Sio wakati wa kujiuzulu au kupanga kustaafu. Ni wakati wa kutenda kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Ondoeni kutotenda kwenu na songeni kwa kufuata nyayo za Answaar (ra) waliomnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Ni Answaar (ra) ndio viigizo wachamungu kwa maafisa wa kijeshi wanyoofu wanaoogopa kukutana na Mwenyezi Mungu (swt). Answaar (ra) walifanya biashara ya Dunia hii kwa ajili ya Akhera kwa kutoa Nusrah (msaada wao wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha hukmu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Lazima ufanye vivyo hivyo. Answaar walipigana na majeshi ya madhalimu, kwa nia moja ya kutafuta ushindi na shahada. Mtapata fursa kwa ajili hiyo hiyo, chini ya Khilafah kwa Njia ya Utume, inshaaAllah.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Majeshi yao!

Kuna ombwe kubwa la kisiasa katika Ulimwengu wa Kiislamu, lakini hakuna ukosefu wa uongozi unaostahili kuziba ombwe hilo. Tangu mwaka 1953, Hizb ut Tahrir imefanya kazi bila kuchoka katika Ulimwengu wote wa Kiislamu, na ndani ya makundi yote ya watu, ndani ya kila nchi. Katika muda wote huu na katika sehemu zote hizo, Hizb ut Tahrir daima imekuwa kiongozo mwenye utambuzi na mkweli, kamwe asiyepotosha kwa upotofu. Imevua rai zake zote za kisiasa kutoka kwa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Mashababu wake wamejitolea mhanga kwa khiyari kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), bila kumuogopa yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt), wakipata manyanyaso, mateso, kufungwa jela, kutekwa nyara, kuteswa na kuuawa kwa mikono ya madhalimu. Hebu na tushirikiane na Hizb ut Tahrir kuiregesha Dini yetu nzuri kwenye nafasi yake inayostahiki, katika utawala na mamlaka kama kielelezo chema kwa wanadamu wote. Hakika matendo hayo ya mema yamechelewa sana. Imepita miaka mia moja tangu Khilafah ilipovunjwa na wakoloni na vibaraka wao miongoni mwa Waarabu na Waturuki. Ramadhan hii, mwezi wa ushindi, inatupata katika wakati ambapo Umma unateseka sana, na Gaza Hashem kwenye kilele cha mateso hayo. Kwa nini Pakistan isiwe ya kwanza kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na kutoa afueni kwa Ummah? Hebu na tuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu (swt), na Yeye (swt) atatunusuru. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ * ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” [Surah Muhammad 47:7-9].

Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu